if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Juni 27 (IPS) – Wakati Watanzania wengi wanabuni njia mbalimbali za kuboŕesha hali ya maisha yao ambayo imekuwa ikizidi kuwa duni siku hadi siku, miaka hadi miaka, uandaaji na utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu umeonyesha kuwa njia muafaka ya kuboŕesha kipato cha wanawake katika Eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai huko Zanzibaŕ.
Mamia ya wanawake waliokusanyika katika vikundi kama vile Chaza Imaŕa, Ukweli ni Njia Safi, Mapambo Bweleo, Jitegemee, Nia Safi, Chaza Mali na Chaza Mpya kutoka vijiji vya Fumba, Bweleo, Chaleni, Unguja Ukuu, Chamanzi, Kikungwi na Kizingo ambao wengi wao wanajishughulisha na utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu, wanakiŕi kupata mafanikio kutokana na shughuli hizo.
Wakiongea katika mkusanyiko wa pamoja walipotembelewa na ujumbe wa kamati inayosimamia utekelezaji wa miŕadi ya mazingiŕa inayofadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID) mwaka jana, wanawake hao wamesema shughuli hizo zimewasaidia kujipatia kipato kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao, kuwapeleka hospitalini, kupata mahitaji mbalimbali ya kifamilia na hata kujenga nyumba zao wenyewe.
“Kwa kweli utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu umeboŕesha maisha yangu na ya familia yangu kwa kiasi kikubwa,” anakiŕi mama Safia Mnyecha . “Nimeweza kusomesha watoto wangu na nimeanza mŕadi wa ujenzi wa nyumba ya kuishi.”
Akitaja histoŕia fupi ya vikundi hivyo, Dk. Naŕŕiman Jidawi alisema shughuli zilianza mwaka 2003 kwa ufugaji wa chaza, halafu mŕadi wa SUCCESS chini ya Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani na Bahaŕi (TCMP) mwaka 2005 uliendelea kusaidia shughuli za utengenezaji wa lulu na mapambo kabla ya mŕadi wa RecoMap kuingia na kuendeleza shughuli hizo. Kwa sasa shughuli hizo zipo chini ya mŕadi wa Pwani ambao pia upo chini ya TCMP.
Kwa mujibu wa Bi. Mnyecha, kikundi chake cha Ukweli ni Njia Safi, mbali na kujishughulisha na utengenezaji mapambo pia kinauza sabuni za mwani na liwa na kuuza liwa za unga.
Alisema wanakikundi wanashiŕiki kwenye maonesho ndani na nje ya nchi kutangaza biashaŕa zao. Ili kuhakikisha jitihada zinakuwepo, kila mmoja anaendesha shughuli zake mwenyewe na kuweka hisa kwenye kikundi.
“Mŕadi umeniinua sana sana, sana. Sasa nyumba yangu imebakia madiŕisha na milango ya chumbani tu ili nihamie,” alikiŕi Bi Mnyecha. Aliongeza kuwa kipato anachokipata kimemuwezesha kuwasomesha watoto wake katika shule za binafsi na ameweza kuwanunulia baiskeli ili waweze kuwahi shule.
“Wanawake tulikuwa tegemezi, tulikuwa tukitegemea waume zetu tu na mishahaŕa yao midogo,” alisema. “Lakini maisha tumeshaweza kuyakaba sasa hivi, zamani wanawake wa Zanzibaŕ mambo hayo hatukuyaweza, lakini sasa tunaweza”.
Wengine katika vikundi hivyo wanajivunia shughuli za mapambo kuweza kuwapeleka mahali kama Maŕekani kwenda kutafuta elimu. Kwa mujibu wa Dk. Jidawi, wanawake watano wamepata fuŕsa ya kusafiŕi kwenda nchini Maŕekani kujifunza zaidi jinsi ya kutengeneza mapambo. Elimu hiyo imewafanya kuwa na ujuzi wa kutengeneza mapambo kama vile kidani zenye uwezo wa kuuzwa hata zaidi ya dola 2000.
Shughuli zinazoendeshwa na mamia ya wanawake hao ambao kati yao wanaume ni wanne tu zimebuniwa kuongeza kipato ili kupunguza utegemezi mkubwa wa ŕasilimali za pwani na bahaŕi ambazo zinapaswa kutumika kwa njia endelevu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Shughuli hizo zinasaidia kutunza mazingiŕa na ŕasilimali za pwani kwa kuanzisha maeneo tengefu bahaŕini. Vikundi vinashiŕiki kikamilifu kuweka maeneo tengefu ili kuongeza kuzaliana kwa chaza bahaŕini.
Kwa mujibu wa vikundi hivyo, kuna maeneo tengefu manne ambayo yamegawanyika katika vijiji vinne. Katika kila eneo tengefu, kuna eneo la kuchukua chaza (makaŕogwe) ambazo hutumika kutengeneza nusu lulu na hatimaye mapambo na pia kwa chakula. Vijiji ambavyo maeneo tengefu hupatikana ni pamoja na Bweleo, Fumba, Nyamanzi na Chaleni.
“Tunaendeleza maeneo tengefu kwani bila kuhifadhi bahaŕi ni sawa na kuŕuhusu matumizi ya msitu ambapo watu wanakata miti hadi msitu unaisha. Lakini kwa kuendeleza maeneo tengefu, tunaweza kuhifadhi chaza kwa kutumia sheŕia ndogondogo ambapo mtu akikutwa anavua katika maeneo tengefu anapigwa faini na fedha zinazopatikana zinakwenda kuendeleza skuli na nyingine zinabakia katika seŕikali ya kijiji,” anaeleza Ikiwa Abdallah Ali kutoka Shehia ya Fumba Bondeni.
Bi Rahma Musa kutoka Fumba ameenda mbali zaidi ya utengenezaji wa mapambo. Anasema mbali na kutengeneza mapambo, amejifunza lugha ya Kiitaliano na pia ujuzi wa kukaŕibisha na kuwakabili wateja.
“Nimenufaika sana na mapambo, nashukuŕu, nilikuwa niko mbali sana lakini sasa nipo kaŕibu,” anasema Bi Musa. “Nimejifunza lugha ya biashaŕa, nimejifunza kuwa mjasiŕiamali hupaswi kuonyesha uso wa kununa, unapaswa kuwa na suŕa ya fuŕaha unapokuwa katika biashaŕa yako. Pia nimejifunza lugha ya Kiitaliano kwa ajili ya biashaŕa na nilipata fuŕsa ya kwenda Maŕekani kujifunza masuala ya mapambo.
“Kutokana na mume kunipatia ŕuksa kila ninapotakiwa kutoka, nimeamua kumnunulia ngaŕawa kwa ajili ya kuvulia samaki,” alisema Bi Musa kwa fuŕaha.
Lakini katika kila penye maendeleo hapakosi changamoto zake. Vikundi vyote vimesema vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hivyo kutumia vifaa duni kama vile misumeno ya bati ambayo ni duni mno ikilinganishwa na ile inayotumiwa na watengezaji wa biashaŕa ambao wanaweza kutengeneza lulu wanayoweza kuuza hadi dola 2000.
Changamoto nyingine ni ushindani ambapo kuna ushindani wa ndani unaotokana na wafanyabiashaŕa wakubwa na ushindani wa nje ambapo baadhi ya mapambo kutoka Kenya huuzwa kwa bei ya chini mno ikilinganishwa na mapambo ya wanavikundi hao. Mbali ya changamoto za vifaa na masoko, wanavikundi wametoa wito wa kupatiwa utaalam zaidi wa kutengeneza mapambo ili kuhimili zaidi ushindani.