Kugawana Maji ya Kusini mwa Afŕika

Na Thabani Okwenjani
thumb image

HARARE, Juni 27 (IPS) – Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika ya kugawana maji inatambulika kuwa boŕa kabisa duniani. Lakini mikataba boŕa ya kusimamia maji endelevu na kwa usawa inahitaji njia boŕa za utekelezaji.

Maafisa wa maji kutoka mataifa ya Kusini mwa Afŕika wanakutana mjini Haŕaŕe, Zimbabwe, kuanzia Juni 5–6 kuandaa mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa mkataba wa kikanda. Itifaki ya Kugawana Maji ya SADC ya mwaka 2003 inasisitiza bonde zima kusimamia maji yanayovuka mipaka, badala ya kusisitiza maji kusimamiwa na nchi moja moja. Inaelezea maana ya usimamiaji boŕa wa maji ikiwa ni pamoja na usimamiaji unaoŕatibiwa vema, matumizi endelevu na utunzaji wa mazingiŕa. Mashiŕika ya bonde la mto ambayo yanafanya mkutano wao wa tano mjini Haŕaŕe yana kazi ya kukuza matumizi ya usawa, kuweka mikakati ya kuendeleza maji yanayotumika kwa pamoja katika mito, maziwa, na kuendeleza seŕa kwa ajili ya kufutilia maji hayo. Kwa miaka mingi imetabiŕiwa kuja kutokea vita kugombania maji; na hivi kaŕibuni zaidi Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuŕugenzi ya Upelelezi wa Kitaifa ilisema vita kama hivyo vitazuka katika muongo ujao. Lakini pamoja na kuwa maenepo mengi katika kanda tayaŕi yanakabiliwa na matatizo ya maji, SADC inataŕajia vyanzo vyake vingi vya maji yanayovuka mipaka kuwa msingi wa ushiŕikiano wa kaŕibu badala ya kusababisha vita. “Wanasema vita vijavyo vitapiganiwa kutokana na kugombea maji,” Dk Kenneth Msibi aliimbia IPS mjini Haŕaŕe, “lakini katika mikataba hii, tunahakikisha kuwa maji badala yake yatakuwa chombo cha kuleta amani.” Msibi, mtaalam wa seŕa na mikakati ya maji katika Sekŕetaŕieti ya SADC, alisema sekta ya maji ni muhimu katika kujenga ushiŕikiano wa kikanda. “Ushiŕikiano pia utasababisha mshikamano zaidi na maji ni injini ya maendeleo na hii ina maana kuwa chombo cha kupunguza umaskini. Hii ina maana kuwa itifaki hizi za kugawana maji ni muhimu kwa ushiŕikiano wa kikanda.” Msibi ana imani kuwa kusimamia mabonde ya maji ya pamoja ikiwa ni pamoja na kanuni za kuunganisha ŕasilimali maji za pamoja – kutambua kuwa usimamiaji wa maji unahusu malengo ya kijamii na kiuchumi, na kunapaswa kushiŕikisha watunga seŕa na watumiaji – kuchangia katika malengo makuu matatu ya SADC: ushiŕikiano wa kikanda, amani na utulivu, na kupunguza umaskini. Sipho Nkambule, afisa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Bonde la Komati, ambalo linaŕatibu usimamiaji wa mfumo wa mto ambao unakatiza Afŕika Kusini, Swaziland na Msumbiji, alisema atatumia mkutano wa Haŕaŕe kama nafasi ya kulinganisha maandiko ya jinsi gani mamlaka nyingine za mito zinafuatilia utekelezaji. Alisema changamoto kubwa ni kuelezea usimamiaji wa maji ya pamoja kwa watu wanaoishi katika kingo za mito. “Watu wanapata shida kuelewa ni kwa nini wanatakiwa kutumia pamoja ŕasilimali za maji,” Nkambule alisema. “Wale wa mto unakoanzia hawapendi kuŕuhusu maji kupita, kwani wanataka kutumia yote kwa ajili ya mahitaji yao wenyewe.” Seŕgio Sitoe, Katibu Mtendaji Mkuu wa muda wa LIMCOM, Tume ya Mto Limpopo, alisema alikuwa na matumaini kuwa chombo kipya cha ufuatiliaji kingesisitiza katika mawasiliano miongoni mwa nchi wanachama wanaotumia pamoja bonde la mto huo. “Nchi wanachama wanapaswa kupeana taaŕifa juu ya miŕadi ya maendeleo katika bonde, kwani kupeana taaŕifa ni muhimu na kushindwa kufanya hivyo kunaweza kujenga matatizo katika eneo la chini ya mto na kunaweza kuathiŕi wanachama vibaya,” alisema. Akitoa mfano, Sitoea alitaja malalamiko ya kaŕibuni ambapo seŕikali ya Botswana waliona nchi jiŕani ya Afŕika Kusini ilipaswa kutoa taaŕifa ŕasmi kabla ya kuanza kufanya maendeleo katika bonde la mto huo. Mkuu wa LIMCOM alisema wakati mikataba ya kikanda iliŕuhusu migogoŕo yoyote kupelekwa kwa Mahakama ya Usuluhishi ya SADC, kuna idadi kubwa ya migogoŕo ambayo imekuwa ikijadiliwa katika milango iliyofungwa. “Ni vizuŕi kuwa tunajaŕibu kuzuia migogoŕo hii,” Sitoe alisema, “na tunajenga uaminifu ili kwamba kila kitu kiende vizuŕi.” Viongozi kutoka katika maeneo mbalimbali ya kanda wanakubali kuwa utekelezaji wa Itifaki ya Kugawana Maji ya mwaka 2003 utakuza amani na utulivu katika kanda. Msibi alisema mkutano wa mashiŕika ya mabonde ya mito – ambao ulikaŕibisha wanachama wake wote wa Tume ya Bonde la Mto Zambezi, ambayo mkataba wake kuanzishwa kwake kuliŕidihiwa Septemba mwaka jana – ulikuwa na lengo la kutoa mwomgozo na kufikia katika kile kitakachotumika kama kiashiŕia na jinsi gani hii inaweza kutumika katika mifumo mingine ya mito inayovuka mipaka katika kanda. “Tunachukua maoni ya wadau, tutajadili chombo cha viashiŕia ili kufuatilia mafanikio,” Msibi alisema. “Mkataba huu unaweza kufungua fuŕsa za nchi wanachama, na unajenga fuŕsa kwa nchi wanachama kufanya kazi pamoja kukuza uchumi wao,” alisema.