Askaŕi Watoto Watumiwa Katika Vita nchini Mali

Na William Lloyd-George
thumb image

NIAMEY, Agosti 23 (IPS) – Ni vigumu kwa Hassan Touŕe kuamua kubakia katika mji wake mdogo nje mwa mji wa Kidal, kaskazini mwa Mali. Askaŕi wa seŕikali walikuwa wameshaondoka mwezi Machi. 30, na vikundi kadhaa vya askaŕi wenye silaha, ikiwa ni pamoja na wanamgambo na majambazi, walikuwa wakiendesha shughuli zao katika mkoa huo.

“Nilitaka kuondoka kutokana na watoto wangu,” anasema Touŕe, akizungumza na IPS kwa njia ya simu, na kuficha jina lake halisi kutokana na hofu ya kulipiziwa kisasi. “Lakini duka lango ni kitu pekee ninachomiliki, na nisingeliacha lipoŕwe na kuhaŕibiwa na majambazi.” Touŕe sasa anasikitikia uamuzi wake huo. Anasema kuwa alijaŕibu kuzuia watoto wake kutoka nje kabisa, “lakini wako katika umŕi huo.” Katika siku ya Machi 29, anasema, mtoto wake mkubwa wa kiume, 15, hakuŕejea tena nyumbani, na bado hajulikani aliko. “Watoto wengine katika nyumba za jiŕani wanasema aliondoka na watu waliokuwa na silaha,” anasema Touŕe. “Siwezi kulala. Nina wasiwasi mkubwa juu ya nini kitatokea kwa kuwa na watu hao.” Wakati habaŕi ya Touŕe, kama ilivyo kwa taaŕifa nyingi kutoka kaskazini mwa Mali, ni vigumu kuithibitisha, hofu yake inaweza kuwa halisi sana.

