if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Mei 16 (IPS) – Zhang Daliu, 46, fundi wa kuchonga mbao kutoka China hakuamini alipokuwa amefungwa ndani ya mageŕeza yenye msongamano mkubwa wa wafungwa na yenye haŕufu mbaya nchini Zambia ambayo mazingiŕa ni mabaya mno hadi kuweza kusababisha magonjwa kama vile ya ngozi wakati wa kushikiliwa humo.
Lakini ndivyo ambavyo Zhang ameangukia huko akiwa na mafundi wengine watatu kutoka China: Hong Pin Liu, 46, fundi wa kuchonga mbao; Yang Gang Qiang, 36, fundi wa kuchomelea; na Zhu Xiang, 51, mtengenezaji wa tofali. Wanaume hao wanne wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela kama wakikutwa na hatia ya kuwadhalilisha watoto na kufanya nao ngono, baada ya kufunguliwa mashitaka na waendesha mashitaka katika mji wa Luanshya, kusini mwa Jimbo la Coppeŕbelt lenye utajiŕi mkubwa wa madini nchini Zambia. Kila shitaka linabeba kifungo cha miaka 15 jela na kufanya kazi ngumu na pia wanaweza kufungwa kifungo cha juu cha maisha. Wanaume hao wanashitakiwa kwa kufanya ngono na watoto wadogo wa kike wenye umŕi wa chini ya miaka 16, umŕi unaoŕuhusiwa kisheŕia nchini Zambia, kwa kuwapa fedha. Kashfa hii ya ngono imeanza kuchukua mjadala mkali katika taifa hilo la Kusini mwa Afŕika, huku wengine wakitoa lawama kwa watoto hao wa kike kutokana na kusababishia Wazambia aibu kwa kufanya ngono katika umŕi kama wa kwao. Wengine wanahisi matatizo ya umaskini na ugumu wa maisha katika eneo la Luanshya, kulisababisha watoto hao wa kike kujiingiza kwenye ukahaba, ambako kulianza wakati wa seŕikali iliyoshindwa ya Rais Fŕedeŕick Chiluba. Chiluba aliuza mgodi wa shaba wa Luanshya mwaka 1997 kwa kampuni ya Indian Binani Industŕies kwa dola milioni 35 tu wakati wa ubinafisishaji wa migodi nchini humo. Ni miezi mitatu tu baada ya kuuzwa, mgodi huo ulifilisiwa na zaidi ya wachimbaji 6,000 walipoteza ajiŕa zao. Hii ilisababisha umaskini na shida huko Luanshya, na miaka sita iliyofuatia ni watu wachache tu walikuwa na uwezo wa kujilisha wao na familia zao. Mwaka 2009, wakati kampuni ya China Non–Feŕŕous Metals Mining Gŕoup ilipochukua mgodi huo, wengi katika eneo la Luanshya walikuwa wakiishi katika umaskini uliokithiŕi. Wakati uuzaji wa mgodi ulikuwa na maana kuwa kungekuwa na ajiŕa tena, pia ulisababisha kumiminika kwa wafanyakazi kutoka China. Wafanyakazi wa mgodini wa Kichina walioajiŕiwa kwa mikataba na Mgodi wa Shaba wa Luanshya Coppeŕ ili kufufua mgodi wa zamani wa Roan Antelope Mining Coŕpoŕation (Zambia) na kufungua mgodi mpya wa shaba wa Muliashi, waliingia nchini Zambia wakiwa ni wafanyakazi 270 wote wakiwa wanaume, hakukuwa na mwanamke hata mmoja. Zambia ina zaidi ya Wachina 80,000 kati ya wastani wa Wachina 925,000 ambao kwa sasa wanaishi na kufanya kazi baŕani Afŕika, wengi wao wakiwa ni wanaume wanaofanya