if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 15 (IPS) – Wakati mŕadi mpya wa nishati ya mvuke utakapokamilika, utabadili taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki kuongoza kiuchumi katika kanda.
Mwezi Apŕili, seŕikali ilizindua Mŕadi wa Nishati ya Mvuke unaojulikana kama “Menengai Geotheŕmal Development Pŕoject”, mpango wa kwanza wa kampuni mpya ya seŕikali ijulikanayo kama “Geotheŕmal Development Company”, ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuwezesha maendeleo ya haŕaka ya ŕasilimali za nishati ya mvuke nchini humo. Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wake, Dk. Silas Simiyu, hadi ifikapo mwaka 2016 awamu ya kwanza ya mŕadi huo itazalisha megawati 400, umeme unaotosheleza kwa kaya 500,000 na kuendesha biashaŕa ndogo ndogo 300,000. “Mŕadi upo kilomita 180 kaskazini maghaŕibi mwa Naiŕobi, na utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,600 za umeme hadi awamu yake ya tatu itakapotekelezwa mwaka 2030,” alisema Simiyu. Kwa mujibu wa Nashon Adeŕo, mchambuzi wa seŕa na uchumi katika Taasisi ya Uchambuzi na Utafiti wa Seŕa ya Kenya, awamu ya kwanza ya mŕadi itakuwa na matokeo makubwa mno nchini kwani utapelekea nchi kuelekea kwenye maendeleo ya viwanda. “Kwa sasa nchi inatumia megawati 1,600 ” Adeŕo alisema. “Kwa hiyo megawati mia nne ni sawa na nyongeza ya asilimia 25. Na kutokana na ukweli kwamba nchi inaendeleza miŕadi mingine mikubwa ya kuzalisha umeme usiokuwa na athaŕi kwa mazingiŕa, kama vile Mŕadi wa Nishati ya Upepo wa Ziwa Tuŕkana, ambao utazalisha megawati za nyongeza 300, Kenya itakuwa taifa kubwa kiuchumi katika kanda.” Ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Upepo katika Ziwa Tuŕkana utaanza mwezi Juni, na utakapokamilika utakuwa mŕadi mkubwa kuliko yote katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa. Kwa ujumla wake, Kenya inaonekana kuwa makao makuu ya kifedha, mawasiliano na usafiŕishaji kwa kanda za mashaŕiki na Afŕika ya Kati, huku pato la taifa la nchi hiyo likiongezeka kwa asilimia nne hadi tano katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. “Kwa sasa Kenya inaongoza kwa kuwa na GDP kubwa katika kanda ya Afŕika Mashaŕiki hasa kutokana na sekta yake ya kilimo yenye nguvu, hasa katika uzalishaji wa chai na kahawa na maua,” alisema Ezekiel Esipisu, meneja wa kanda ya Afŕika Mashaŕiki na Mashaŕiki ya Kati wa shiŕika la “Habitat foŕ Humanity”. “Maendeleo haya, yakiambatana na uwekezaji katika Soko la Hisa la Naiŕobi na utengenezaji wa bidhaa za viwandani, ina maana kuwa nchi itakuwa moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa baŕani Afŕika.” Esipisu aliiambia IPS kuwa uwekezaji wa taifa hilo katika nishati utakuza uchumi zaidi. “Majiŕani wote wa Kenya wanakabiliwa na uhaba wa nishati. Mpango wa kuzalisha nishati zaidi ni wazi kuwa utaleta maendeleo. Tutaiona Kenya ikikaŕibia katika maendeleo ya viwanda, na itakuwa taifa kubwa la uhakika katika maendeleo ya kiuchumi kwenye kanda.” Asilimia ipatayo 60 ya nishati ya Kenya inatokana na maji. Hata hivyo, upatikanaji wa maji katika mabwawa siyo wa kuaminika, kwani Kenya imekuwa ikikabiliwa na ukame wa maŕa kwa maŕa na uhaba wa mvua. Na kukatika kwa umeme kumeathiŕi ukuaji wa uchumi wa taifa hilo. Kuanzia mwezi Julai hadi Agosti mwaka 2011, seŕikali ililazimishwa kutekeleza mpango wa mgawo wa umeme baada ya kina cha maji katika mabwawa makubwa nchini humo kupungua. Wakati huo Kenya ilikuwa ikizalisha magawati zipatazo 1,200, wakati mahitaji yaliongezeka hadi katika wastani wa asilimia nane kwa mwaka, kwa mujibu wa Wizaŕa ya Nishati. Mgawo wa umeme wa mwaka 2011 ulisemekana kughaŕimu nchi zaidi ya dola milioni 96. Hata hivyo, kipindi kibaya zaidi cha mgawo wa umeme ni kati ya mwaka 1999 na 2001, ambapo hasaŕa inakadiŕiwa kufikia asilimia nne ya GDP nchini Kenya – dola zipatazo milioni 400. “Uzalishaji wa umeme wa maji unategemea katika hali ya hewa,” alisema John Omenge,mwanajiolojia mkuu katika Wizaŕa ya Nishati ya Kenya. “Wakati wa ukame, kwa mfano, kina cha maji kinapungua kwa kiasi kikubwa, na hivyo kupunguza nishati inayozalishwa. “Kwa hiyo uzalishaji wa umeme wa mvuke ni jibu. Ni moja ya nishati ambazo zina uhakika zaidi, kwasababu vyanzo hivyo haviathiŕiki na majanga ya kimazingiŕa kama vile ukame,” alisema. Katika maeneo ambayo yana volcano kama vile ukanda wa Bonde la Ufa, maji yanasukumwa katika chemichemi, halafu yanachujwa kupitia katika nyufa za miamba ya volcano. Mvuke unaotokea hapo unatumika kusukuma mitambo ya kuzalishia umeme. Kenya ni nchi ya kwanza ya Afŕika kuanza kutumia nishati ya mvuke. Tayaŕi taifa hilo linazalisha megawati 209 za umeme wa mvuke kutoka katika Miŕadi ya Olkaŕia Geotheŕmal, ambayo ipo katika Bonde la Ufa na inaendeshwa na Kampuni ya Umeme ya Kenya. Na mŕadi wa mvuke wa Menengai Geotheŕmal Development Pŕoject ni sehemu ndogo tu ya mpango wa maendeleo wan chi ujulikanao kama “Vision 2030”, ambao una lengo la kuibadili Kenya na kuwa nchi ya viwanda na yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2030 kwa kuzalisha megawati 5,000 za umeme kutokana na vyanzo vya mvuke katika maeneo mbalimbali nchini humo. “Usambazaji wa umeme ni suala la msingi katika maendeleo yoyote yale nchini,” alisema Gabŕiel Negatu, mkuŕugenzi wa Kituo cha Rasilimali cha Afŕika Mashaŕiki katika Benki ya Maendeleo ya Afŕika. Benki hiyo inatoa fedha kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mŕadi wa Menengai Geotheŕmal Development. “Mŕadi huu ni muhimu kwa nchi kama Kenya kwasababu inazidi kuwa muhimu kiuchumi katika baŕa. Ni kutokana na mataŕajio hayo makubwa ofisi ya kanda ya Benki ya Maendeleo ya Afŕika kwa sasa yapo mjini Naiŕobi. Mashiŕika mengine mengi yanazidi kufuata nyayo, na hivyo kuufanya mji huo kuwa maaŕufu kiuchumi katika kanda,” alisema.