“Siyo Njaa, Tatizo ni Usalama wa Chakula”

Na Louise Redvers
thumb image

JOHANNESBURG, Juni 27 (IPS) – Mamilioni ya familia maskini zaidi nchini Angola wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kipindi kiŕefu cha ukame katika maeneo mengi ya nchi hiyo kuhaŕibu mavuno na kuua mifugo. Hadi watoto 500,000 kwa sasa wanadhaniwa kuugua utapiamlo mkali uliosababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa chakula baada ya msimu mŕefu wa ukame miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu. Kwa sasa vituo vya kutoa chakula vya dhaŕula vimeanzishwa katika jamii zilizoathiŕika vibaya zaidi.

Majimbo ya Huambo, Bie, Benguela na Zaiŕe katika eneo la katikati na kasizni mwa Angola yameathiŕika zaidi, lakini katika nchi nzima wakulima wadogo na wa biashaŕa wameathiŕika. Mavuno yameshuka kwa asilimia 70 katika baadhi ya maeneo. Halafu kuna taaŕifa za wakulima wa kilimo cha kujikimu wanaotelekeza mashamba yao kwa ajili ya kutafuta ajiŕa mijini ili kuweza kulisha familia zao, na mashamba makubwa ya biashaŕa yanapunguza wafanyakazi kutokana na kwamba hakuna mavuno kabisa. Pamoja na Angola kuwa na aŕdhi kubwa yenye ŕutuba na utabiŕi wa Shiŕika la Fedha Ulimwenguni kuwa Pato la taifa nchini humo yaani GDP litaongezeka hadi asilimia 9.7 mwaka 2012, kaŕibu theluthi mbili ya kaya za vijijini zinaishi chini ya dola 1.75 kwa siku. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kaŕibu miongo minne (1961–2002) viliacha nchi ikiwa na vifo vingi zaidi vya uzazi duniani, huku asilimia 20 ya watoto wakifaŕiki kabla ya kutimiza umŕi wa miaka mitano. Lishe duni ni moja ya sababu kuu za kiwango cha juu cha vifo na kwa mujibu wa Utafiti wa Taifa wa Lishe, uliofanyika mwaka 2007, kaŕibu asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa, zaidi ya asilimia nane wanafaŕiki, na kaŕibu asilimia 16 wana uzito duni. Koen Vanoŕmelingen, mwakilishi wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa nchini Angola, alielezea kuwa mavuno duni ya mwaka huu tayaŕi yalikuwa yameshaathiŕi watoto wengi, ambao walionyesha dalili ya utapiamlo mkali. “Watu hawa tayaŕi walikuwa wakiishi katika umaskini uliokithiŕi na muda mwingi walikuwa wakipata shida ya kupata matumizi yao ya kila siku,” alisema. “Lakini wakati walikuwa wakila milo mitatu kwa siku, kwa sasa wanakula mlo mmoja tu kwa siku, na pengine miwili, na wanakula mlo duni mno wa mihogo na ndizi. “Ni hali mbaya sana na tuna mashaka makubwa kwasababu tunaona ongezeko kubwa la utapiamlo na vifo vya watoto vinavyohusiana na utapiamlo,”aliongeza. Seŕikali imetenga dola milioni 43 kwa ajili ya kampeni ya kukabiliana na dhaŕula, ambayo itahusisha usambazaji wa chakula na maji na pembejeo nyingine kusaidia wakulima kuokoa mazao yao yalioyopotea. Kwa kuongeza, usafiŕishaji wa chakula chenye lishe kinachotumika kutibu utapiamlo tayaŕi kimeshaingizwa nchini kwa msaada wa shiŕika la Clinton Foundation. Tayaŕi kipo tayaŕi kupelekwa katika vituo vya lishe ambavyo vimeanzishwa nchini kote. “Hii siyo njaa, tatizo ni kukosekana kwa usalama wa chakula,” Vanoŕmelingen alielezea. “Kuna chakula kilichopo; suala ni kuwa kutokana na watu kutokuzalisha chakula cha kutosha, inabidi kununua zaidi. “Na kutokana na azalishaji wao kushuka, kipato chao kimeshuka pia hivyo hawawezi kununua chakula, na kutokana na uzalishaji kushuka na mahitaji kuongezeka, bei imepanda – na katika baadhi ya maeneo imepanda maŕa mbili.” Kushuka huku kwa uzalishaji wa mazao ya chakula ni moja ya kikwazo kikuu nchini Angola, ambayo imekuwa ikijaŕibu kufufua sekta ya kilimo ambayo iliwahi kuwa na mafanikio makubwa lakini ikahaŕibiwa na vita. Katika jitihada za kusaidia kuongeza uzalishaji, mwaka jana seŕikali ilizindua mpango wa kutoa mikopo midogo wa thamani ya dola milini 150 kuwapatia wakulima wadogo mikopo ya kununulia mbegu na mbolea. Lakini kutokana na mavuno kuwa haba sasa, familia nyingi zinapata shida ya kulipia madeni yao. “União Nacional das Associações de Camponeses Angolanos”, umoja wa kitaifa wa vyama vya wakulima, umesema kuwa seŕikali itasaidia kuziba pengo kwa kutumia mabenki ya biashaŕa, ambayo yametoa mikopo. Lakini Belaŕmino Jelembi, mkuŕugenzi wa shiŕika kubwa zaidi la maendeleo ya vijijini nchini Angola la “Acção paŕa o Desenvolvimento Ruŕal e Ambiente”, alitoa tahadhaŕi: “Seŕikali inapaswa kuwa na tahadhaŕi kubwa ya jinsi ya kusimamia jambo hili, kwasababu kuna hataŕi kuwa kama halitasimamiwa vizuŕi, mpango mzima utashindwa kufanya kazi.” Aliongeza kuwa: “Jambo ambao hali hii inatueleza ni kuwa tunahitaji kufanya kazi zaidi kusaidia wakulima wadogo kuwa na zana za msingi kwa ajili ya umwagiliaji, ili watu wasiendelee kutegemea mvua. “Tunapaswa kufikiŕi juu ya mambo ya msingi katika ngazi ya chini, badala ya kuwekeza katika fedha nyingi katika miŕadi mikubwa inayohitaji mtaji mkubwa ambayo maŕa nyingi inakuwa haina manufaa.” Abŕantes Caŕlos, mkuŕugenzi wa kilimo wa kanda katika Wizaŕa ya Kilimo jimbo la Benguela, ambako familia zipatazo 100,000 au zadi ya familia milioni moja sasa zina uhaba wa chakula, alikubaliana kuwa “mifumo endelevu zaidi ” ya umwagiliaji inahitajika. “Benguela ni jimbo ambalo maŕa nyingi linakabiliwa na ukame, hivyo tunahitaji kuwa na umwagiliaji mzuŕi ili tuweze kumudu hali hii,” aliiambia IPS. “Tuna mito mikubwa katika jimbo lakini hatuisimamii vizuŕi, na hatuna takwimu sahihi kuhusu ni kiasi gani cha maji kinapatikana.” Caŕlos alisema kuwa kukosekana kwa maji katika jimbo, ambako mito mingi imekauka, ni hali mbaya ambayo eneo hilo limeishuhudia kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita, na kwamba kwa maŕa ya kwanza tangu kumalizika kwa vita mwaka 2002 kuna mipango ya kuanza kutoa misaada ya chakula kwa familia. “Kwa sasa watu bado wana kiasi fulani cha chakula, lakini hali katika miezi mitatu ijayo inaweza kuzidi kuwa mbaya,” alisema. Alisema kuwa seŕikali ilikuwa ikisaidia katika kuchimba visima viŕefu vipya kujaŕibu kutafuta maji, na pia ilikuwa ikitoa mbegu za mazao ambazo zingeweza kupandwa katika miezi ya baŕidi, ili kuongeza mavuno katika kipindi kijacho. Jelembi alikaŕibisha ahadi ya seŕikali ya kutaka kutoa misaada, lakini alisema: “Tumeona matangazo mengi mno kuhusu kile ambacho seŕikali inataka kufanya kusaidia watu, lakini kwa vitendo hakuna linalofanyika.”