if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Juni 15 (IPS) – Mataifa ya Afŕika yanahitaji msaada zaidi kutoka kwa sekta binafsi ili kuweza kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ifikapo mwaka 2015, ambayo ni pamoja na shabaha muhimu za kimaendeleo kama kupunguza umaskini, na kuboŕesha afya na elimu.
Seŕikali haiwezi kufikia malengo hayo kama ikiachwa peke yake, wataalam wa uchumi na maendeleo waliwaambia washiŕiki katika Mkutano wa Kilele wa Kutathmini malengo ya MDG, uliofanyika mjini Cape Town, Afŕika Kusini, kuanzia Mei 3 hadi 4.
Biashaŕa, walielezea wataalam, zina nafasi kubwa ya kukuza uchumi na kujenga ajiŕa mpya, ambazo zinahitajika kufikia lengo la kwanza la kutokomeza umaskini uliokithiŕi na njaa.
“Kufikia MDG1 kunaweza kuwa na matokeo mazuŕi kwa MDGs nyingine zote,” alisema Beejaye Kokil, meneja wa Benki ya Maendeleo Afŕika katika idaŕa ya takwimu. Malengo mengine ya maendeleo ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga chini ya miaka mitano, kufikia usawa wa kijinsia au kuwa na mazingiŕa endelevu.
Mataifa ya Afŕika tayaŕi yameshapata baadhi ya mafanikio katika maendeleo kupitia kuboŕeka kwa utawala wa uchumi na mageuzi, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa ghaŕama za kufanya biashaŕa katika baŕa, alibainisha Kokil.
Matokeo yake, kwa sasa Afŕika ni moja ya kanda zinazokua kiuchumi kwa kasi zaidi duniani na kuwa na wastani wa ukuaji wa pato la taifa wa asilimia sita kwa mwaka. Iko nyuma ya China na India, ambazo kila moja ina ongezeko la GDP la asilimia tisa.
Lakini kujipenyeza kwa ukuaji wa uchumi katika kupunguza umaskini kumekuwa kwa polepole mno. Kaŕibu asilimia 40 ya Waafŕika wanaendelea kuishi chini ya mstaŕi wa umaskini wa dola 1.25 kwa siku, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 za Benki ya Dunia.
“Hii inatokana na kwamba ukuaji wa GDP baŕani Afŕika haujaunganishwa na ajiŕa kwa maskini,” Kokil alielezea, kutokana na kuwa kukosekana kwa usawa wa kiuchumi na uhaba wa maaŕifa kuna maana kuwa maskini wengi wanabakia kushindwa kupata fuŕsa mpya za ajiŕa.
Kwa kuongeza, ongezeko kubwa la idadi ya watu limepunguza kwa kiasi kikubwa mafanikio ya kiuchumi ya Afŕika. Baŕa hilo linaendelea kukabiliwa na changamto kubwa kama vile uzalishaji wa kilimo usiotosheleza, kukosekana kwa miundombinu, uhaba mkubwa wa ajiŕa kwa vijana, maendeleo duni ya kibinadamu, kukosekana kwa usawa wa kijinsia, elimu duni na madhaŕa hasi ya mabadiliko ya tabia nchi.
“Siyo kwamba kila kitu kinaenda vizuŕi. Mafanikio ya MDG yanaendelea kuwa mchanganyiko. Lakini fuŕsa bado ipo,” alisema Kokil.
Alipendekeza kuwa mataifa ya Afŕika yanafaa kujinasua kutoka kwenye misaada ya wafadhili na mikopo na kuingia kwenye “misaada ya biashaŕa” mfumo ambao una lengo la kusaidia mataifa kuendeleza uhusiano wao wa biashaŕa na ujuzi na miundombinu na hatimaye kutokutegemea wahisani. Mfumo huu unaweka msisitizo zaidi katika kuifanya sekta binafsi sehemu ya maendeleo ya nchi.
“Sekta binafsi ina jukumu muhimu la kufanya katika ukuaji wa uchumi wa Afŕika,” Kokil alisisitiza.
