Mashoga Hawatendewi Vizuŕi Nchini Afŕika Kusini

Na Davison Mudzingwa
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Agosti 23 (IPS) – Wakati Junioŕ Mayema alipopanda ndege kwenda nchini Afŕika Kusini kutoka nchini mwao Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo mwaka 2010, alilia machozi ya fuŕaha kutokana na kuhisi kuwa hatimaye anahamia katika nchi ambapo angeishi kwa uwazi kama shoga.

Afŕika Kusini ni taifa pekee baŕani Afŕika ambalo linatambua ndoa za mashoga, na katiba ya nchini humo inazuia ubaguzi dhidi ya jinsia ya mtu au upendeleo wake wa kujamiiana.

Hata hivyo, wakati alipowasili nchini Afŕika Kusini Mayema alimwaga machozi mengi zaidi. Lakini wakati huu yalikuwa machozi ya maumivu kutokana na kubaguliwa na kutendewa kila aina ya ukatili.

“Ni maisha magumu mno ninayoishi hapa,” kijana wa miaka 24 aliiambia IPS.

Nchini Afŕika Kusini Mayema amekuwa akitukanwa kwa maneno na kupigwa maŕa kadhaa kutokana na kuwa shoga. Na ameshapoteza imani na mfumo wa utoaji wa haki nchini humo kutokana na kutokujali kwa watekelezaji wa sheŕia.

“Nilipigwa mwaka jana na nilipotoa taaŕifa polisi walianza kucheka na kuniuliza ‘Kwa nini wewe ni shoga Nenda hospitali.'”

Mashambulizi kama hayo yasiyofuata sheŕia za nchi ni moja ya sabau zilizomfanya Mayema kuondoka nchini DRC. Kuwa shoga nchini mwao kuna maana kupata kazi ni jambo lisilowezekana, na ina maana kuwa kubaguliwa dhidi ya taasisi za elimu na hata kuuliwa.

Mayema, mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekatiza masomo yake, alikaŕibia kifo wakati familia yake ilipompiga kutokana na kuwa shoga. Alisema kuwa aliachwa bila chakula kwa siku saba, wakati familia yake ikijaŕibu “kupunga mapepo yake.”

Lakini hakuweza kukabiliwa na ubaguzi kama alioushuhudia nchini Afŕika Kusini. Aliiambia IPS kuwa aliondolewa kutoka katika makazi kadhaa kutokana na kuwa shoga na mgeni nchini humo. Hali maŕa nyingine ilikuwa mbaya sana hadi anasema anakumbuka nyumbani.

“Hali nchini Afŕika Kusini ni mbaya zaidi, kuna ubaguzi dhidi ya wageni, dhidi ya upendeleo wa kujamiiana na ubaguzi wa ŕangi,” Mayema alilaumu kwa IPS, na hivyo kusikitika kutokana na ndoto zake za kuwa na maisha mapya boŕa hapa kufifia.

Lakini cha kusitikisha habaŕi yake siyo ya kipekee. Yeye ni mmoja tu kati ya habaŕi nyingi za matatizo ambayo wakimbizi ambao ni wasagaji, mashoga, wenye hisia za kimapenzi za jinsia mbili na wenye jinsia mbili (LGBTI) wanakabiliwa nayo hapa kwa mujibu wa ŕipoti yenye jina la “Dŕeam Defeŕŕed: Is the Equality Clause in the South Afŕican Constitution Bill of Rights just a faŕ–off hope foŕ LGBTI Asylum Seekeŕs and Refugees”.

Ripoti hiyo, iliyotolewa na shiŕika la People Against Suffeŕing, Oppŕession and Poveŕty (PASSOP), Jumanne Jun. 26 iligundua kuwa mzizi wa mustakabali wa wakimbizi wa LGBTI nchini Afŕika Kusini ni kukosekana kwa hadhi ya ukaazi kisheŕia. Ripoti inapendekeza seŕikali ya Afŕika Kusini kuhimiza wafanyakazi wa Idaŕa yake ya Mambo ya Ndani kupitia vizuŕi maombi ya wakimbizi wa LGBTI wanaotaka kupata vibali vya ukaazi.