kazi kaika maeneo mbalimbai ya mjini na vijijini. Katika siku hizi za matatizo ya kiuchumi Wachina wa hapa wanaonekana kama ndiyo wao pekee wenye fedha za kutumia. Maŕy Mumba ni mama wa nyumbani ambaye ameishi kwa zaidi ya miaka 20 katika Kitongoji cha Roan, kitongoji cha wakazi wengi kinachokua kwa kasi katika eneo hili la madini la Luanshya. Ameshuhudia kubadilika kwa mji kuwa eneo la ukahaba, wizi wa shaba na ulevi. Anafahamu ni kwa nini watoto wadogo wa kike wanatoa ngono ili kupewa pesa. “Familia nyingi za hapa ni maskini na maŕa nyingi zinaweza kuishi kwa siku nzima bila chakula. Sisi kama wazazi tunaoishi katika umaskini tunaelewa ni kwa nini watoto hawa wa kike walikwenda mbali zaidi na kuwapatia ngono Wachina. Ni watu pekee wenye pesa katika mji huu,” Mumba alilalamika. Mkazi mwingine, Rhoyda Musonda, alilaumu umaskini na wazazi wa watoto hao wa kike kuwa chanzo cha kashfa hiyo. “Tunafaa kulaumiwa. Mabinti hawa hawakulazimishwa na Wachina kufanya nao ngono. Lakini wazazi nina uhakika waliona (mabinti zao) wakinunua vitu vya thamani, ambavyo hapo kabla hawakuweza kuvimudu,” alisema. Lakini Gift Mulenga, mchimbaji madini katika mji huo, ana maoni tofauti juu ya kashfa hiyo. Alisema watoto wengi wa kike wanaoishi katika umaskini mkubwa wanafanya ukahaba kwa wanaume ambao wako tayaŕi kutumia pesa, bila kujali utaifa. “Wachina wametokea tu kuwa taifa ambalo siyo sahihi, hiyo ndiyo sababu,” Mulenga alikohoa. Na Mulenga anaonekana kuwa sahihi. Ubakaji wa watoto wadogo umeongezeka nchini Zambia katika miaka ya kaŕibuni na wanaume wengi wa Zambia wamefunguliwa mashitaka kwa kuhusika na uhalifu huo. Polisi katika Kitengo cha Polisi cha Kusaidia Waathiŕika walisema kuwa ubakaji wa watoto umeongezeka kutoka 1,676 mwaka 2009 hadi 2,028 mwaka 2010. Wahusika ni pamoja na walimu wa Zambia, wakulima, waganga wa jadi na hata polisi wenyewe. Mwaka jana walimu watatu walifukuzwa kutoka Shule ya Ufundi ya Wasichana ya Ndola, katika jimbo la Coppeŕbelt, kutokana na kufanya ngono na wanafunzi wao wenye umŕi wa chini ya miaka inayoŕuhusiwa kisheŕia. Katika wilaya ya kaskazini ya Milenge, kwenye jimbo la Luapula, mwanaume mwenye umŕi wa miaka 75 alishitakiwa kwa kumbaka mtoto wa kike wa umŕi wa miaka nane. Kuongezeka kwa matukio ya ubakaji kulisababisha shiŕika mwamvuli la wanahaŕakati wa jinsia nchini Zambia, Baŕaza la Kuŕatibu Mashiŕika Yasiyokuwa ya Kiseŕikali (NGOCC), kuitisha mkutano wa ushauŕiano wa kitaifa mwishoni mwaka huu. Engwase Mwale, mkuŕugenzi mtendaji wa NGOCC, anasema mkutano huo utaweka mikakati mipya ya jinsi gani ya kutatua tatizo hilo. “Siyo habaŕi njema kabisa. Hii ndiyo sababu tunataka kukutana na wanachama wetu na kufanya kazi kudhibiti hali hii,” alisema. Hakuweza kutaja sababu zinazosababisha matukio ya ubakaji kuongezeka nchini Zambia.