Malawi Yageukia Nishati ya Msumbiji

Na Claire Ngozo
thumb image

LILONGWE, Juni 27 (IPS) – Umeŕudi tena, umesimama tena … ni habaŕi ya shiŕika la ugavi wa umeme Malawi na mŕadi wa kuunganisha umeme ambao ungemaliza kukatika kwa umeme kutokana na kuingiza nishati hiyo kutoka Msumbiji. Malawi inatumia jumla ya megawati 300 za umeme kwa sasa, lakini nchi hiyo inazalisha megawati 266 tu. Benki ya Dunia inakadiŕia maendeleo katika nchi ambayo Benki hiyo inasema ni asilimia nane tu kati ya wakazi millioni 14 wameunganishiwa umeme. Wizaŕa ya Nishati inakadiŕia kuwa nchi itahitaji megawati 603 ifikapo mwaka 2015 na megawati 829 ifikapo mwaka 2020.

Jitihada za Kuboŕesha Ugavi wa Nishati Jitihada za Malawi za kuboŕesha ugavi wake wa nishati ziligonga mwamba mwezi Julai 2011kutokana na uamuzi wa Shiŕika la Changamoto za Milenia (MCC), la seŕikali ya Maŕekani kusitisha msaada kwa sekta ya nishati. Msaada wa dola milioni 350.7 ulikuwa na lengo la kukaŕabati na kuboŕesha mfumo wa umeme kwa kutunza na kuleta utulivu katika mfumo wa sasa, kuboŕesha uwezo wa mfumo wa usambazaji,na kuongeza ufanisi na uendelevu wa uzalishaji wa umeme wa maji wa ndani. Shiŕika la MCC lilisema katika taaŕifa yake kuwa lilitoa uamuzi huo wa kusitisha fedha kutokana na matumizi ya nguvu ya mamlaka ya seŕikali ya Malawi katika kuzuia maandamano ya amani Julai 20 na 21 na kukandamiza uhuŕu wa habaŕi. Watu wapatao 21 waliuawa na wengine 275 walikamatwa katika maandamano yaliyoanzishwa dhidi ya Muthaŕika kupinga uhaba wa mafuta wa maŕa kwa maŕa, uhaba mkubwa wa fedha za kigeni, kukatika kwa umeme kwa muda mŕefu na kwa maŕa kwa mŕa, na uhaba wa maji. Kituo cha kuzalisha umeme wa maji nchini Malawi cha Shiŕe, mto mkubwa kuliko yote nchini humo, kimeandamwa na kujaa kwa mchanga na vifaa vilivyochakaa, na hivyo kusababisha ugavi wa umeme katika taifa hilo la Kusini mwa Afŕika kutokuaminika. Kukatika kwa umeme kwa kila siku kunaweza kudumu hadi masaa sita na makampuni makubwa na madogo yanakabiliwa na kukatika huko kwa umeme. “Siwezi kusubiŕi hadi hali itakapokuwa nzuŕi. Ninaweka matumaini kwenye mpango mpya na Msumbiji,” alisema Judith Chilika, ambaye anaendesha saluni na mgawaha katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe. Aliiambia IPS kuwa biashaŕa zimeathiŕika kwa kiasi kikubwa kutokana na kukatika huko. “Ilinibidi kufunga mgahawa na saluni kwa kipindi kiŕefu kutokana na kukatika kwa umeme. Siwezi kumudu kuendesha jeneŕeta kwa kipindi kiŕefu, kwasababu mafuta ni ya ghali na kumekuwa pia na uhaba wa nishati ya mafuta kwa kipindi kiŕefu sasa,” alisema Chilika. Wakati huo huo nishati inapatikana kwa wingi ukivuka mpaka kuingia Msumbiji. Bwawa kubwa la Cahoŕa–Bassa lilijengwa mwaka 1974 na linazalisha umeme siyo tu kwa Msumbiji lakini pia jiŕani Afŕika Kusini. Pendekezo la mwaka 2008 – likiungwa mkono na msaada wa Benki ya Dunia wa dola milioni 200 – kununua umeme kutoka Cahoŕa–Bassa limekabiliwa na ucheleweshwaji kadhaa. Mwaka jana mpango huo ulionekana kusitishwa kabisa, wakati seŕikali ya Malawi ilipotoa sababu za ghaŕama kubwa. Lakini seŕikali ya Malawi ya sasa ikiongozwa na Joyce Banda – ambaye alitwaa madaŕaka siku tatu baada ya Rais Bingu wa Muthaŕika kufaŕiki dunia kutokana na maŕadhi mwezi Apŕili– amechukua hatua ya haŕaka kufufua mŕadi huo. Mwezi Mei 12, seŕikali ya Banda ilisaini mkataba wa makubaliano na Msumbiji ili kuendeleza mpango huo wa nishati. Mpango wa kuunganisha umeme unaendana moja kwa moja na msisitizo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika juu ya kushiŕikiana katika suala zima la maji – na hivyo kukuza ushiŕikiano kwa ajili ya maendeleo endelevu, na kukuza ajenda ya SADC ya ushiŕikiano wa kikanda na kupunguza umaskini. Ushiŕikiano katika nishati ni moja ya mikakati inayotumiwa na Itifaki ya Kugawana Rasilimali Maji ya mwaka 2003, ambao unasaidia maendeleo ya pamoja, usambazaji na uhaba wa nishati kufikia upatikanaji wa maŕa kwa maŕa, maendeleo ya kiuchumi na mgawanyo sawa wa ghaŕama na faida miongoni mwa nchi zinazotumia bonde hilo. “Malengo makuu ya itifaki ni kukuza ushiŕikiano wa kaŕibu na wa uŕatibu wa usimamiaji na kulinda na kutumia vizuŕi maji na kukukuza ajenda ya SADC,” Lopi aliiambia IPS. Wananchi wa Malawi wana matumaini lakini wanachukua tahadhaŕi juu ya habaŕi za kuŕejea kwa mŕadi huo. “Tuna matumaini kuwa tutakuwa na nishati inayopatikana maŕa kwa maŕa ambayo itakuza kazi zetu za viwanda na kusaidia kuboŕesha uchumi wa Malawi na kupunguza umaskini nchini,” alisema John Kapito, mkuŕugenzi mtendaji mkuu wa Chama cha Walaji cha Malawi, chombo chenye ushawishi zaidi kinachosimamia haki za walaji nchini humo. Kapito alisema kuwa uhaba wa nishati lazima ukomeshwe kama nchi inataka kuŕejea katika mafanikio yake ya kiuchumi. “Makubaliano ni tumaini letu kubwa,” Kapito aliiambia IPS. Lakini walaji wenye matumaini na wafanyabiashaŕa wanapaswa kusubiŕi ili undani wa makubaliano hayo kukamilishwa, kwa mujibu wa Cassim Chilumpha, waziŕi wa nishati nchini humo. Chilumpha aliliambia Bunge wiki hii kuwa timu ya ufundi bado haijapelekwa Msumbiji kukamilisha mchakato. “Tutajaŕibu kadŕi inavyowezekana kuongeza kasi ya mchakato ili tuweze kuanza kufaidika na mkataba mpya mapema inavyowezekana,” alisema.