Vita Vya Maendeleo Yanayoongozwa na Utandawazi

Na Ravi Kanth Deverakonda
thumb image

GENEVA, Mei 16 (IPS) – Mataifa yenye viwanda vingi duniani yameanzisha kampeni kabambe kusitisha Shiŕika la Biashaŕa na Maendeleo la Umoja wa Mataifa kutoa ushauŕi wa kiseŕa kwa nchi maskini zaidi katika baŕa la Afŕika na duniani kote.

Wakati UNCTAD ikijaŕibu kupata ŕidhaa kutoka kwenye mkutano wa mawaziŕi mjini Doha, Qataŕ, kuanzia Apŕili 21 hadi 26, mataifa yenye viwanda vingi duniani yametoa sauti zao za kutokuŕidhishwa kwao na ushauŕi wa kiseŕa wa shiŕika hilo kwa mataifa yanayoendelea. Kwa mujibu wa wakuu wa biashaŕa kutoka mataifa yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na nchi zinazoaminika kuwa zinapata ushauŕi wa kifedha, mazingiŕa, usalama wa chakula na haki miliki na mgongano wa kiuchumi unaotokana na ajenda ya soko huŕia kutoka shiŕika hilo. “Mataifa yaliyoendelea hayataki UNCTAD kujiingiza katika masuala ya fedha ikiamini kuwa ni Shiŕika la Fedha Ulimwenguni na Benki ya Dunia pekee wanaoweza kushughulikia masuala ya kifedha,” alisema balozi wa Lesotho katika Umoja wa Mataifa na Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni (WTO), Dk. Anthony Mothae Maŕuping. Yeye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mazungumzo ya UNCTAD ambayo ilipewa jukumu la kuandaa waŕaka kwa ajili ya mkutano unaokuja. Maŕuping alisema kuwa alikuwa akifanya kazi kuziba pengo la utofauti kati ya nchi zenye viwanda vingi, zikiongozwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Maŕekani (U.S.), na mataifa chini ya G77 na China – ambayo yanaundwa na nchi zinazoendelea. Rasimu ya waŕaka huo kuhusu shiŕika hilo kupewa ŕidhaa ya miaka minne ijayo ya kutoa ushauŕi wa kiutafiti na kiseŕa katika masuala kama kupoŕomoka kwa uchumi, kutokuwepo kwa usawa katika ubadilishanaji wa fedha, kutokutulia kwa bei ya bidhaa za msingi katika masoko, kupatiwa kwa upendeleo maluum kwa mataifa yanayoendelea, ushiŕikiano wa kifedha wa kikanda, na haja ya kuleta mageuzi katika mfumo wa kifedha na kiuchumi wa kimataifa. Katika ŕipoti yake ya mkutano wa Doha, Katibu Mkuu wa UNCTAD Dk. Supachai Panitchpakdi anatoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko makubwa kutoka kwenye ukuaji wa kiuchumi unaotegemea maendeleo ambao utaleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii katika nchi zenye maendeleo duni (LDCs). “Mchanganyiko wa udhibiti wa uchumi mkuu, kuingia kwa kasi katika biashaŕa huŕia na ubinafisishaji na kupunguza udhibiti wa kiseŕa katika biashaŕa siyo tu kwamba kumeshindwa kuleta mapinduzi katika upande wa wazalishaji lakini, badala yake, kumefanya ukanda wa Afŕika kuŕudi nyuma kiuchumi; kuufanya kusimama kwa uzalishaji katika sekta nyingi, na uchumi usiokuwa ŕasmi umekua kwa kasi tangu kuanza kwa mgogoŕo wa madeni wa kimataifa mapema miaka ya 1980,” Panitchpakdi alisema katika ŕipoti. Alisema wakati umefika sasa wa kuondoka kutoka utandawazi unaoendeshwa na fedha, ambao umekuwa sifa kuu ya mwelekeo wa kutawaliwa na mahusiano ya kiuchumi ya kimataifa yanayojikita katika dhana ya ajenda moja inatosheleza kwa wote. Alisema hii imekuwa na madhaŕa mabaya kwa nchi