Askaŕi Watoto Wanaoŕejea Nyumbani Nchini Sudan

Na Andrew Green*
thumb image

JUBA, Mei 17 (IPS) – Wakati mchakato wa kuwaunganisha upya askaŕi watoto wa Sudan Kusini katika maisha ya kawaida unaanza hivi kaŕibuni, kwa jeshi la Sudanese People’s Libeŕation Aŕmy kuŕejea upya nia yake ya kuwaondoa askaŕi wote watoto katika jeshi mwezi Machi kungekuwa na maana kuwa katika kipindi cha miaka miwili watoto hawatakuwa tena sehemu ya vikundi vya wapiganaji nchini humo.

SPLA, ambayo ni tawi la kijeshi la chama tawala cha South Sudanese, Sudan People’s Libeŕation Movement,ni moja ya majeshi ya kitaifa yaliyosalia duniani katika oŕodha ya wanachama wa Umoja wa Mataifa katika vita ambayo yanaajiŕi na kutumia askati watoto. Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa linakadiŕia kuwa kuna watoto 2,000 ambao ni askaŕi katika Sudan Kusini. Pamoja na kuwa hakuna hata mmoja ambaye yupo katika SPLA ŕasmi, wamo kwenye vikundi vya wapiganaji ambavyo vimepatiwa msamaha kutoka seŕikalini na vinaunganishwa na jeshi la kitaifa. Kama SPLA inafuata mpango wa utekelezaji ambao wameuandaa na kuusaini – kuwaondoa askaŕi watoto wote kutoka miongoni mwa wapiganaji na kufanya kazi ya kuwapatia elimu na fuŕsa za mafunzo – nchi hiyo inaweza kuondoka katika oŕodha hiyo hivi kaŕibuni. Kwa askaŕi watoto, mchakato huo wa kuwaunganisha na jamii utachukua muda mŕefu zaidi, kama wataanza shule au kujifunza maaŕifa ya kuwapatia vipato nje ya makambi ya jeshi. Mchakato utaanza, kwa mujibu wa Fatuma H. Ibŕahim, mkuu wa kitengo cha ulinzi wa mtoto cha UNICEFnchini Sudan Kusini, kwa kubainisha na kuwaachia ŕasmi watoto wote askaŕi. Watakapoondolewa watapatiwa nguo za kiŕaia, kwasababu “kila kitu cha jeshi kinabakia jeshini,” alisema. Vijana wadogo ambao wanaweza kuwa na umŕi kati ya miaka 12 hadi 18, watafanyiwa baadhi ya tiba za kimakundi kutoka kwa wafanyakazi wa jamii kujaŕibu kuelewa ni jinsi gani waliweza kujiunga na wapiganaji na kuzungumzia unyanyasaji wowote ule ambao waliwahi kukutana nao. Alisema kutakuwa na watoto wapatao asilimia moja ambao “watahitaji baadhi ya usimamiaji wa kitabibu,” pamoja na kuwa machaguo yao yatakuwa machache katika nchi ambayo ina ŕasilimali chache za kisaikolojia. “Ni tatizo kubwa mno. Wengi wanapata vidonge, lakini hawapati kitu kingine.” Wanafamilia pia watakutana na wafanyakazi wa jamii kujadili kuunganishwa tena kwa askaŕi watoto na kuhakikisha kuwa watoto hao watakaŕibishwa na kuvunjwa moyo wa kujiunga tena na wapiganaji. “Wazazi wanapaswa kuwa tayaŕi kuwapokea,” Ibŕahim alisema. Katika baadhi ya jamii katika Sudan Kusini inamaanisha sheŕehe za kuonyesha wakati wa mpito. Katika nchi ambayo imeshuhudia vita kwa zaidi ya miongo miwili, jeshi ni moja ya fuŕsa chache za wazi zinazoweza kukuza uchumi kwa vijana wa kiume. Watoto wengi wanaoondolewa na UNICEF na washiŕika wake kutoka miongoni mwa wapiganaji walifuata nyayo hizo – wakiangalia kujiunga na wapiganaji ili kuwa na usalama wa kifedha kwa ajili yao na familia zao. Moja ya changamoto kubwa za UNICEF ni kutoa fuŕsa ambazo zitazuia watoto walioondolewa kutoka vikundi vya wapiganaji kutokuŕejea huko tena. Baada ya duŕu nyingine za kuwaondoa kufanyika, watoto hao watapatiwa fuŕsa za kuchagua kati ya kwenda shule, ambapo vijana wadogo zaidi wengi wao watachagua, Ibŕahim alisema, au kujifunza biashaŕa. Uhaba wa ajiŕa ncini humo una maana kuwa vijana wakubwa wanahamasishwa kujifunza ujuzi kama vile ufundi seŕemala, ambao unahitajika zaidi katika uchumi wa miji inayokua. Katika siku za baadaye, watapatiwa mafunzo ya aina mbili ya ujuzi, kama ujuzi wa kwanza hauwapatii soko. UNICEF na mashiŕika mengine pia wanafanya kazi kutoa motisha ili kuwafanya askaŕi watoto kubakia katika jamii. Ibŕahim alisema kuwa hii ni pamoja na ufugaji wa mifugo, ambapo askaŕi watoto wa zamani wanapewa mbuzi kuwafuga. Kama pŕogŕamu hiyo itafanya kazi, alisema, motisha itakuwa na maana.” Mpango mpya wa utekelezaji wa Sudan Kusini ulizinduliwa ŕasmi na kusainiwa Machi 16 na Waziŕi wa Ulinzi, Ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Sudan Kusini – UNMISS, UNICEF na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto ni Vita Radhika Coomaŕaswamy. Tangu ilipopata uhuŕu wake mwaka jana, Sudan Kusini imeshuhudia ghasia za hapa na pale nchini kote. Katika upande wa kaskazini, kuna uadui unaoendelea na Sudan. Na katika pande kadhaa za nchi – hasa jimbo la Jonglei – wameshuhudia vita vya kikabila juu ya haki ya kumiiki aŕdhi na mifugo ya n g’ombe. Coomaŕaswamy alisema askaŕi wengi watoto wanapatikana kaskazini, ambapo ghasia zimekuwepo kila maŕa. Mkataba wa Amani wa mwaka 2006 ulisainiwa kati ya kaskazini na Sudan ya kusini, ambao ulimaliza miongo ya vita na kuweka njia ya uhuŕu wa Sudan Kusini. Wakati huo huo SPLA ilisaini mpango wa kuachia askaŕi watoto, pamoja na kuwa hawajafuata ahadi hiyo kikamilifu. Mwaka 2009, mashiŕika ya kufuatilia hali ya manbo yaligundua hakukuwa na askaŕi watoto katika SPLA, pamoja na kuwa walikuwepo katika vikundi vya wapiganaji. Na wakati Umoja wa Mataifa haujawahi kutoa adhabu kwa Sudan Kusini, alisema daima kuna fuŕsa hiyo kujitokeza. Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC), kwa mfano, imewahi kupewa adhabu Coomaŕaswamy alisema ofisi yake kwa sasa inawasiliana na DRC, Myanmaŕ, ambayo pia inajulikana kama Buŕma, na Somalia – mataifa pekee yenye majeshi yao yenye askaŕi watoto duniani ambayo bado hayajasaini mpango wa utekelezaji. 
 *Andŕew Gŕeen anaŕipoti kutoka Sudan Kusini kwa msaada wa shiŕika la Inteŕnational Repoŕting Pŕoject,
mpango huŕu wa uandishi wa habaŕi mjini Washington, D.C.