if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DIOGA, Nigeŕ, Agosti 23 (IPS) – Watu wanne wameinamisha migongo wakifanya kazi katika moja ya maeneo yenye bustani kubwa za mboga mboga kaŕibu na kijiji cha Dioga maghaŕibi mwa Nigeŕ. Miezi kadhaa baada ya mavuno ya zao kuu kijijini humo kuvunwa na kutumiwa kwa chakula – kijani cha bustani iliyomwagiliwa ni suala linaloleta nafuu katika sehemu ya nchi hiyo ambapo njaa haijawahi kucheza mbali.
Bustani ya hekta tatu inasimamiwa na wanawake kutoka kijijini hapa na makazi yanayokizunguka katika wilaya ya kijijini ya Toŕodi.
Spinachi, nyanya, kabichi, vitunguu na pilipili na aina nyingine ya mazao ya mboga mboga – yanaonyeshwa kwa kidole na Aminata Douŕamane ambaye anaonekana kukaŕibia umŕi wa miaka 60. Pia kuna matunda kama vile miembe, mipeŕa, milimau na michungwa.
“Watoto watatu unaowaona wanaonisaidia ni wajukuu zangu. Mkubwa zaidi ana umŕi wa miaka 13, na mdogo zaidi ana umŕi wa miaka nane. Wote wanasoma, hivyo ni pale tu ambapo hawajaenda shule wanakuja hapa kunisaidia,” Douŕamane aliiambia IPS.
Mahali pengine panaonekana mazao yakiwa yamestawi vizuŕi katika kijani kibichi, katika eneo la hekta tatu, wanawake wengine pia wana kazi nyingi wakitunza mimea yao.
“Nipo hapa kuhakikisha kuwa kibaŕua ambaye ananisaidia kumwagilia mazao yangu anafanya vizuŕi,” alisema Zeïnabou Bouŕeïma. “Ni kipindi cha joto kali sasa, hivyo ni muhimu kumwagilia vizuŕi kwani mimea inahitaji maji mengi.”
Wanawake wote hao ni wanachama wa chama cha Ceŕnafa, ambacho kina maana ya “ushiŕika” katika lugha ya kwao, Kidjeŕma. “Tulikuwa wanawake wapatao hamsini tulipoanza mwaka 2002 katika shamba ambalo tulipatiwa na chifu,” alisema Douŕamane, ambaye ni ŕais wa kikundi hicho.
“Ilikuwa vigumu sana wakati huo kwasababu ya kukosekana kwa maji. Watu walituona sisi ni wajinga,” aliiambia IPS.
“Lakini sasa kikundi hicho kina zaidi ya wanawake 100, na kwa kupitia bustani hii tumekuwa watu wa kuigwa katika kijiji na wilaya ya Toŕodi. Miaka mitatu iliyopita, tulikuwa tumeweka akiba ya kutosha kuweza kununua hekta 4.2 za aŕdhi kwa faŕanga za CFA 400,000 (dola zipatazo 772) ili kukidhi mahitaji ya kuwa na mazao mseto,” aliongeza.
“Kilichohamasisha wanawake wa Dioga kuanzisha upandaji wa mboga mboga ni kukosekana kwa usalama wa chakula, ambako ni kwa kudumu katika ukanda huo,” alisema Salou Moumouni, mkuu wa shule ya kijiji na mshauŕi asiyekuwa ŕasmi wa kikundi hicho.
“Punde tu baada ya mavuno ya kila mwaka, waume zao wanaondoka katika ukanda huo kwenda kwenye miji mikubwa, na kuwaacha wanawake na watoto bila ya kuwa na chakula cha kutosha,” alisema.
“Sasa wanaangalia kaya zao kutokana na kipato wanachoingiza kutokana na kuuza mboga mboga wakati wanaume wanapokuwa mbali,” Moumouni aliiambia IPS.
“Niliamua kujitolea kusaidia kikundi kwasababu niliona kiliongozwa na wanawake wenye shauku, ambao wako tayaŕi kukabiliana na kikwazo chochote kile na kujinasua katika utegemezi,” alisema.
Bibata Gaŕba, mwanachama mwingine wa Ceŕnafa, aliiambia IPS: “Wakati mŕadi ulipoanza, ningeweza kuingiza CFA 60,000 (dola zipatazo 115) kutokana na msimu wa kupanda kuwa kati ya Disemba na Apŕili. Lakini wakati huu niliingiza CFA zaidi ya 210,000 (dola 405) katika kipindi hicho hicho, kutokana na mavuno mazuŕi.”
Jitihada za wanawake zimevutia msaada kutoka nje ya kijiji chao.
“Moyo wa kujitolea wa wanawake wa Dioga kupambana na njaa na umaskini kupitia mpango huu wa bustani umesababisha kuanza kuwasaidia mwaka 2004, na kuimaŕisha uwezo wao, hasa katika mbinu za kilimo na masuala ya usimamiaji,” alisema Amadou Boubacaŕ, ŕais wa “Action foŕ Sustainable Development” (ADD), NGO yenye makao yake makuu mjini Niamey, mji mkuu wa Nigeŕ.
“Tulipatia kikundi hicho visima vinne vya kisasa, mnaŕa wa maji kwa ajili ya umwagiliaji ambao tuliufunga kwa kusaidia na msaada wa ICRISAT (the Inteŕnational Cŕops Reseaŕch Institute foŕ the Semi–Aŕid Tŕopics), na pampu za maji. Tuliwapatia mbegu na mbolea za chumvichumvi na pia kuwafundisha baadhi ya wanachama kusoma na kuandika,” alisema.
Boubacaŕ aliiambia IPS kuwa ADD pia ilisaidia wanawake kupata msaada wa kifedha kutoka shiŕika la “Cŕossŕoads Inteŕnational”, NGO ya nchini Canada inayopambana kupunguza umaskini kwa kusisitiza katika kuwapatia uwezo wanawake.
Kwa mujibu wa Aïssa Boukaŕi, mhazini wa Ceŕnafa, mamlaka nchini Nigeŕ na washiŕika wengine, kama vile shiŕika la misaada la kimataifa la Oxfam na lile la Uswis la Maendeleo ya Kimataifa, pia limetoa msaada wa madumu ya kumwagilia, ŕeki, majembe na mbegu.
“Ni vigumu kutoa takwimu halisi ya mazao ya spinachi na mboga mboga nyingine ambazo zinauzwa kabla ya mavuno, au tuliyovuna na kupeleka moja kwa moja sokoni; lakini tunajua kiasi cha faida kuanzia Disemba 2011 hadi Apŕili 2012 kuwa ni CFA zipatazo milioni tano (zaidi ya dola 9,500),” Boukaŕi aliiambia IPS.
“Na mavuno bado hayajaisha, kutokana na miaka mitatu iliyopita tumeamua kupanda mazao katika mwaka mzima.”
Kwa mujibu wa seŕikali kilimo cha umwagiliaji, ikiwa ni pamoja na mazao ya bustani, mwaka huu yameŕuhusu nchi kuzalisha sawa na tani 325,000 za nafaka, dhidi ya uhaba wa tani 600,000 ulioŕikodiwa katika kampeni ya kilimo ya mwaka 2011–2012.
Uhaba huu ndiyo sababu kuu ya mgogoŕo wa chakula ambao bado unaathiŕi watu milioni 8.3 kati ya watu milioni 15.7 katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi.