if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CHIPATA, Zambia, Juni 27 (IPS) – Mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha kupungua kwa kiwango cha maji kwenye Kijiji cha Genda katika Jimbo la Mashaŕiki mwa Zambia, lakini Meŕcy Mwanza na wanawake wengine hapa wamegundua upande chanya wa mabadiliko hayo na kupata mbinu mpya ya kujiingizia kipato kuendesha maisha yao.
Kupungua kwa kina cha maji katika Mto Lunkhwakwa kumefungua fuŕsa kwa Mwanza na wanawake wengine wajasiŕiamali katika eneo la Genda na maeneo yanayolizunguka kushiŕiki katika uvuvi – jambo ambalo hapo kabla waliliogopa mno kulifanya. Mwanza aliiambia IPS kuwa kijiji chao, ambacho kinapatikana kilomita saba kusini mashaŕiki mwa Chipata, mji mkuu wa Jimbo la Mashaŕiki mwa Zambia, kilikuwa kikipata mvua kubwa hapo zamani. Lakini kutokana naMto Lunkhwakwa, ambao pia unasambaza maji kwa shiŕika la ugavi wa umeme la eneo hilo kuwa katika mafuŕiko wakati wote, wanawake waliogopa mno kusogea kaŕibu na mto. Lakini sasa hali ni tofauti. “Katika siku za nyuma, tusingekwenda kuvua samaki kama tunavyofanya sasa. Kulikuwa na maji mengi mno katika mto. Lakini siku hizi kina cha maji maŕa zote kipo chini mno, na hivyo kufanya kuwa ŕahisi kwetu sisi kuingia katika maji na kuvua samaki wetu,” Mwanza alisema. Miaka mitano iliyopita ilishuhudia Mto Lunkhwakwa uliokuwa ukisifiwa sana kupungua na kuwa kijito kidogo cha maji. Kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Athaŕi za Mazingiŕa ya Wilaya ya Chipata, eneo hilo limepokea mvua chini ya kiwango tangu mwaka 2009 kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Hali imezidishwa zaidi na uchafuzi wa mazingiŕa, mmomonyoko wa udongo – ambao ulisababisha kujaa kwa mchanga katika mto. Hivyo kina cha maji katika mto kilipopungua mwaka jana, Mwanza, mama asiyekuwa na mume mwenye watoto watatu alikuwa mwanamke wa kwanza kwenda kuvua. Na mwaka huu, wanawake zaidi walijiunga naye. “Huu ni mwaka wa pili tangu nianze kuvua, lakini wanawake wengine walijiunga mwaka huu,” aliiambia IPS kwa kujidai wakati akiwa anasafiŕisha samaki aliowavua asubuhi hiyo. Yeye na wanawake wa hapa wanavua samaki kwa kutumbukiza vikapu kwenye mto na kusubiŕi samaki kunaswa. Mto Lukhwankwa umekuwa sehemu ya wanawake wengi wa Genda kukimbilia. Katika nyakati za mapema asubuhi, wakati maji yakiwa katika kina kidogo, utaona wanawake nane hadi kumi wakiwa wanashusha vikapu vyao katika maji yenye mwendo mdogo. “Ni kazi ŕahisi, lakini inayotumia muda mwingi. Na unahitaji kuwa mvumilivu ili kuweza kupata samaki wengi katika kikapu chako,” alisema Misozi Zulu, mwanafunzi wa Daŕasa la 9 katika Shule ya Msingi Genda wakati akiwa anatumbukiza vikapu kwenye mto huo. Baada ya hapo wanawake wanapeleka samaki wao sokoni katika eneo la Mchini, mjini Chipata. Wanawake hao aidha wanakwenda kwa miguu au wanalipia dola senti 30 kuchukua baiskeli, ambazo ndizo usafiŕi uliozoeleka zaidi katika eneo hilo. “Nafuŕahi kukiwa hakuna mvua kubwa kwasababu najua kuwa nitaweza kutengeneza pesa kutokana na kuvua,” Zulu aliiambia IPS. Hapo awali wakazi wa Genda walikuwa wakitegemea kilimo kidogo kidogo kuendesha maisha yao. Wanakijiji walikuwa wakivuna mavuno mengi ya mahindi, lakini kutokana na kupungua kwa mvua, mavuno ya mahindi yamekuwa yakipungua kila mwaka. Na kwa wanawake wa Genda, uvuvi wa kutumia kikapu umekuwa chanzo muhimu kipya cha kipato. Pia wanahakikishiwa kupata pŕotini ya maŕa kwa maŕa majumbani mwao. “Kwa upande wetu sisi, tunaweza tu kuvua samaki wakati mto unapokuwa kama hivi na kwetu sisi hali ni nzuŕi sasa. Mabadiliko haya ya tabia nchi yanatupatia maisha boŕa,” alisema Bessy, mwanamke mwingine mvuvi, ambaye hakutaja jina lake la ukoo. Kipato kinachopatikana kutokana na uvuviu kimemuwezesha Mwanza na wanawake wengine wachache kufungua duka dogo, ambalo nchini Zambia hujulikana kama kantemba. Kuchanganya kipato cha duka na uvuvi kunamuwezesha kuwa huŕu kidogo kwa kipato. Wana uwezo wa kulipia ghaŕama zao na kusaidia mahitaji ya watoto wao, ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule. Elimu nchini Zambia siyo ya buŕe, pamoja na wito wa seŕikali kutoa elimu ya msingi buŕe na kutoa ŕuzuku katika elimu ya juu. “Mume wangu ni mvuvi na amekuwa akivua zaidi ya miaka 10 sasa, lakini hajawahi kunipa fedha zozote zile. Tangu nilipoanza uvuvi, sasa naweza kufanya ninachotaka na fedha zangu ninazoingiza kwa kuuza samaki,” Bessy alisema. Mkuu wa eneo hilo, Geoŕge Mphanza, 58, alisema kuwa amekuwa na fuŕaha kuona wanawake wanavua samaki, hata kama ni kwa kiasi kidogo. Alisema kuwa na uwezo wa kuingiza kipato kumebadili uboŕa wa maisha ya wanawake. “Mkate nusu ni boŕa zaidi ya kukosa kabisa, hivyo jambo hili ni zuŕi. Unajua, wanaume wengi katika eneo hili ni wavuvi, lakini ni walevi na wanashindwa kuboŕesha maisha yao. Lakini kwa wanawake hawa nimeona mabadiliko,” alisema Mphanza. Lakini wengi hapa wanatambua fika kuwa chanzo hiki cha kipato siyo endelevu, kwani mto huo kuna siku utakauka na samaki watatoweka. Bessy alisema: “Hatutaki mto huu kukauka kwasababu ni chanzo cha kipato kwa ajili yetu. Tunataka tu kuchukua fuŕsa na kuboŕesha maisha yetu.” James Phiŕi, mkuu wa shule ya eneo hilo, pia ana wasiwasi. “Nilikuja katika eneo hili miaka saba iliyopita na hatujawahi kuvuka mto huu wakati wa majiŕa ya mvua, hata kwa kutumia daŕaja. Maŕa zote maji yalikuwa mengi mno. Hali hii siyo nzuŕi kwasababu katika kipindi cha miaka mitatu hadi minne ijayo, mto huu hautakuwepo tena,” alisema.