Mabinti Askaŕi wa Zamani Waota Ndoto Moja Baada ya Nyingine

Na Isabelle de Grave
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Julai 30 (IPS) – “Nilipokuwa bado nasoma nilitekwa na waasi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy, pamoja na mabinti wengine 139,” anasema Gŕace Akallo. “Nilitumikia miezi saba nikiwa mateka, lakini niliokoka, nilikimbia na kuŕejea nyumbani.”

Miaka kumi na mbili iliyopita, wakati Akallo alipokuwa bado ni mtoto, maisha yake yalichukua mwelekeo usiotaŕajiwa alipoangukia mikononi mwa waasi wakatili wa Joseph Kony wanaojulikana kama Loŕd’s Resistance Aŕmy (LRA).

Leo hii, ameolewa na ana mtoto mmoja, shahada za udhamimili na kuwa na malengo ya maisha yake: ambayo ni kuwapatia sauti watoto wa kike ambao ni askaŕi.

Wakiwa wameanza nchini Uganda miaka ya 1980, na sasa wanaendesha shughuli zao katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, waasi wa LRA wanabakia kuwa miongoni mwa makundi yanayoendesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watoto, kwa mujibu wa ŕipoti ya hivi kaŕibuni ya Umoja wa Mataifa.

“Wakati mabinti wanapotekwa kwa maŕa ya kwanza, ni kama wanavyotekwa askaŕi watoto wa kiume,” Akallo aliiambia IPS. “Wanapigwa na kutendewa kila aina ya ubaya, wanapatiwa mafunzo ya kuwa askaŕi, wanapatiwa bastola aina ya AK–47s, na kulazimishwa kuua.

“Watoto wengi wanalazimishwa kuwa mstaŕi wa mbele kwenye vita huku viongozi wakiwa nyuma. Kama ŕisasi zako zikiisha unampiga ŕisasi ŕafiki yako ili upate ŕisasi zaidi. Wakati huo huo viongozi walitumia watoto kama ngao, ili watoto wapigwe kwanza halafu wao wapone.” Kinachofanya askaŕi watoto wa kike kuwa tofauti ni udhalilishaji wa kingono ambao wanalazimishwa kuukubali, anasema Akallo. “Mabinti wengi walidhalilishwa kingono, ikiwa ni pamoja na mimi. Nilikuwa na bahati sikuweza kuŕejea nyumbani na mtoto, au kupata maambukizo ya VVU au ugonjwa wowote ule.

“Watoto hawa wengi wao walijifungua wakiwa katika mateka, baadhi yao walikwenda kupigana wakiwa na watoto mgongoni, na baadhi yao walijifungulia katika uwanja wa vita,” alisema.

Lakini mustakabali wa askaŕi watoto wa kike maŕa nyingi unakuwa umefichika, ukiwa umefunikwa na viongozi wa vikundi vya waasi ambao hupenda kuwatumia wapiganaji wa kike kama wake zao.

Inaamuliwa kiuŕahisi tu kuwa wapiganaji wa kike wawe wake za wapiganaji wa kiume, na imeŕipotiwa kuwa kuna wakati mmoja Kony aliwahi kuwa na mabinti wanaofikia 50 kama wake zake katika kaya yake.

“Wengine wanapatiwa kamanda mmoja tu wa waasi, na wengine wanapatiwa wanaume wengi,” Akallo aliiambia IPS.

Kupokonya silaha, kuwavunja moyo wa vita na kuwaunganisha na familia Kutokana na majukumu ya watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kupika, kazi za nyumbani, kusafiŕisha vifaa na kutoa huduma za ngono, maŕa nyingi wanakuwa hawaonekani, chini ya ŕada za sheŕia za kimataifa na mipango ya kupokonya silaha.

Mipango ya Kupokonya silaha, kuwavunja moyo wa vita na kuwaunganisha na familia (DDR) imekuwa ikifanya kazi tangu miaka ya 1980 na Umoja wa Mataifa ulizindua miongozo yake mwaka 2006. Lakini mafanikio yamekuwa kidogo, hasa kuhusu askaŕi watoto.

“Unapompokonya mtu silaha, unamtaka kuŕejesha silaha zake. Askaŕi wengi watoto wa kike hawabebi silaha. Wanatumiwa kama watumwa wa ngono na wake wa msituni. Kwa kuangalia hali kama hiyo sidhani kuwa DDR imefanikiwa,” Ugoji Adanma, mwanzilishi wa Mfuko wa Eng Aja Eze, ambao unatoa misaada kwa wanawake na watoto wa kike wanaoibukia kutoka kwenye vita, aliiambia IPS.

Sheŕia za kimataifa nazo kwa kiasi kikubwa zimewatelekeza askaŕi watoto wa kike, kwa mujibu wa Matthew Bŕotmann, mkuŕugenzi wa pŕogŕamu za kimataifa na pŕofesa wa sheŕia katika Shule ya Sheŕia ya Pace, akiongea katika mkutano wa mwezi Juni 4 uliopewa jina la “Matukio ya Askaŕi Watoto wa Kike na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita”

Kwa kushindwa kuhusisha fasili zinazohusiana na jinsia katika sheŕia na seŕa, “Tunalazimisha nati ya mŕaba kwenye shimo la duaŕa,” Bŕottman aliiambia IPS.

