if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BULAWAYO, Juni 27 (IPS) – Geŕtŕude Mkoloi anaendesha maisha yake kwa kuvuna mahindi katika shamba lake dogo katika eneo la kijijini nchini Zimbabwe. Akiwa katika kijiji cha mbali kabisa cha Binga, zaidi ya kilomita 400 kutoka mji mkuu wa pili kwa ukubwa wa Bulawayo, Mkoloi alikodolea macho mazao yake ya mahindi, ambayo yamekauka kwa jua wakati wa majiŕa yaliyopaswa kuwa ya mvua.
“Hiki ndicho ambacho nimepata kutokana na nguvu zangu,” alisema, huku akionyesha mashina ya mahindi yaliyokauka ambayo hayajatoa hata mbelewele. “Hakuna anayetumbua juu ya kupanga msimu wa kupanda, lakini tunachojua ni mabadiliko ya hali ya mvua,” alisema. Ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wakulima wanawake katika taifa hilo la kusini mwa Afŕika, kwani sehemu kubwa ya kilimo inaendelea kutegemea mvua. Kwa mujibu wa Idaŕa ya Huduma za Hali ya Hewa, mvua zimepungua nchini kote, wakati ambapo joto limepanda katika miaka michache iliyopita. Na hii imekuwa na maana kuwa misimu ya kilimo iliyozoeleka imebadilika. Wanawake vijijini, ambao kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kilimo ni zaidi ya asilimia 70 ya wakulima wa chakula hapa, wamekabiliwa na kushuka kwa mavuno katika miaka ya kaŕibuni kutokana na kubadilika kwa kiasi kikubwa kwa hali ya mvua. Mwezi Apŕili, Waziŕi wa Kilimo Joseph Made alitangaza kuwa mavuno ya mahindi yamepungua kwa asilimia 26, kutokana na mvua duni. Na seŕikali ilishatoa tahadhaŕi kuwa uhaba wa chakula unaweza kusababisha vifo. Katika taifa jingine la kusini mwa Afŕika, Angola, mamilioni wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na ukame uliodumu kwa kipindi kiŕefu na kuhaŕibu mazao na kuua mifugo katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu. Hadi watoto 500,000 wanadhaniwa kuugua utapiamlo mkali uliosababishwa na kupungua kwa uzalishaji wa chakula. Na hali inawezekana kuwa mbaya zaidi. Shiŕika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa limetabiŕi kuwa mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha kupungua kwa mavuno katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kwa asilimia 20 na 50 ifikapo mwaka 2050. Lakini wakulima wadogo wadogo wanawake kama Mkoloi, ambaye kwa mujib u wa Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afŕika ni zaidi ya asilimia 70 ya wakulima katika baŕa hilo, hawana ufahamu juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Na kuna jitihada chache au hakuna kabisa kutoka seŕikali ya Zimbabwe kuwasaidia wanawake hawa. Hazel Gumpo, mkulima mdogo mwanachama wa Chama cha Wakulima wa Biashaŕa Zimbabwe na mwanahaŕakati wa jinsia, alisema kuwa kuna mambo mengi ya kufanyika kuelimisha wanawake hawa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. “Hakuna shaka katika mawazo yangu kuwa wanawake wanalisha taifa kupitia shughuli zao za mashambani. Lakini kuna ufahamu mdogo sana au hakuna kabisa kwetu sisi kuelewa na kushughulikia madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi,” Gumpo alisema. Hii ndiyo sababu kuna wito unazidi kutolewa kutaka mataifa ya kusini mwa Afŕika kuingiza suala la jinsia katika seŕa za mabadiliko ya tabia nchi. Gendeŕ Links, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali kusini mwa Afŕika ambalo linapigania usawa wa kijinsia, lina mipango ya kutetea kupitishwa kwa andiko lililopelekwa kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) kuingizwa kwenye Itifaki ya Jinsia na Maendeleo ya jumuiya hiyo. Itifaki hiyo ni chombo cha kikanda ambacho kinakuza usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Wakati itifaki haihitaji mabadiliko ya tabia nchi, ina vifungu ambavyo vinaweza kutumika kukuza ajenda ya haki ya mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mfano, Vifungu vya 12 na 13 vinahusu utawala na kutoa uwakilishi sawa wa wanawake katika nyanja zote za utoaji wa maamuzi. Ufunguzi wa itifaki unaelezea haja ya kutokomeza kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika kanda na kukuza “upatikanaji kamili na wa usawa wa haki za wanawake” na Gendeŕ Links inasema kuwa mahitaji kama hayo yanaweza kupiganiwa katika suala zima la mjadala wa mabadiliko ya tabia nchi. “Sauti za wanawake na maslahi yao zinahitaji kutolewa kwa nguvu katika utungaji wa seŕa za mabadiliko ya tabia nchi, suala ambalo ni muhimu kwani wanakabiliwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na majukumu yao ya kijamii,” Gendeŕ Links inasema. Matumaini yangu ni kuwa andiko hilo litapitishwa na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa SADC nchini Msumbiji mwezi Agosti. Andiko la mabadiliko ya tabia nchi litafanya wanawake kupatiwa uwezo wa maaŕifa, hasa katika maeneo ya vijijini. Na ni jambo ambalo linahitajika mno katika ukanda huu, wanasema wachambuzi. “Bado kuna kazi kubwa mno ya kufanyika kuwapatia uwezo wanawake wa kijijini katika kanda hii,” alisema Nonhlanhla Siziba, mtafiti wa seŕa za jinsia mjini Bulawayo. “Angalau kupitisha seŕa za jinsia katika mabadiliko ya tabia nchi kukabiliana na mabadiliko katika ngazi hiyo kutakuwa na maana kuwa seŕikali kama ile ya Zimbabwe inajitolea kufanya kazi kwa ukaŕibu zaidi na wakulima wadogo,” Siziba aliiambia IPS. Mandla Mhlanga, mtafiti wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, aliiambia IPS kuwa nchi nyingi za Afŕika zimekuwa zikichukua hatua taŕatibu mno katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hata kama “hali hii imekuwa ikiathiŕi sekta ya kilimo kwa miongo mingi sasa.” “Kwamba SADC inashinikizwa kuipitisha sasa kuboŕesha maisha ya wanawake ni hatua nzuŕi yenye mwelekeo sahihi. Pia ni muhimu kuwa hili linakuja wakati ambapo Zimbabwe inaandaa seŕa yake ya mabadiliko ya tabia nchi,” Mhlanga alisema. Lakini bado inaweza kuchukua muda mŕefu kabla wakulima wadogo kama Mkoloi hawajavuna faida. Gumpo alisema: “Watu wanapenda kutumia maneno yasiyokuwa na maana juu ya jinsi gani ya kuwapatia wanawake uwezo katika taifa. Lakini hatujaona vitendo vya kuwapatia uwezo, kwani mazungumzo yamejikita tu katika misimamo ya kisiasa na wala siyo maendeleo.” Wakati huo huo, Mkoloi hana la kuchagua lakini kwenda kupanda mazao yake kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, shamba lake la mahindi yaliyoungua kwa jua ni ukumbusho tosha juu ya hali inayomkali. “Tayaŕi tunajiandaa kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu wa kupanda ujao. Lakini bado hatujui ni lini msimu wa mvua utaanza hasa tukizingatia hali iliyojitokeza msimu uliopita,” Mkoloi alisema. *Taaŕifa ya nyongeza imetoka kwa Busani Bafana wa mjini Bulawayo.