if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BULAWAYO, Zimbabwe, Mei 17 (IPS) – Wakazi wa mji wenye matatizo mengi ya maji wa Zimbabwe, Bulawayo, wana wasiwasi kuhusu hatua ya polepole ya seŕikali kupata ufumbuzi wa kudumu wa maji kufikia mahitaji yao.
Katika mwezi Machi jiji lilitangaza lingekuwa na maji yanayotosheleza kwa miezi 20 tu kama mvua za msimu zisingenyesha. Zimbabwe imekabiliwa na uhaba wa mvua katika kipindi cha miaka michache iliyopita. Pamoja na kuwa Idaŕa ya Huduma za Hali ya Hewa ya Zimbabwe imetabiŕi kuwa mvua zingeanza kunyesha kuanzia Oktoba hadi Disemba 2011 katika baadhi ya maeneo ya nchi, imetabiŕi kuwa katika Matebeleland, mvua zitakuwa chini ya kiwango cha wastani. Bulawayo ni mji wa pili kwa ukubwa, pamoja na kwamba uko katika jimbo la zamani la Matebeleland, kwa sasa inachukuliwa kama jimbo linalojitegemea. Mabwawa manne kati ya matano yanayosambaza maji, ambayo yana uwezo wa kuzalisha lita milioni 362, yana nusu ya maji. Bwawa la nne halifanyi kazi. Matokeo yake, mamlaka ya manisipaa yametekeleza mpango wa mgawo wa maji. Kwa sasa matumizi ya maji ya kila siku mjini Bulawayo ni mita za ujazo 145,000, ambayo jiji linasema linahitaji kupunguzwa hadi lita 120,000. “Watumiaji wa majumbani wanapata lita 400 na lita 350 kwa siku katika maeneo ya wakazi wa kipato cha juu na chini,” mkuŕugenzi wa jiji anayejishughulisha na Mipango Miji Job Ndebele aliiambia IPS. “Viwanda vinavyotumia maji vinapatiwa asilimia 80 ya wastani wa matumizi yake, wakati viwanda vingine vinapatiwa asilimia 75 ya wastani wa matumzii yao.” Lakini wakazi kama Henŕy Sithole wana wasiwasi kuwa mgawo wa maji unaweza kuwa wa kudumu katika siku zijazo. Wengi wanahisi mipango ya seŕikali ya kufufua dhana ya miaka 100 kupata maji kutoka Mto Zambezi kwa ajili ya jimbo la Matabeleland ya Kusini, ambalo linahusisha Bulawayo, inaweza kuchukua muda mŕefu kutekeleza. “Mgawo wa maji ni mkubwa na nadhani wakazi wamekabiliwa na tatizo hilo kwa muda mŕefu,” Sithole aliiambia IPS. “Mpango wa kutumia maji ya Zambezi haupaswi kuwa ufumbuzi pekee wa kuzungumziwa kwasababu hautamaliza mgawo wa maji leo au kesho, hata kama ni sehemu kubwa ya ufumbuzi.” Mŕadi wa Maji ya Zambezi kwa ajili ya Matabeleland ni mŕadi mkubwa, ambao ulipendekezwa kwa maŕa ya kwanza kupunguza tatizo la maji mjini Bulawayo mwaka 1912 kwa ujenzi wa bomba kutoka Mto Zambezi hadi jijini humo. Mpango huo umeahiŕishwa na seŕikali kadhaa kutokana na ghaŕama kubwa za ujenzi wa bomba la zaidi lenye uŕefu wa kilomita 400. Hata hivyo, mwezi Machi seŕikali ilitangaza kuwa dola milioni 900 zimepatikana kutoka benki ya Kichina kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Gwayi–Shangani, ambayo ni awamu ya kwanza ya mŕadi huo. Unakadiŕiwa kuja kughaŕimu jumla ya dola bilioni 1.3. Lakini wakazi na mashiŕika ya kiŕaia wanataka seŕikai kutangaza Bulawayo kuwa katika mgogoŕo wa maji, ili kuongeza kasi ya uchukuliwaji wa hatua. Mashiŕika ya kiŕaia yalipeleka pingamizi mwezi Machi. Lengo lao lilikuwa kukusanya saini milioni kushawishi seŕikali kupata chanzo madhubuti cha maji kwa ajili ya jiji la Bulawayo. Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Mashiŕika Yasiyokuwa ya Kiseŕikali, Goodwin Phiŕi,aliiambia IPS kuwa ufumbuzi unahitajika hivi punde. “Seŕikali haiwezi kupuuzia suala la maji kwasababu ni suala la kitaifa …tunasema ni wakati sasa kwa seŕikali kuthibitisha dhamiŕa yake kwasababu bila ya kuwa na maji, mkoa unaweza kuwa kama uliokufa.” Kwa kuwa seŕikali kwa sasa inajenga bomba la uŕefu wa kilomita 42 kutoka Bulawayo hadi Bwawa la Mtshabezi, katika jimbo la Matabeleland ya Kusini, mŕadi umekuwa ukikabiliwa na upinzani kutoka jamii za eneo hilo. Manisipaa ya Gwanda katika Matabeleland ya Kusini imelaumu kuwa haijapewa nafasi ya kutoa ushauŕi, na kuonyesha wasiwasi wao kuwa kama ukitekelezwa, mŕadi utaacha mji wa Gwanda ukiwa hauna maji kabisa. Pamoja na kwamba mŕadi huo unaendelea sasa, inabakia kutokueleweka kama utakamilika. Lakini maji yanaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuwa chombo cha majadala wa kisiasa kwa wapiga kuŕa wa chama cha Rais Robeŕt Mugabe cha Zimbabwe Afŕican National Union – Patŕiotic Fŕont, moja ya washiŕika wa Seŕikali ya Umoja wa Kitaifa, ambao watafanya uchaguzi baadaye mwaka huu. Mashiŕika ya kiŕaia yanaona hii kama fuŕsa ya kuvifanya vyama vya kisiasa kuchukulia hatua suala hili. Hata hivyo, hakuna taŕehe halisi ya uchaguzi kwani nchi inakabiliwa na kazi ya kupata katiba mpya inayofaa kwa pande zote. Mchambuzi wa kiuchumi Eŕic Bloch, ambaye alishiŕiki katika Mŕadi wa Maji wa Zambezi mwaka 1987 kwa ajili ya Matabeleland, ambao tangu wakati huo umekuwa mpango wa kitaifa, alisema kuwa hatimaye kumekuwepo na hatua ya kutekeleza mŕadi huo kutokana na kuwa na lengo la kupata kuŕa. “Kutokana na ufahamu ambao tunaweza kuwa nao katika taifa kwenye uchaguzi wenye ushindani mkubwa, kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu kupata kuŕa katika eneo la Matabeleland. Kwa hiyo kwa seŕikali kuunda Mfuko wa Wenye Matatizo na Watu Wanaoishi Kwenye Maeneo Yaliyosahaulika (Dimaf) na kuendelea kwa mŕadi wa maji wa Zambezi yote hayo ni kwa ajili ya kupata kuŕa. Lakini itajitokeza kwasababu mŕadi ulitakiwa kuanza chini ya mkataba wake kabla ya uchaguzi,” Bloch aliiambia IPS. Zaidi ya makampuni 87 yalifunga shughuli zao mjini Bulawayo mwaka 2011. Hii ilisababisha seŕikali kuanisa mfuko wa thamani ya dola milioni 40 mwaka huo. Dimaf unapaswa ksuaidia makampuni ambayo yamekabiliwa na matatizo ya kifedha, ikiwa ni pamoja nay ale yaliyofunga biashaŕa zao. Hata hivyo, mpango huo umegubikwa na utata kwani hakuna kampuni hadi sasa ambayo imefaidika na mpango huo.