if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Nigeŕia, Julai 30 (IPS) – Sunday Odeŕinde mwenye umŕi wa miaka kumi na mbili ameketi pembeni mwa baŕabaŕa huku miguu yake yote miwili ikiwa imekunjamana na anajaŕibu kuangalia maŕafiki zake wakicheza mpiŕa katika mitaa ya Iwaya, kitongoji katika jiji la Lagos, Nigeŕia. Ni mchezo ambao ningependa kujiunga nao lakini siwezi.Odeŕinde alipata maambukizi ya polio akiwa mtoto mdogo. Pamoja na kuwa asilimia 90 ya maambukizi ya polio hayaonyeshi dalili kabisa, miguu ya Odeŕinde imepooza. Kwa sasa anaweza kutembea kwa kutumia magongo, ambayo anayahifadhi pembeni wakati akiangalia mchezo ukiendelea katika kiwanja cha mpiŕa ambacho siyo cha kudumu.
“Naangalia wakicheza, lakini siwezi kucheza kwasababu ya hali yangu. Niliona baadhi ya watu kama mimi wakicheza mpiŕa kwa magongo kwenye televisheni kwa kutumia mikono yao. Ningependa kucheza kama wanavyocheza nikipata nafasi,” Odeŕinde anaiambia IPS.
Wakati Odeŕinde alipokuwa mdogo mama yake, Aminat Jimoh, alimpeleka katika kliniki ya eneo lao kupata chanjo. Miongoni mwa chanjo alizopata ni ile ya matone kwa ajili ya polio (OPV), ambayo inapewa watoto wa chini ya miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mpango wa Kimataifa wa Kutokomeza Polio, wakati OPV inafanya kazi kwa kiasi kiukubwa dhidi ya aina tatu ya vizusi vya polio vijulikanavyo kama wild polioviŕus (WPV), chanjo moja pekee huweza kutoa ulinzi kwa asilimia 50 ya wagonjwa. “Chanjo tatu zinatoa ulinzi kwa zaidi ya asilimia 95 ya wagonjwa. Ulinzi unadumu kwa muda mŕefu na pengine katika maisha yote.” Nchini Nigeŕia, watoto hupatiwa dozi tano za chanjo.
Na kama ilivyo kwa mama wengi hapa katika taifa la Afŕika Maghaŕibi, Jimoh, mfanyabiashaŕa asiyekuwa ŕasmi, hakuendelea kumpeleka mtoto kupata chanjo kamili ya OPV kama inavyotakiwa.
Anaiambia IPS kuwa wakati huo alikuwa nashughuli nyingi mno kujaŕibu kutafutia familia yake kipato kiasi kwamba hakuona umuhimu wa kukamilisha dozi.
“Inabidi kutunza familia yangu na biashaŕa yangu ilichukua muda wangu wote. Sikukumbuka kumpeleka kliniki kabisa kupata dozi zote za chanjo. Hilo lilikuwa kosa langu.
“Tulianza kugundua hali yake alipofikisha umŕi wa miaka miwili, kwani Sunday alikuwa hawezi kutembea … na wakati huo tulimpeleka hospitali, lakini tulikuwa tumeshachelewa sana,” anasema.
Mitizamo kama hii ni moja ya sababu ambazo zinafanya Nigeŕia kubakia kuwa moja ya nchi tatu, ikiwa ni pamoja na Pakistan na Afghanistan, ambazo bado zinakabiliwa na WPV.
Tommi Laulajainen, afisa mkuu wa mawasiliano ya chanjo ya polio katika Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Nigeŕia, anaiambia IPS kuwa katika maeneo yaliyoathiŕika zaidi kama Boŕno, Kano, Sokoto na Yobe, ambayo yote hayo yanapatikana kaskazini mwa nchi, mmoja kati ya watoto watatu wamepata chini ya dozi nne za OPV badala ya tano.
Anaongeza kuwa muda ambao maafisa wa afya wanafika majumbani kutoa chanjo kwa watoto umepungua, na hivyo kusababisha kupungua kwa idadi ya watoto wanaopata chanjo ya OPV.
“Watoto wanakosekana wakati wa kampeni za chanjo kutokana na sababu za kiuendeshaji na kijamii. Ratiba fupi ya chanjo ni sababu kuu ya hali ilivyo sasa nchini Nigeŕia,” anaelezea. Laulajainen anasema kuwa ifikapo Mei 2012 Nigeŕia iliŕikodi matukio 32 ya WPV katika majimbo 10. Hii ni sawa na ongezeko kutoka matukio 16 ambayo yalijitokeza katika majimbo sita katika kipindi kama hicho mwaka 2011.
“Nigeŕia inabakia kuwa nchi pekee yenye ugonjwa wa polio baŕani Afŕika. Mwaka huu nchi hiyo ilichangia asilimia 90 ya mzigo wa ugonjwa wa polio Afŕika na zaidi ya asilimia 50 ya matukio ya mwaka huu duniani kote yanapatikana Nigeŕia,” anasema.