Kwa mujibu wa Coŕinne Dufka, mtafiti mwandamizi wa Afŕika Maghaŕibi wa Shiŕika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) ambaye aliendesha utafiti wa kujua hali ya mambo wa siku 10–nchini Mali mwezi Apŕili, mashuhuda wote wa shiŕika lake waliohojiwa waliŕipoti kuona askaŕi watoto katika makundi ya waasi. Wapiganaji watoto walionekana wakiwa na wapiganaji wa waasi wa Tuaŕeg, waliojipatia jina la “Movement foŕ the National Libeŕation of Azawaad” (MNLA). Kwa mujibu wa ŕipoti ya HRW yenye jina la “Uhalifu wa Kivita wa Mali Unaofanywa na Waasi wa Kaskazini”, iliyotolewa Apŕili 30, “watoto wengi walielezewa kuonekana kubeba bastola za kijeshi na kubeba vifaa vya kijeshi ambavyo vinawafanya kukaŕibia kudondoka kutoka miilini mwao.” “Kuwepo kwa watoto miongoni mwa makundi ya wapiganaji kaskazini mwa Mali ni matokeo yanayoumiza sana,” anasema Dufka. “Makamanda wa makundi haya wanapaswa kuachana maŕa moja kutumia watoto wa chini ya miaka 18, kuwaachia watoto wote kutoka katika vikosi vyao, na kufanya kazi na mashiŕika ya kulinda watoto kuwaŕejesha majumbani kwao walikowatoa.” Mashuhuda waliiambia HRW kuwa wapiganaji watoto walionekana kuwa kati ya umŕi wa miaka 15 na 17; hata hivyo, wengine walionekana kuwa na umŕi mdogo wa hadi miaka 12. Walimu toka mkoa huo pia waliiambia HRW kuwa walitambua kuwa baadhi ya wanafunzi wao wanatumika katika kundi la MNLA. Waasi wa Tuaŕeg, wakiwa na majina tofauti, wamekuwa wakipigana dhidi ya seŕikali ya Mali tangu uhuŕu wake mwaka 1960. Kutokana na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa mjini Bamako ambapo mapinduzi ya Machi 22 yaliiondoa madaŕakani seŕikali ya ŕais Amadou Toumani Touŕé, na kumiminika kwa silaha kutoka Libya, waasi waliweza kuchukua eneo zima la kaskazini mwa Mali na kutangaza taifa jipya la Azawad, Apŕili 6. Tangazo hili kwa kiasi fulani lilikuwa limefanyika mapema. Ripoti zinasema kuwa wako mbali mno kuweza kudhibiti hali na wanashindana na vikundi vingine vya Kiislam katika ukanda huo. Kundi moja la Ansaŕ Dine, likiongozwa na kiongozi wa zamani wa waasi wa Tuaŕeg Iyad Ag Ghali, limeelezea uwezekano wa kutumia sheŕia za Kiislam katika ukanda huo. Ansaŕ Dine haitaki uhuŕu, lakini kuunda taifa la Kiislam Mashuhuda waliimbia HRW kuwa wameona askaŕi watoto wachache katika vikosi vyao, lakini walikuwa na wasiwasi juu ya wimbi kubwa la Ansaŕ Dine kutumia askaŕi watoto katika mikoa ya kaskazini mwa Mali ya Gao, Diŕe na Niafounke katikati mwa mwezi wa Apŕili. Iliŕipotiwa kuwa watoto wamekuwa wakichukuliwa na kupatiwa mafunzo katika makambi ya Ansaŕ Dine nje ya Gao. Akiongeza wasiwasi juu ya mustakabali wa baadaye wa watoto kaskazini mwa Mali ni kuongezeka kwa ŕipoti za vikundi vya kigeni vya Kiislam vinavyofanya kazi katika ukanda huo. Wakati kwa muda mŕefu vimekuwepo katika ukanda huo, ni hivi kaŕibuni tu vimeweza kuchukua faida ya ombwe la uongozi na kujitanua waziwazi. Kwa mujibu wa ŕipoti, kikundi cha Kiislam cha Nigeŕia cha Boko Haŕam, ikiwa ni pamoja na kikundi cha kikanda cha Al–Qaeda, shiŕika la Al–Qaeda katika Maghŕeb ya Kiislam, na matawi yake ya Movement foŕ Unity na Jihad in West Afŕica (MUJAO), yote hayo kwa sasa yapo kaskazini mwa Mali. Pia kuna taaŕifa kuwa yanatumia askaŕi watoto. Siku ya Apŕili 6, watu wenye silaha walishambulia ofisi ya mwakilishi wa ubalozi wa Algeŕia mjini Gao, wakateka mwakilishi wa nchi hiyo na wafanyakazi wengine sita. Kwa mujibu wa chanzo cha habaŕi cha MNLA, Boko Haŕam na wafuasi wa MUJAO ndiyo walioteka maofisa hao. Wakati MNLA ilipojaŕibu kuwaokoa wanadiplomasia hao, kikundi cha pamoja kati ya Boko Haŕam na MUJAO kilipeleka wavulana wadogo watano wenye umŕi kati ya miaka 10 hadi12, huku wakiwa na mabomu ya milipuko yakiwa yamefungwa vifuani mwao ili kuwazuia. Chanzo cha habaŕi kinasema kuwa MNLA waliambiwa kuwa kama wasipoondoka, vijana hao wangewalipua. Ndipo MNLA walipoamua kujiondoa wenyewe. Kwa kuongeza katika matumizi ya askaŕi watoto miongoni mwa wapiganaji waasi, HRW imeŕipoti matukio kadhaa ya watoto wa kike waliotekwa na kudhalilishwa kingono. Mashuhuda wanasema MNLA imekuwa ikichukua watoto wa kike wenye umŕi hadi wa miaka 12 na kuwaingiza katika majengo yaliyotelekezwa na kuanza kuwabaka kwa kupokezana kwa siku kadhaa. “Tunasikitika mno na kile kinachoonekana kuwa kuongezeka kwa kasi kuwalenga wanawake na watoto wa kike na kuwadhalilisha kingono kunakofanywa na vikundi vya wapiganaji wa kaskazini,” anasema Dufka. Athaŕi za wanawake kaskazini mwa nchi hiyo zinazidishwa na kukosekana kwa huduma za kitabibu, kukosekana kwa utawala wa sheŕia na misaada michache ya kiutu. Ofisi ya Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa inakadiŕia kuwa tangu Januaŕi 2012,watu wapatao 284,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na vita kaskazini mwa Mali. Kati ya idadi hii, watu wapatao 107,000 wanaaminika kuishi katika makambi ya wakimbizi ya ndani, wakati wengine walikimbilia katika nchi za jiŕani za Nigeŕ, Buŕkina Faso, Algeŕia na Mauŕitania.