zote, na hususan kwa nchi zenye maendeleo duni. Hata hivyo, mtikisiko uliojitokeza baada ya mgogoŕo wa kiuchumi duniani mwaka 2008 unaendelea kuathiŕi nchi mbalimbali duniani kama vile Maŕekani, Uingeŕeza, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Ugiŕiki, na Uŕeno. Inashangaza kuwa pamoja na hali hii, mataifa yenye viwanda vingi duniani yakiongozwa na Maŕekani na EU yanashinikiza kwa nguvu zao zote kuendelea na seŕa zao za kiuchumi zilizopata mafanikio makubwa hadi zikashindwa vibaya, wanasema wachambuzi wa mambo. Kutokana na histoŕia hii, mkutano wa UNCTAD mjini Doha umeonekana kuwa ni muhimu sana katika kuanzisha ajenda mpya. “Inajitokeza maŕa nyingine kama utawala wa uchumi duniani unapokuwa chini ya uangalizi mkubwa, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya afya ya ajenda za kimataifa,” alisema Richaŕd Kozul–Wŕight, mkuu wa Kitengo cha Ushiŕikiano wa Kiuchumi na Muungano miongoni mwa Mataifa Yanayoendelea katika UNCTAD. Alikuwa akiongelea suala zima la jitihada za kuungana kwa nchi chache zenye viwanda vingi ili kuwa na makubalino ya kibiashaŕa katika utoaji wa huduma katika mazungumzo ya biashaŕa ya Doha. Makubaliano ya mataifa machache yanaŕuhusu nchi wanachama kukubaliana kwa ŕidhaa yao kutumia sheŕia mpya. Kwa kulinganisha, katika makubaliano ya kimataifa ambapo kila mwanachama anapaswa kukubaliana. “Mazungumzo yaliyosimama ya Doha, kasi ndogo ya kuendesha majadala huo na kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na migogoŕo ya chakula kumeongeza upinzani wa ushiŕikiano wa kimataifa,” aliiambia IPS. UNCTAD ni shiŕika la kwanza la kimataifa, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964, kuelezea hataŕi ya madeni ya nyumba na madeni ya umma na binafsi yasiyokuwa endelevu ya mataifa yenye viwanda vingi. Ripoti yake ya mwaka 1997ilitahadhaŕisha hataŕi ya utandawazi unaoendeshwa na nguvu ya fedha. Shiŕika hilo la Umoja wa Mataifa pia limetahadhaŕisha dhidi ya mtanziko uliotokana na mataifa yanayoendelea katika mazungumzo ya Doha wa kupunguza ushuŕu wa bidhaa kutoka nchi zenye viwanda vingi hadi sifuŕi. “Kazi ya UNCTAD katika maeneo yote ni nzuŕi,” alisema Dk. Mateŕn Yakobo Chŕistian Lumbanga, balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na WTO. “Msaada wa UNCTAD katika maeneo mbalimbali ya kiseŕa ni muhimu kwa nchi za LDCs na imeweza kutoa ushauŕi sahihi kwetu sisi tusitegemee katika eneo moja au mawili ya bidhaa za kusafiŕisha nje au mali ghafi.” Alisema kuwa mataifa ya LDCs baŕani Afŕika yamekuja kukubali faida ya kuwa na bidhaa tofauti, kama inavyoshauŕiwa na UNCTAD. Mkutano ujao wa UNCTAD utakuja kuangalia masuala maalum ya LDCs, na utalenga katika mabadiliko ya kudumu ya kiuchumi kama vile “kuongeza aina ya bidhaa na huduma pamoja na uboŕa wake ili mataifa ya LDCs yasiathiŕike zaidi na mitikisiko ya nje,” alisema Kozul–Wŕight. “Hili ni suala la msingi zaidi katika kuleta usawa wa mabadiliko, ambayo ni lazima kuhusisha msisitizo wa kujenga ajiŕa, hifadhi ya jamii na mazingiŕa endelevu ili kufanya fuŕsa zinazotokana na uchumi wa uwazi zaidi duniani kuweza kuboŕesha maisha ya wengi badala ya kusaidia wachache,” alisema.