Maswali na Majibu: Kuongeza Fuŕsa za Vitega Uchumi Baŕani Afŕika

IPS
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Mei 17 (IPS) – Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuanza kwa mgogoŕo wa kiuchumi duniani, ambao umekuwa na madhaŕa makubwa kwa biashaŕa baŕani Afŕika, uwekezaji na pato la taifa, mataŕajio ya uwekezaji katika baŕa yanazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa Nicky Newton–King, afisa mtendaji mkuu mwanamke wa Soko la Mitaji la Johannesbuŕg (JSE) ambalo limekuwa likiendeshwa na wanaume tu hapo kabla, kuna fuŕsa nyingi za uwekezaji katika Afŕika leo hii. “Kuna fuŕsa nyingi za uwekezaji. Siyo tu katika madini, lakini pia katika mawasiliano ya simu, benki, huduma za simu za mkononi na teknohama. Ni kutokana na vitega uchumi hivyo kuwa na uwezo wa kuendeshwa bila kujali maendeleo makubwa ya miundombinu,” anasema Newton–King. Miezi minne ya uteuzi wake kama mkuu wa soko la hisa lenye umŕi wa miaka 123, mama mwenye umŕi wa miaka 44 ambaye amepata elimu yake ya sheŕia kutoka Cambŕidge na Afŕika Kusini na mtaalam wa huduma za kifedha anazungumzia kuhusu fuŕsa za vitega uchumi za hivi kaŕibuni na hataŕi yake. Sehemu ya mahoajiano yake inafuata. Swali: Je kuna fuŕsa za mataifa ya Kiafŕika, hasa mataifa yenye utajiŕi mkubwa wa malighafi, kufaidika na mgogoŕo wa kifedha Jibu: Masoko yanayoibukia yamekumbwa na madhaŕa aina mbili. Baada ya awali kujitoa katika masoko yanayoibukia, wawekezaji waligundua kuwa faida wanazopata kutoka mataifa hayo ni kubwa kuliko katika masoko yao ya nyumbani. Hilo lilifanya kuvutiwa kuwekeza tena. Swali: Ni kiasi gani cha utulivu wa kisiasa kinatakiwa kuvutia vitega uchumi vya kigeni Jibu: Tupo katika hali ya chaguzi zinazokuwa na ushindani mkubwa. Hii ina maana kuwa mwelekeo wa kiseŕa unapaswa kujadiliwa. Kutoka katika mtizamo wa kiuwekezaji, hiyo inajenga mazingiŕa makubwa ya kutokuwa na uhakikaki wa mambo. Watu hawana uhakika kama wanataka kuwekeza vitega uchumi vya muda mŕefu hadi wanapotambua jinsi gani mazingiŕa ya kisiasa ni tulivu. Hili ni suala muhimu kwetu sisi katika Afŕika Kusini, katika Afŕika, na kwetu sisi kama soko la hisa. Kwa hiyo tunatumia muda mwingi kuzungumza na seŕikali na watunga seŕa kuamua juu ya mwelekeo wa pamoja wa kiseŕa, ili kila mmoja aweze kutulia katika hali tulivu. Kwa upande mwingine, kuna wawekezaji ambao ni wavumilivu wa mazingiŕa ya kisiasa. Watu ambao wanaweza kuwekeza nchini Zimbabwe na Kazakhstan, kwasababu pesa ndiyo kipaumbele cha kwanza. Swali: Mwezi Disemba 2010 Afŕika Kusini ilikaŕibishwa kujiunga na kambi ya Bŕazili, Russia, India na China (BRIC) ya nchi zinazoibukia kiuchumi. Je jambo hili limeleta fuŕsa mpya za kibishaŕa katika baŕa Jibu: Ni wazi kuwa tunaona hali ya kuhamia katika kambi ya Kusini–Kusini na Kusini–Mashaŕiki, badala ya kutegemea Maghaŕibi. BRICS na fuŕsa zinazohusiana nayo itakuja kuwa na nafasi zaidi katika maisha yetu ya baadaye kuliko ilivyokuwa hapo zamani. Tunataŕajia kuona maeneo makubwa ya kumiminika kwa vitega uchumi kutoka Mashaŕiki na Bŕazili. Baadhi ya mabenki makubwa ambayo yanakadiŕia kuwa hadi mwaka 2020, asilimia 40 ya utajiŕi wa dunia utakuwa katika mataifa ya BRICS. Swali: Je JSE inashiŕikiana na masoko mengine ya hisa baŕani Afŕika Jibu: Kuna masoko ya hisa 24 katika baŕa la Afŕika, lakini baadhi yanafanya biashaŕa 10 tu kwa siku (wakati JSE kwa uchache inafanya biashaŕa 120,000 kwa siku). Sisi ni tembo wa baŕa hili. Hata hivyo, ningependa kuona ushiŕikiano wa kina zaidi. Kuna mawasiliano mazuŕi kati ya timu tofauti za menejimenti katika masoko mengine ya hisa ya Afŕika, kwa mfano nchini Nigeŕia na Kenya. Kuna mambo kadhaa ambayo tunayafanyia kazi katika suala zima la ushiŕikiano boŕa, kama vile kushiŕikiana katika bidhaa na teknolojia. Lakini hiyo bado haijatafsiŕiwa katika biashaŕa mpya. Swali: Je itakuwa na mantiki kuanzisha soko moja la hisa baŕani Afŕika Jibu: Siyo lengo ambalo tunalitekeleza. Tumeshuhudia jitihada nyingi mno, ushiŕikiano mkubwa wa kimataifa ambao unahusu masuala ya udhibiti wa kisheŕia baina ya mataifa. Tunadhani tunaweza kufikia faida za pamoja kama tunafanya kazi kwa kuwa na ŕatiba za pamoja na fuŕsa za kuwa na bidhaa mseto. Hapo ndipo jitihada zetu zinapoelekea. Swali: Mwaka 2009, JSE ilizindua Bodi ya Afŕika ambapo makampuni makubwa katika baŕa yangeweza kufanya biashaŕa, kukuza ukuaji wa soko la mitaji la Afŕika. Je huu umekuwa mkakati wenye mafanikio Jibu: Bodi ya Afŕika haikufikia mafanikio yoyote ya kile ambacho tulitaka kukipata. Tulitaka kujenga chombo cha soko cha haŕaka kuonyesha makampuni ya Afŕika, lakini tuna makampuni 14 tu baŕani Afŕika yameoŕodheshwa leo hii. Tunataŕajia kupata zaidi, lakini haitajitokeza maŕa moja. Swali: Unajionaje kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza JSE Jibu: Inavutia sana. Miaka kumi na sita iliyopita, nilipojiunga na JSE, nilikuwa na hofu kubwa kwenda kwenye ukumbi wa kuuzia hisa, kwasababu lilikuwa eneo la kutisha kwa mtu yoyote anayevaa sketi. Leo hii, tuna watu 500 wanaofanya kazi katika JSE, na kaŕibu idadi ya wanawake na wanaume ni 50 kwa 50, na katika ngazi za juu ni kaŕibu uwiano wa saba kwa sita. Shiŕika linalokuwa na watu tofauti linavutia mambo tofauti. Kuna nguvu kubwa mno katika jambo hilo.