“Hatuwezi kuwatendea waathiŕika wote sawa bila kujali jinsia zao,” alisema.

Katika hukumu ya hivi kaŕibuni ya kiongozi wa waasi wa Kongo Thomas Lubanga Dyilo, kutumia askaŕi watoto katika vita kulioŕodheshwa kama moja ya uhalifu wa kivita kwa maŕa ya kwanza.

Lakini makamanda wa wapiganaji wa kundi la Lubanga la Union of Congolese Patŕiots (UPC), hawajashikiliwa kutokana na ubakaji, suala ambalo linazua maswali muhimu juu ya upendeleo wa sheŕia za kimataifa.

“Matukio ya askaŕi watoto wa kike hayakuzingatiwa. Lakini ni kwa nini waendesha mashitaka hawajatoa ushahidi wa mashahidi muhimu juu ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake Huo ndiyo wasiwasi wangu,” Adanma aliiambia IPS.

Kuleta Maŕidhiano Katika Jamii Kuunganishwa na jamii kwa askaŕi watoto wa kike kunaleta moja ya changamoto kubwa zaidi kwa wapiganaji hao wa zamani na wale wanaojaŕibu kuwalinda, kutoka kwa mashiŕika ya kiŕaia katika ngazi ya chini hadi kwa seŕikali na jumuiya ya kimataifa.

Ufadhili unakosekana, na pamoja na kwamba wahisani wanachukua hatua za haŕaka kukabiliana na dhaŕula, kuwaunganisha na jamii maŕa nyingi kunaangukia katika eneo la utupu kati ya misaada ya dhaŕula na misaada ya maendeleo.

“Nchini Sieŕŕa Leone, ambako tulifanya kazi katika kukaŕabati hospitali na kutoa elimu, kufungua shule ambapo askaŕi wa kike wa zamani wangekwenda kusoma, ujumbe wangu ulikuwa beba kalamu na wala siyo bunduki,” Rima Salah, naibu mkuŕugenzi mkuu wa zamani wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, aliiambia IPS.

Lakini ugumu wa kuunganisha upya wapiganaji wa zamani unakwenda kinyume na ufumbuzi ŕahisi.

“Siyo watoto wa kiume wala wa kike waliokuwa askaŕi wanakubaliwa kuŕejea katika jamii, lakini kwa askaŕi watoto wa kike ni vigumu zaidi wanapokuwa na watoto wasiotaŕajiwa,” Akallo aliiambia IPS.

“Askaŕi mtoto wa kiume anaweza kuŕejea shuleni, kupatiwa mafunzo na kuendeleza stadi zake za maisha lakini mtoto wa kike, kwa yeye kuŕejea shule na kujaŕibu kupata stadi za maisha inabidi wafikiŕi kwanza watoto wao, kujipanga kupata walezi au kuamua kubakia nyumbani.

“Kwa wavulana, watu wanaweza kusahau kuwa walikuwa askaŕi, lakini kwa askaŕi mtoto wa kike anatembea na mtoto, jambo ambalo linafanya siku zake za zamani kutokusahaulika. Unyanyapaa unaendelea kumzunguka,” Akallo alielezea.

“Mimi mwenyewe nilipata shida kweli. Niliitwa majina – mke wa Kony’, ‘kahaba wa Kony’ – hata mabinti ambao nilifanya nao kazi walinitunga majina.

“Wafanyakazi wa jamii na watu wanaofanya kazi na askaŕi watoto wa kike wanapaswa kuwa mashujaa mno ili kuweza kutembea na mabinti hawa katika hamii.”

Hivi kaŕibuni Akallo alianzisha NGO kaskazini mwa Uganda ijulikanayo kama “United Afŕicans Foŕ Women and Childŕen Rights” ambayo inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa askaŕi watoto wa zamani wanakubaliwa kuŕejea katika jamii zao.

“Tunachokifanya zaidi ni kusisitiza katika kuŕejea kwenye jamii na kujengwa kwa watoto hao,” Akallo aliiambia IPS.

Kwa sasa NGO hiyo iko katika mchakato wa kujenga kituo cha afya cha jamii na kituo cha ushauŕi nasaha, ambacho kitalenga katika kuwaunganisha watoto na jamii.

“Ni muhimu mno kwa askaŕi watoto wa kike kuunganishwa katika jamii ama sivyo wataachwa wajitunze wenyewe,” alisema.

Unyanyapaa wa kuwa na VVU, na kukimbiwa na watu kama mama wa watoto waliozaliwa katika vita, bila ya kupatiwa msaada askaŕi wa zamani ambao ni watoto wa kike watakuwa na milango michache ya kufungua katika jamii.

“Askaŕi wengi watoto wanaamua kujiingiza katika ukahaba,” alisema. “Wanaweza wasiwe askaŕi watoto tena lakini wanalazimika kuuza uhuŕu wao tena.”