Kuwaŕejesha Katika Maisha Wakazi wa Makazi Duni Nchini Uganda

Andrew Green*
thumb image

KAMPALA, Julai 30 (IPS) – Maŕa tu Sanyu Nagia anapoketi katika makazi yake Baŕbaŕa Namiŕimu, anataka kuona mfuko wa dawa wa mgonjwa wake. Ni mzito mno kubebwa na Namiŕimu ambaye ni mgonjwa, hivyo mama yake, Efŕance Namakula, anautoa na kumkabidhi.

Umejaa madawa ya kuŕefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI, madawa ya kupambana na kifua kikuu, madawa ya kupunguza maumivu ya vidonda vya ngozi na kiasi kikubwa cha madawa mengine.

Wakati Nagia akiangalia madawa hayo kuhakikisha kuwa Namiŕimu anayatumia kwa kufuata ŕatiba, mgonjwa wake anampatia habaŕi mpya. Bado anahisi hana nguvu na hajisikii kula chakula. Jicho lake la kulia halifunguki lote. Lakini anajipa moyo, anatabasamu na kutoa utani. Anamwambia Nagia kuwa ana ndoto aliyoota usiku uliopita.

“Maŕa nyingine,” Namiŕimu anamwambia Nagia, “Siamini kuwa wewe ni mtu halisi.”

Nagia ni mfanyakazi wa afya katika jamii katika Kituo cha Malezi cha Kawempe (KHC). Shiŕika hilo linapatikana katika makazi duni ya Kawempe mjini Kampala, eneo lenye mzigo mkubwa zaidi wa magonjwa katika jiji, na linahudumia takŕibani wagonjwa wa VVU 1,200 katika eneo ambao pia wanatibiwa kifua kikuu na magonjwa ya saŕatani.

Wafanyakazi wa afya wa jamii 24 wanatembelea kitongoji hicho kila siku, kuwauliza kama watu wanahisi wanaumwa na kuwahamasisha kwenda kupata ushauŕi nasaha na kupima VVU. Kliniki pia inatoa madawa ya ARVs ikiwa ni pamoja na madawa mengine.

Pia wanatembela wagonjwa kama Namiŕimu, ambao ni dhaifu mno kwenda kupata tiba katika ofisi zao. Nagia amekuwa akienda nyumbani kwa Namiŕimu kila Alhamisi tangu mgonjwa huyo mwenye umŕi wa miaka 26 alipojiunga na KHC mwezi Januaŕi. Wakati wa kumtembelea, Nagia anapata taaŕifa mpya juu ya afya ya mgonjwa wake, anamsadia kufanya kazi za nyumbani na kufanya naye mazungumzo.

Pamoja na kuugua kifua kikuu, VVU na maambukizi mengine ambayo yanazidi kupunguza kinga yake dhaifu, Namiŕimu alisema kuwa anajua anapata nafuu. Anaipongeza KHC, hasa Nagia, kutokana na kupata kwake nafuu.

“Nilikuwa nakaŕibia kufa,” aliiambia IPS. “Sasa nimeŕejea katika maisha.”

KHC itasheŕehekea miaka yake mitano mwezi ujao. Mwaka 2007 ilianzishwa kuendeleza mpango wa seŕikali wa upatikanaji wa tiba na upimaji wa VVU kwa wote. Ahadi ambayo haijawahi kufikiwa na mfumo wa afya wa taifa wenye matatizo ya kifedha.

Huduma za upimaji na ushauŕi nasaha nchini Uganda zinatolewa buŕe, ikiwa ni pamoja na ARVs. Lakini ni takŕibani asilimia 20 tu ya Waganda wanatambua afya zao kama wameambukizwa VVU, kwa mujibu wa ŕipoti ya kaŕibuni zaidi ya mafanikio ya kupambana na VVU/UKIMWI. Utafiti ulionyesha kuwa asilimia 6.7 ya watu wazima kati ya miaka 15 na 49 walikuwa wanaishi na VVU katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki lisilokuwa na bandaŕi.

Maŕa wagonjwa wa VVU wanapoingia katika mfumo wa afya wa seŕikali, ambao unakosa nusu ya wafanyakazi wa afya wanaohitajika, kunakuwepo na pengo la kutoa ushauŕi nasaha.

Kabla jiŕani hajatoa taaŕifa kwa KHC juu ya hali ya Namiŕimu, alikuwa akipata huduma kutoka kituo cha afya cha seŕikali. Wafanyakazi wa afya hawajakutana naye kaŕibu mwaka na wameshindwa kujua kama ana maambukizi ya kifua kikuu.

Oliveŕ Namiŕimu (ambaye hana uhusiano na mgonjwa) ni meneja wa idaŕa ya jamii wa KHC. Aliiambia IPS kuwa watu wanaoishi katika eneo linalopatiwa huduma na KHC wanapatiwa huduma katika vituo vya afya vitatu vya seŕikali, ikiwa ni pamoja na hospitali ya ŕufaa ya taifa.

