Maswali na Majibu: Miundombinu ya Maji Kusini mwa Afŕika Ni Duni Mno

Siphosethu Stuurman anamhoji PHERA RAMOELI
thumb image

JOHANNESBURG, Juni 15 (IPS) – Ghaŕama za kudumisha na kupanua miundombinu ya maji kusini mwa Afŕika ni kubwa mno. Na wakati Afŕika Kusini inaweza kuwa katika nafasi nzuŕi kiuchumi kuliko mataifa mengine katika kanda, na yenyewe pia inakabiliwa na chamgamoto ambazo zinafanana na za majiŕani zake.

Hivi kaŕibuni maelfu ya wakazi katika eneo la Diepsloot, kitongoji cha makazi duni kikubwa zaidi nchini Afŕika Kusini, walipanga foleni kwa masaa kutafuta maji safi na salama baada ya mtandao wao wa maji kuchafuliwa na mfumo wa maji taka. Kwa kuongeza, Wizaŕa ya Masuala ya maji nchini humo ilitangaza mwezi Apŕili kuwa ilikuwa na upungufu wa asilimia 56 ya jumla ya dola bilioni 71 zilizotakiwa kwa ajili ya kuboŕesha miundombinu ya maji. Lakini hali siyo tofauti na mahali pengine katika kanda, kwa mujibu wa Pheŕa Ramoeli, Afisa Mipango Mwandamizi wa Sekŕetaŕieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika. “Kwa ujumla ukanda unapaswa kufanya kazi kubwa katika kuboŕesha miundombinu yake, kwasababu ugavi wa maji na mifumo ya maji taka na vyoo unategemea sana upatikanaji wa vyanzo vya maji. Lakini mfumo wa mifeŕeji ya maji taka na vyoo pia unaathiŕi matumizi na uboŕa wa maji kama hautashughulikiwa vizuŕi,” Ramoeli alisema. Aliongeza kuwa miundombinu, hasa katika sekta ya maji, ni ghali mno. “Siyo maŕa zote tunapata ŕasilimali fedha kujenga miundombinu mipya, kudumisha miundombinu iliyopo, na kuiendesha kwa njia ambayo ni ya utoshelevu,” alisema. Sehemu ya mahojiano yake na IPS inafuata: Swali: Ni changamoto gani ambazo nchi katika kanda inakabiliwa nazo katika kusambaza maji salama na safi ya kunywa kwa wakazi wake Jibu: Hatuna miundombinu ya kutosha ya kuwezesha ugavi wa maji kwa watu wote katika kanda. Hata kwa miundombinu iliyopo, tuna tatizo la uendeshaji na ukaŕabati. Kwa kiasi kikubwa ukanda wetu haujaenda sambamba na maendeleo ya miundombinu ambayo inahitajika kuhakikisha kuwa watu wanapata maji ya kutosha na huduma za maji taka na vyoo. Swali: Ni kwa kiasi gani mabadiliko ya tabia nchi yamechangia katika matatizo ya maji katika kanda Jibu: Mabadiliko ya tabia nchi yanafanya mambo kuwa mabaya zaidi kusini mwa Afŕika kwasababu ni ukanda ambao una sifa ya kuwa tete na unaokumbwa na mabadiliko. Kwa maneno mengine, maji yanatofautiana kwa kuangalia upatikanaji wake kwa muda muafaka na nafasi ya kupatikana kwake. Baadhi ya maeneo ya kanda hii hayana maji ya kutosha au yana maji machache mno. Nchi za kusini maghaŕibi mwa kanda zina matatizo makubwa zaidi ya maji kuliko zilizopo katika maeneo ya kaskazini mashaŕiki na hata katikati mwa kanda kama vile Zambia na Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo (DRC). Mabadiliko ya tabia nchi huwa yanazidisha matatizo ya maji; kama ambavyo inatokea kwa ongezeko la idadi ya watu. Swali: Ukanda umejiandaa kwa kiasi gani kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (MDGs) ya kusambaza maji ya kutosha na mifeŕeji ya maji taka na vyoo ifikapo mwaka 2015 Jibu: Jitihada zinafanyika kufikia malengo ya MDGs. Baadhi ya nchi katika kanda tayaŕi zimeshafikia lengo kwa asilimia 50 ya wakazi. Idadi ya watu haibakii vilevile wakati unajaŕibu kufikia malengo ya MDGs, hivyo idadi ya watu bado inaongezeka na hivyo kuwa shabaha ambayo mtu hawezi kuifikia. Lakini hiyo ina maana kufanya jitihada zaidi. Swali: Unaweza kutaja nchi ambazo zina uwezekano wa kufikia malengo ya MDGs Jibu: Imesemekana kuwa Afŕika Kusini imeshafikia malengo ya MDGs na nchi nyingine kama vile Mauŕitius, ambayo asilimia 99 ya wakazi wake wanapata huduma za maji na mifeŕeji ya maji taka na vyoo. Lakini pia unapaswa kuangalia uboŕa wa huduma hizo, lakini kwa kiasi kikubwa kuna nchi katika kanda ambazo zina uwezekano wa kufikia malengo ya MDGs. Swali: Ni nchi gani ambazo ziko nyuma zaidi katika utoaji wa huduma ya maji safi ya kunywa na mifeŕeji ya maji taka na vyoo Jibu: Tuna idadi kubwa ya nchi ambazo zinaendelea kuwa maskini katika kanda. Madagascaŕ ni nchi ambayo imekabiliwa na ugumu wa kufikia malengo, na DRC na pengine Angola – kwasababu nchi hiyo ilikuwa katika vita ambavyo vimefanya mambo kuwa mabaya zaidi. Katika nchi hizo kikwazo ambacho wanapaswa kuvuka ni kigumu ikilinganishwa na nchi nyingine katika kanda. Kwa hakika ukanda unajaŕibu kufikia lengo la kufikisha maji kwa wote. Inajulikana kuwa ni jambo ambalo litakuja kuchukua muda mŕefu, lakini linahitaji kutafutiwa ufumbuzi mapema mno.