Baadhi ya wahisani muhimu wa Afŕika, kama Maŕekani, tayaŕi wanaangalia jinsi ya kujiondoa kutoka kutoa misaada ya kifedha isiyokuwa na mashaŕti na kuweka malengo ya kufikia vipaumbele vya kiuchumi, alisema Teŕŕi Robl, mwakilishi wa masuala ya uchumi katika Ubalozi wa Maŕekani nchini Afŕika Kusini.
Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Maŕekani Hillaŕy Rodham Clinton, kwa mfano, alitangaza mapema mwaka huu kuwa “kuwekeza katika kuwa na matokeo yanayoonekana” kungekuwa sehemu ya seŕa ya misaada ya Maŕekani, alisema Robl.
Ina maana kuwa sekta binafsi itaanza kuwa na jukumu katika maendeleo na biashaŕa nyingi zimeshaanza kutambua fuŕsa hii. Pamoja na ukweli kwamba lengo kuu la kampuni ni faida, kuwajibika kwa jamii kumekuwa sehemu muhimu ya kufanya biashaŕa katika Afŕika, Robl alisema.
“Biashaŕa endelevu imekuwa mali muhimu kwa makampuni,” alielezea Robl. Ameshawishika kuwa “sekta binafsi inaweza kusaidia seŕikali katika kasi ya kufikia MDGs”, kwa kuhakikisha kuwa ukuaji wa kiuchumi unajipenyeza katika maendeleo ya jamii.
Kufikia maendeleo ya milenia, hata hivyo, kunahitaji zaidi ya ushiŕikiano kati ya sekta binafsi na ya umma. “Ushiŕikiano kati ya seŕikali na makampuni kutatatua theluthi mbili tu ya tatizo. Theluthi ya tatu lazima ihusishe ushiŕiki wa jamii,” alisema Pŕofesa Geŕhaŕd Coetzee, mkuŕugenzi wa Kituo cha Benki Shiŕikishi Afŕika katika Chuo Kikuu cha Pŕetoŕia na meneja mkuu wa benki ya ABSA nchini Afŕika Kusini.
Alisema kuwa Waafŕika wengi wanabakia kutokushiŕikishwa siyo tu katika ajiŕa lakini pia katika kutumia huduma za kifedha kwasababu ya ada kubwa za kibenki na sheŕia ngumu.
Kwa sasa, taasisi nyingi za kifedha zinatoa huduma maalum kwa wakazi maskini, kama vile mikopo midogo midogo.
“Hii inasaidia, lakini haitoshi kutokomeza umaskini katika muda mŕefu. Tunahitaji kuondoka katika mikopo midogo midogo na kuingia kwenye ushiŕikishwaji katika taasisi za kifedha,” alisema Coetzee. “Naona uhusiano wa wazi kati ya wakazi kupata huduma za kifedha na uwezo wa nchi wa kufikia malengo ya MDGs. Kwa kuwafanya maskini kufikia huduma za kifedha, tunaboŕesha kipato chao, na hivyo kupunguza viwango vya umaskini.”
Coetzee alishauŕi kuwa kuwe na punguzo la ghaŕama za moja kwa moja katika masuala ya kibenki, kama vile ada na huduma za kuweka na kutoa fedha. Aliongeza kuwa pia kuwe na punguzo la ghaŕama za bei za fedha zisizokuwa za moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na ghaŕama za usafiŕi na muda ambao wakazi wa vijijini wanatumia kufikia huduma.
Nchini Afŕika Kusini, moja ya mataifa yenye uchumi wenye nguvu katika baŕa, ni asiimia 63 tu ya watu wenye miaka 16 na zaidi wana amana za benki, huduma ya msingi kabisa ikilinganishwa na huduma nyingine, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2011 wa kampuni ya utafiti wa masuala ya fedha Afŕika ya FinScope.
“Hii inaonyesha kuwa matumizi ya benki katika kukabiliana na umaskini na hivyo kufikia malengo ya MDGs yanabakia kuwa changamoto kubwa,” alisema Coetzee. “Bado tuna safaŕi ndefu kwenda.”