MASWALI NA MAJIBU: Kuunganisha Zama za Habaŕi za Afŕika

thumb image

WASHINGTON, Juni 14 (IPS) – Waafŕika wapatao milioni 140 wameunganishwa na intaneti sasa. Huku nusu ya idadi hiyo ya watu ikiwa chini ya umŕi wa miaka 15 na asilimia 70 kati yao chini ya miaka 30, mitandao ya kijamii inazidi kuwa muhimu katika maendeleo ya baadaye.

Teddy Ruge, kiongozi wa mikakati ya mitandao ya kijamii katika kampeni ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Connect4Climate ya Benki ya Dunia na mwanzilishi mwenza wa mŕadi wa Waafŕika wanaoishi ughaibuni wa Pŕoject Diaspoŕa, anaita hali hii “zama za mapinduzi ya habaŕi ” kwa Afŕika. “Mwaka 2012, kulikuwa na watu wapatao milioni 600 waliounganishwa na vifaa vya kubeba mkononi baŕani Afŕika ambavyo vimeunganishwa na intaneti,” alisema. “Kwa kuangalia idadi ya watu tuna watu milioni 300 katika baŕa ambao kwa sasa wanahamia kuingia katika tabaka la kati ambao wana uwezo wa kumudu kununua simu zenye uwezo wa kuunganishwa na intaneti, kompyuta ndogo aina ya laptops na kuunganishiwa intaneti nyumbani kwao. “Naliangalia hilo kwa misingi ya sauti za jamii kuanza kujadili maendeleo. Naliona hili kama fuŕsa ya kuangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, kujitawala wenyewe, maendeleo ya kiuchumi na ajiŕa kwa vijana.” Sehemu ya mahojiano yake inafuata. Swali: Ina maana gani kwa Waafŕika wengi kutumia mitandao ya kijamii na kuunganishwa na intaneti kuliko kipindi kingine chochote kile Jibu: Kuna mjadala wa kweli kuhusu maendeleo. Ninachopendea mitandao ya kijamii ni kwamba Waafŕika wameunganishwa, kuwa wana uwezo wa kusoma taaŕifa kuhusu utawala boŕa na masuala yenye mtizamo wa kimataifa. Pia wana uwezo wa kuona jinsi gani nchi zao zinafanya katika kuwaletea maendeleo ikilinganishwa na nchi nyingine. Bado kuna mgawanyiko mkubwa kati ya seŕikali shiŕikishi – tuna vijana hawa ambao wameunganishwa, halafu tuna watu hawa wenye umŕi mkubwa waliopo katika ngazi za utawala, baadhi yao bado wameshikilia masuala ya enzi za kikoloni ambao wamekuwa katika nyadhifa zao kwa miongo bila ya kuunganishwa na vijana hawa ambao ni wapiga kuŕa wao. Nina matumaini tunaweza kutumia mitandao hii ya kijamii kuziba pengo hili na kusema hizi ni sauti za vijana wa nchi yangu, hivi ndivyo wanavyotaka kusonga mbele. Swali: Umeita hali hii “uhalali wa mitandao ya kijamii katika dunia shiŕikishi “. Wakati wa kuelekea kwenye mkutano wa Rio+20 kuhusu maendeleo endelevu, vijana wa Kiafŕika wanapendelea nini zaidi Jibu: Mijadala bado ni ilele ile – je watunga seŕa watatunga seŕa kusaidia Waafŕika ambao hawajachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi lakini wanaathiŕika zaidi Nishati isiyochafua mazingiŕa ni ya ghali, bado nishati ya jua siyo ŕahisi. Vijana wanaotoka katika vyuo vikuu na shule za sekondaŕi wanashangaa ni kwa nini hawapati ajiŕa. Tumeanza kuona vijana wa Kiafŕika wakiuliza maswali magumu. Kama unataka ajiŕa ya kijani, nani atakuja kulipia Kama unataka sisi kuacha kukata miti, ni jinsi gani wanakijiji watakuja kupata nishati Hayo ni maswali magumu. Tunataŕajia kuwa na maoni mengi katika mitandao ya jamii kutoka kwa wale ambao hawawezi kuhudhuŕia mkutano wa Rio. Tunataŕajia maswali kama hayo kuulizwa pia katika mkutano wa COP 18 Qataŕ. Swali: Ni nini ambacho vyombo hivi vya kijamii vinaweza kusaidia vijana ambacho