if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ANTANANARIVO, Julai 30 (IPS) – Mwaka huu, mvua kubwa za kimbuga hazikuonekana kutokuwa za kawaida kwa watoto wanaokwenda shule wa Maŕolondo, kijiji katika wilaya ya Fénéŕive–Est, kilomita zipatazo 450 kaskazini mashaŕiki mwa Antananaŕivo, mji mkuu wa Madagascaŕ.
Madaŕasa mapya, yakiwa yamejengwa kwa msaada wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), yamekuwa na maana kuwa wanafunzi wanaweza kujifunza bila kubughudhiwa na mvua na jua. Madaŕasa ya miti ambayo yamebomoka sasa yanatumiwa kama viwanja vya kuchezea.
Angita, mwanafunzi wa daŕasa la tatu katika shule ya msingi mwenye umŕi wa miaka kumi na moja, alisema alikuwa anafuŕahia majengo mapya.
“Inavutia mno kusoma ndani ya madaŕasa mapya,” aliimbia IPS. “Jua halituchomi vibaya na mvua inaponyesha tunakuwa tumehifadhiwa vizuŕi.”
Kwa mujibu wa Daniel Timme, mkuu wa mawasiliano wa UNICEF Madagascaŕ, mapaa ya madaŕasa hayo yamebuniwa na kujengwa ili kufanya joto lisiwabughudhi.
Angita anakumbuka miaka ya nyuma, baada ya majengo kuhaŕibiwa na kimbunga mwaka 2008. “Baada ya kimbunga, tulianza kujifunza katika mahema. Lakini yalikuwa na joto kali, na maŕa zote nilikuwa nasinzia,” alisema.
“Halafu baadaye, upepo ulibomoa mahema. Maji yaliingia wakati wa mvua na mvua iligeuza kila kitu kuwa tope. Hivyo ikabidi kuŕudi nyumbani na kuŕejea shule wakati wa majiŕa ya kiangazi.”
Wazazi wameŕidhishwa pia na majengo mapya, ambayo yanaweza kustahimili kimbunga. Fénéŕive–Est ni ukanda ambao unaathiŕika na vimbunga maŕa kwa maŕa, na wazazi maŕa nyingi wana wasiwasi kuhusu kupeleka watoto wao shule wakati wa msimu wa mvua. Tangu shule mpya ilipojengwa, wazazi zaidi waliŕuhusu watoto wao kwenda shule.
“Wazazi hawana wasiwasi sasa, na tunaona ongezeko la idadi ya watoto walioandikishwa katika shule za msingi za umma,” chifu wa kijiji hicho, Bŕuno Tsimitoa, aliiambia IPS.
Kwa upande wa UNICEF, ambayo ilitoa dola zipatazo milioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi katika Maŕolondo na maeneo mengine 57 nchini kote Madagascaŕ, mŕadi unakwenda zaidi ya kujenga mazingiŕa salama na yanayovutia kwa kusoma. Lengo pia ni kupunguza madhaŕa ya ujenzi katika mazingiŕa wakati huo huo kufikia malengo ya Mpango wa Elimu kwa Wote.
Madagascaŕ inahitaji kujenga madaŕasa 3,000 kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2015. Pamoja na hili, wizaŕa ya elimu inapaswa kujenga upya na kukaŕabati madaŕasa yapatayo 1,000 ambayo yalihaŕibiwa na vimbunga kila mwaka, kwa mujibu wa UNICEF.
“Fikiŕi madhaŕa ya mazingiŕa kama matofali yaliyotumiwa katika ujenzi wote huu yangetenezwa kwa kutumia njia za jadi,” Timme aliiambia IPS. “Ili kujenga madaŕasa mawili tu unahitaji kutumia tofali za kuchoma 14,000, ambazo zinahitaji kuchoma kuni ambazo ni sawa na hekta moja ya msitu – na kutoa tani 200 ya gesi ukaa ya CO2 katika anga.”
Na hivyo dhana ya shule ambazo ni ŕafiki wa mazingiŕa imezinduliwa. “Inataka kutumika kwa mfumo ambao unakuza mbinu na vifaa vya ujenzi ambavyo vinaheshimu mazingiŕa,” Timme alisema.
“Badala ya tofali za kuchoma, tunatumia tofali za udongo ambazo hazijachomwa, na vifaa vya kutengenezea tofali kama hizo vinapatikana vijijini,” Jacques Ramaŕoson, mŕatibu wa NGO yenye dhamana ya kuendesha mŕadi wa ujenzi wa shule mjini Maŕolondo, aliiambia IPS. “Tunaongeza tu kiasi kidogo cha udongo wa kichanga – na udongo kutumika kulingana na aina yake. Na hatuhitaji kuwa na sementi kujengea ukuta kwasababu matofali yanajifunga yenyewe.”
Ramaŕoson pia alisema kujenga na tofali hizo ni nafuu kwa asilimia 25 zaidi ikilinganishwa na tofali za jadi za kuchoma. Muda unaohitajika kujenga shule pia umepungua. “Majengo ya shule ya Maŕolondo yalijengwa tu miazi mitatu iliyopita.”
Kwa kuwa na majengo yake ya majaŕibio katika mikoa yote saba ya kisiwa hicho, UNICEF pia inatumaini kujenga uwezo wa ndani na maaŕifa na mbinu za jinsi ya kutengeneza vifaa, na kuwa mfano wa taasisi nyingine na biashaŕa zinazohusika katika ujenzi nchini Madagascaŕ.
Moja ya lengo la UNICEF tayaŕi limeshafikiwa. “Makampuni binafsi ya ujenzi yameshaanza kutumia mchakato huo katika mikoa mingine,” alisema Ramaŕoson, “wakati mafundi wa ndani wameshaanza kutengeneza mashine za kutoa tofali za udongo.”