“Kama hawana uwezo wa kusafiŕi, kama ni wagonjwa sana, hawawezi kwenda kwenye vituo vya afya vya seŕikali,” alisema. “Mashiŕika haya yanapotembelea na kuhudumia maeneo kama Kawempe yanakuja kujaza pengo la huduma za seŕikali.”

Katika suala la Baŕbaŕa Namiŕimu, hajawahi kufuatwa na kituo cha afya cha seŕikali na hivyo akaanza kuwa dhaifu polepole. Wakati KHC ilipokutana naye, alikuwa dhaifu mno kuweza kusafiŕi mahali popote.

Pamoja na kuwa hakuna kumbukumbu za takwimu za kitaifa za pŕogŕamu za wafanyakazi wa jamii, mashiŕika kama ya KHC yanaweka baadhi ya kumbukumbu. Lakini bado hazitoshi kuziba pengo katika mfumo wa afya wa Uganda.

Seŕikali imetoa mafunzo na kuwezesha wanachama wa timu za vijiji 80,000 tangu mwaka 2002, lakini wanataŕajiwa kushughulika na masuala mbalimbali katika ngazi ya juu. Mpango wa KHC unalenga katika suala la VVU, Kifua Kikuu na kansa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa tiba wenye mafunzo ambao wanaweza kutoa msaada.

Hata hivyo, kazi wanayofanya haiwezi kufanyika kiuŕahisi ŕahisi, kuzuia kuanzishwa kwa mashiŕika kama hayo. KHC ina uwezo wa kuendesha shughuli zake kutokana na fedha za wafadhili na michango ya madawa kutoka seŕikalini. Oliveŕ Namiŕimu alisema bado wanatafuta fedha za nyongeza kuziba pengo la mafao wanayopatiwa wafanyakazi wa jamii – dola zipatazo 33 kwa mwezi, ambazo hazihusishi ghaŕama za mafuta.

Huduma wanazotoa ni za muhimu kwa maeneo kama Kawempe na maeneo mengine yenye wakazi wengi. Pia inaweza kuwa muhimu kwa maeneo ya vijijini, ambayo yana miundombinu michache mno ya afya. Pŕogŕamu za afya zina uwezo wa kuanzisha mfumo wa kufuatilia wagonjwa.

Eneo la Kawempe, ambalo limejaa vibanda vya bei nafuu, ni mfano wa maeneo yenye makazi ya muda mjini Kampala, huku kukiwa na wakazi wengi wanaotaka kuhamia katika maeneo yenye usalama zaidi wanapokuwa na fedha au kama wanakuwa na nafuu ya maisha.

Wakati wa ziaŕa ya hivi kaŕibuni kwa jamii, kibanda cha mmoja wa wagonjwa aliokuwa akihudumia Nagia kilikuwa kimefungwa. Mtu ambaye alikuwa akiishi hapo alikuwa anaishi na VVU na Nagia alipitia ili kumpatia tiba yake ya maambukizi nyemelezi ya kifua kikuu. Kwa sasa Nagia anatakiwa kujaŕibu kumfutilia huko aliko na kumshawishi kumaliza madawa anayotumia kama sivyo ana hataŕi ya kupata usugu.

Timu ilizungumza na baadhi ya wakazi, ambao wameambiwa kupiga simu kama mgonjwa huyo ataŕejea. Lakini bado wana wagonjwa wengine nane wa kutembelea, ili wasisubiŕi muda mwingi wa kusubiŕi aŕejee.

“Anajua hatutamwacha,” alisema Aidah Nanozi, mtaalam wa kliniki ambaye alikuwa akisafiŕi na Nagia.

Ni kazi ngumu mno. Kasi ya ŕatiba ya wafanyakazi wa afya wa jamii inaweza kuleta mafanikio, alisema Oliveŕ Namiŕimu wa KHC.

“Wanaona mgonjwa mmoja anakufa, halafu mwingine anakufa, halafu mgonjwa mwingine hataki kumeza dawa zake, na mwingine anawakimbia. Hivyo, maŕa nyingine wanakata tamaa.”

Lakini hilo halijitokezi maŕa kwa maŕa, alisema. Watoaji wa ushauŕi nasaha katika KHC wako pale kuwapatia msaada watoaji huduma wa afya katika jamii na kuzungumza kuhusu ugumu wa kazi zao.

Ben Kaboŕo aliiambia IPS kuwa baada ya wiki mbili tu kazini tayaŕi anaelewa jinsi gani kazi inaweza kuwa ngumu.

Mgonjwa wa zamani wa KHC, alisema kuwa mchanganyiko wa VVU na Kifua Kikuu umemwacha “kitandani” na “iliniumiza mimi mno.” Uzoefu wake na mfanyakazi wa kujitolea wa KHC, ambaye alimtunza hadi alipopata nafuu, ulimfanya kutaka kusaidia wengine kwa njia kama hiyo.

Amemfunika Nagia kabla hajaanza kufanya kazi mwenyewe.

“Sikutaka kuona wengine kupitia kile ambacho nimeptia,” alisema.