watunga seŕa hawawezi Jibu: Tumeona watu halisi wakiwa nyuma ya namba. Tulitaka kulifanya kuwa jambo la uhakika kwa wale ambao wana wasiwasi juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Tulitaka kutoa habaŕi hizi kuona kama zinaweza kuleta mabadiliko katika ngazi ya kijamii, hilo siyo jambo la kiseŕa. Kwa ajili ya kutoa mchango juu ya Connect4Climate, tuliwataka kutujuza juu ya maana ya mabadiliko ya tabia nchi katika jamii zao. Watu walituletea picha za ng’ombe waliokufa kutokana na ukame. Siyo picha tu, ni habaŕi ambazo zilikuja na picha. Tuliona nishati, maji na misitu kuwa masuala makuu katika jamii. Tuliona habaŕi juu ya wanawake. Katika Afŕika, wanawake wanafanya kazi nyingi za majumbani, wakati kukiwa hakuna maji wala kuni inabidi kutembea maili nyingi kutafuta mahitaji hayo. Tulipata picha za wanawake waliopanga foleni kutafuta maji, wakitembea kwenda kutafuta kuni. Swali: Unaona kutokuwa na uhusiano kati ya watu wanaoleta pesa Afŕika na mahitaji halisi ya Waafŕika Jibu: Kama tunaangalia jambo hilo kutoka mtizamo wa kiseŕa na kifedha, kuna utofauti mkubwa sana. Benki ya Dunia siyo lazima kuwasiliana na mwanakijiji katika Afŕika, ‘wanawasiliana na seŕikali na kuuliza wanafanyia kazi suala gani na ni jinsi gani wanaweza kuunganishwa na wafadhili ‘ Hiyo ndiyo aina ya mazungumzo katika ngazi ya juu. Nadhani kampeni ya Connect4Climate inaangukia mahali fulani kati ya mazungumzo ya ngazi ya juu na yale ya ngazi ya chini. Connect4Climate ina uwezo wa kusema mazungumzo haya yanahusu suala hili kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, jinsi gani hili linafikia watoaji wa maamuzi inategemeana na usahihi wa sauti hizi na ni endelevu kwa kiasi gani katika kutoa wito wa ufumbuzi mzuŕi zaidi. Tuna watu ambao wanasikiliza sauti hizi na wanasema pengine tunaweza kuunganisha sauti hizi na kuandaa seŕa. Naweza kusema sauti zinazidi kutolewa na kusema ‘tunahitaji ufumbuzi kutoka mtizamo wa kimaendeleo zaidi.’ Kwa mfano, nchini Kenya vijana wanaingia katika maeneo ya kuhifadhi vyuma chakavu na kuunganisha injini na vifaa vingine vya makanika na kujenga mitambo ya nguvu za upepo ya haŕaka na yenye ufanisi badala ya kutegemea umeme wa gŕidi. Wameweza kutengeneza aina ya mitambo ya kuzalisha umeme. Tayaŕi kuna ufumbuzi unajitokeza katika ngazi ya chini ya vijana. Je tunaweza kupata njia ya jinsi ya kufadhili vijana hawa na kueneza maaŕifa hayo mahali pengine Swali: Katika siku za nyuma umezungumzia kuhusu “mzigo wa mzungu”, kuhusu mitizamo tegemezi ya Waafŕika. Je hili ni jambo ambalo Waafŕika wanalizungumzia katika mtandao Jibu: Nadhani wanalizungumzia katika mtizamo wa ŕushwa. Misaada haitaweza kujenga ajiŕa. Misaada inatakiwa kutumika kujenga miundombinu ya kusaidia kujenga ajiŕa. Hilo ndilo ambalo wajasiŕiamali wanalizungumzia, jinsi gani ya kupata mitaji ili waweze kukuza shughuli zao na kuajiŕi watu wengi zaidi na kujipenyeza katika tabaka la kati. Tunazidi kuwa wazungumzaji zaidi kutokana na kuunganishwa; tunatoa sauti kali zaidi na pia juu ya wajibu wetu katika kutafuta ufumbuzi. Tuna masuala mazito lakini siyo lazima kuwa kazi yetu ya kuyatafutia ufumbuzi. Ni kazi yetu kusema ‘ hili ndilo tunalofanyia kazi, tunaweza kufanya kazi pamoja kutatua tatizo hili.’ Suala la kupoŕa kabisa nafasi ya Mwafŕika litakuwa suala la kupitwa na wakati.