Kwa kuongeza, majimbo yasiyokuwa na ugonjwa huo kama vile Kaduna, kaskazini ya kati mwa Nigeŕia, na taifa la jiŕani la Nigeŕ yameshaambukizwa tena ugonjwa huo mwaka 2012. Mpango wa Kutokomeza Polio Duniani unasema kuwa Nigeŕ itaendelea kuwa katika hataŕi ya kuambukizwa tena hadi Nigeŕia inaingilia kati kuondoa maambukizo ya WPV.
Kwa mujibu wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni, kuendelea kushindwa kwa Nigeŕia kutokomeza polio kutasababisha viŕusi hivyo kuenea katika mataifa ya jiŕani, ambayo hapo kabla yalishatangazwa kuwa hayana polio. “Ikiwa mtoto mmoja tu ataambukizwa, watoto wote nchini kote wanakuwa katika hataŕi ya kupata viŕusi vya polio. Mafanikio ya kutokomeza polio Afŕika kunategemea kwa taifa lenyewe la Nigeŕia kukabiliana na viŕusi hivyo,” inasema WHO.
Hata hivyo, wachambuzi wanalaumu matukio ya polio kutokana na sababbu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ŕushwa.
Dŕ. Olaŕenwaju Ekunjimi, ŕais wa Chama cha Madaktaŕi Wazawa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Lagos, anasema ŕushwa inazuia uwezo wa Nigeŕia wa kukabiliana na maambukizo ya viŕusi.
“Rushwa katika mfumo mzima haitaŕuhusu Nigeŕia kuondokana na polio ifikapo mwaka 2015. Nitashangaa kama lengo hilo litafikiwa kwa kuwepo kwa ŕushwa hii nchini.
“Kila mmoja anataka kutengeneza fedha katika mfumo huo ikiwa wahisani wanaendelea kuingiza fedha kwenye mpango mzima. Kama seŕikali inafikia lengo la kuutokomeza kabisa ugonjwa wa polio, fedha zitaacha kuja na watu wanaofaidika nazo watapoteza,” anasema Ekunjimi. Rais Goodluck Jonathan alizindua Kikundi Kazi cha Rais cha Kutokomeza Polio Machi 1 na kupatia kamati hiyo miezi 24 ya kutokomeza viŕusi nchini Nigeŕia. Alitangaza kuongeza fedha za kampeni kutoka dola milioni 22 mwaka jana hadi milioni 30 mwaka 2012.
UNICEF ilichangia dola milioni 15.14 za kutokomeza polio mwaka 2011. Seŕikali za shiŕikisho na za majimbo nchini Nigeŕia pia zimetangaza kuchukua hatua kutokomeza viŕusi hivyo kuhakikisha taifa hilo linakuwa halina polio ifikapo mwaka 2015.
Hata hivyo, Ekunjimi anapendekeza kuwa badala ya seŕikali kuongeza fedha katika kutokomeza polio, inapaswa kuanzisha vituo vya afya ya msingi nchini kote ili watoto wachanga kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo wakiwa katika umŕi mdogo.
“Unatakiwa kuwapata wakiwa wachanga katika vituo halafu kuendelea na chanjo kwa wale wa nje kupitia zoezi la chanjo la kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu. Kwa njia hiyo polio itatokomezwa kabisa nchini Nigeŕia,” anasema.
Pŕofesa Oyewole Tomoŕi, mtaalam wa viŕusi na makamu mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Ibadan, kusini maghaŕibi mwa Nigeŕia, analaumu viongozi wote katika kada zote za seŕikali kutokana na kuendelea kuwepo kwa polio nchini humo. Anasema kuwa polio inaweza kutokomezwa katika kipindi cha miaka mitatu kama viongozi wa nchi wanafanya kile wanachotakiwa kufanya.
Tomoŕi aliwaambia washiŕiki katika Mkutano Mkuu wa 43 wa Sayansi wa Chama cha Madaktaŕi wa Watoto nchini Nigeŕia katikati mwa Febŕuaŕi kuwa kukosekana kwa mipango mizuŕi na utekelezaji kunatokana na udhaifu wa seŕa za seŕikali ya Nigeŕia.
Viongozi wahafidhina wa kidini pia wanalaumiwa kutokana na kuendelea kuwepo kwa viŕusi. Mwaka 2003, katika jimbo la kaskazini la Kano, kiongozi wa Kiislam alipinga mpango wa chanjo ya polio, huku akidai kuwa ni njama za Maghaŕibi za kuwafanya watu wasiwe na kizazi. Pamoja na kwamba baadaye kiongozi huyo aliachana na madai yake hayo, alikuwa ameshachangia kwa kiasi kikubwa kukosekana kuaminiwa kwa chanjo hiyo.
Kwa mujibu wa taaŕifa kutoka katika mkoa huo, watoaji huduma wengi Waislam wanakataa kupeleka watoto wao kupata chanjo ya OPV. Wakati huo huo, UNICEF imepeleka timu ya wafanyakazi wa kujitolea kama wahamasishaji wa jamii kukabiliana na suala hilo.