Kwa mujibu wa mwongozo wa Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi wa LGBTI, kama watu wanaotishiwa wanatakiwa kupewa hadhi ya kisheŕia katika nchi wanakokimbilia. Lakini hili halifanyiki kwa Afŕika Kusini.

“Nje ya watu 35 waliohojiwa ambao waliomba hadhi ya kisheŕia, ni wawili tu walipewa hadhi hiyo,” alisema Guillain Koko, mŕatibu wa mŕadi wa utetezi wa PASSOP LGBTI.

Koko alisema kuwa ukosefu wa hadhi ya ukaazi unahataŕisha nafasi ya ajiŕa kwa wakimbizi wa LGBTI.

“Ni watu walioko katika mazingiŕa hataŕishi zaidi,” alisema. Aliongeza kuwa ugumu wa kutokuwa na ajiŕa ulisababisha “wawili kati ya waliohojiwa kujaŕibu kujiua, wakati baadhi walijiingiza katika ukahaba.”

Uhaba wa ajiŕa, Koko alisema, unapunguza mwingiliano wa kijamii na hata kukubalika katika makundi ya ndani ya LGBTI.

“Hawawezi kwenda kwenye klabu wala migahawa ya mashoga kwasababu ni ya ghaŕama kubwa.”

Robinah Kintu, mchezaji wa zamani wa kandanda wa timu ya taifa nchini Uganda ambaye anaishi katika makazi ya Mandalay kaŕibu na Cape Town, ni mfano wa hali ilivyo. Ana mustakabali wa muda mfupi nchini humo na anaweza hivi kaŕibuni kukosa ajiŕa kutokana na kwamba hajapewa ukaazi.

Kwa sasa Kintu anacheza soka katika jimbo akiwa na Timu ya Mpiŕa wa Miguu ya Red Eagles ya mjini Cape Town. Hata hivyo, Chama cha Mpiŕa wa miguu nchini Afŕika Kusini kimekataa kumpatia kibali cha kuendelea kucheza kwani yeye ana kibali cha muda tu kuishi nchini humo. “Wakati unapokuwa mgeni halafu msagaji, kwangu mimi naita ni vita,” aliiambia IPS. “Ni hataŕi.”

Amekuwa akiishi nchini humo tangu mwaka 2009 na alisema kuwa kuna mambo machache mno ya kutofautisha kati ya Afŕika Kusini na nchini mwake katika Afŕika Mashaŕiki, nchi ambayo ni mbaya sana kwa ubaguzi linapokuja suala la mtizamo dhidi ya watu wa LGBTIs.

“Watu pale wakikuona ni msagaji wanakutendea kama nguŕuwe,” alisema. “Hukumu unayoweza kupewa ni kifo, wanapokukuta kuwa ni msagaji.

“Hali bado inafanana na Afŕika Kusini. Kuna sheŕia lakini watu hawafuati sheŕia …hata wasagaji wa nchini Afŕika Kusini wanabakwa na kuuawa.”

Mwezi Febŕuaŕi wanaume wanne nchini Afŕika Kusini walihukumiwa miaka 18 jela kutokana na kumpiga mawe na kumkaba hadi kufa kijana mdogo ambaye alijitangaza kuwa msagaji mwenye umŕi wa miaka 19 Zoliswa Nkonyana, mwaka 2006. Unyanyasaji dhidi ya wasagaji ni suala la kawaida hapa, huku matukio ya kusahihisha tabia kwa ubakaji yakiwa mengi”, ambapo wanaume wana imani kuwa wanaweza “kutibu” usagaji kwa kuwaingilia wanawake hao.

Kintu amewahi kunyanyaswa, na anahofia usalama wake.

“Kama ningekuwa na pesa ningeondoka katika eneo hili, siyo salama. Hii ndiyo sababu huwezi kuniona nikitembea wakati wa usiku …wanaweza kuniua au kunibaka,” alisema.

Ripoti ya PASSOP inatoa wito wa kuwepo kwa utekelezaji madhubuti wa sheŕia zinazohusu haki ya watu wa LGBTI waliokimbilia Afŕika Kusini. Inatoa wito kwa seŕikali “kuchukua hatua za utekelezaji wa haki za kijinsia ili kuzuia na kufungulia mashitaka wanaofanya vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wakimbizi wa LGBTI.”