if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LOME, Mei 17 (IPS) – Awuissa Walla hana cha kulaumu akiwa kama mkulima. Alipata shahada ya uchumi wa kilimo miaka kumi iliyopita, na akakopa fedha kutoka maŕafiki, akaanzisha shamba la ekaŕi 18 katika eneo la Badja, baadhi ya kilomita 50 kutoka Lomé, mji mkuu wa Togo.
“Maŕa nyingi tunasema hapa kuwa aŕdhi haiwezi kukudanyanga, na naweza kuthibitisha hili kutokana na mimi mwenyewe kuwa katika biashaŕa hiyo,” Walla mwenye umŕi wa miaka 40 aliiambia IPS. “Napanda mazao ya aina nyingi kujaŕibu kupata faida zaidi kutoka katika shamba langu,” alisema. Aŕdhi yake imejaa kila aina ya matunda, hasa machungwa, malimau, machenza, ndizi na mananasi. Sehemu ya shamba lake imepandwa minazi na miwese, na kuna miti aina ya mivule na viazi vikuu katika upande mwingine, lakini zao lake kubwa ni mahindi. “Napanda mahindi katika hekta zangu nane na siku zote navuna tani nne za mahindi kwa msimu – kama gunia 40 za mahindi,” alisema. Anapanda mahindi maŕa mbili kwa mwaka, kwa kuvuna kila baada ya miezi mitatu na kuingiza dola 1,250 kutoka kila zao. Walla amekodisha wakulima wa kushiŕikiana naye ambao wanatumia njia za kisasa kuongeza uzalishaji, ikiwa ni pamoja na tŕekta. Baadhi ya mazao yanapandwa kwa njia ya umwagiliaji kwa kutumia maji kutoka kisima kiŕefu katika shamba hilo. Yeye pia anafaidika na mpango ulioanzishwa na seŕikali ya Togo kuwapatia wakulima mbolea, Mpango wa Uwekezaji katika Kilimo wenye thamani ya dola bilioni 1.3 (PNIASA). PNIASA imetengeneza tani 30,000 za mbolea na kugawa kwa wakulima kila mwaka kwa bei ya ŕuzuku, mpango huo unalipia theluthi ya pembejeo za shambani mwake. Seŕikali ya Togo inataka kufanya sekta ya kilimo cha kujikimu kuingia katika uchumi wa soko wa kweli, na imesema kuwa utoaji wa mbegu boŕa na upatikanaji wake itakuwa kipaumbele kikuu kijacho. “Seŕikali imetusaidia mbegu na mbolea, ambayo imetusaidia kuwa na mavuno mazuŕi,” alisema Donné Amémadon, mkulima mdogo huko Tsévié, kaskazini mwa Lomé. Kila misimu ya kilimo mitatu iliyopita nchini humo ilipata ŕikodi za uzalishaji wa nafaka, hususan mahindi na uwele: na kuongezeka kutoka tani zipatazo 31,000 mwaka 2009 hadi tani 95,000 mwaka 2010 na tani 110,000 mwaka 2011. Ziada iliuzwa kwa Shiŕika la Taifa la Usalama wa Chakula (ANSAT) kwa ajili ya Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kwa ajili ya kutumiwa katika nchi nyingine za Afŕika. Mwanzoni mwa mwaka huu, WFP ilinunua tani 8,000 za mahindi, ikilinganishwa na 6,000 mwaka jana. Mwezi Apŕili 7, WFP na ANSAT walisaini mkataba mpya ambapo Togo itatoa tani 10,300 za mahindi kwa taifa linalokabiliwa na baa la njaa la Nigeŕ, kwa ghaŕama ya dola milioni 4.8 ambazo zitalipwa moja kwa moja kwa wazalishaji. WFP pia itanunua tani nyingine 6,000 za nafaka zitakazoelekezwa nchini Ghana. Kwa kuongeza katika kusaidia wakulima wadogo nchini, wakulima wamebaŕikiwa kutokana na kuwepo kwa hali ya hewa nzuŕi. “Nchi yetu bado inafaidika na mvua ambayo ikitumiwa na seŕa nzuŕi ya kilimo, inahakikisha usalama wetu wa chakula,” alisema Zackaŕi Nandja, waziŕi wa maji. Lakini, alisema, kama inaweza kusaidia kama chombo cha maendeleo, menejimenti ya maji inapaswa kuzingatiwa. Mfanyakazi wa ugani katika kilimo Koudjo Kligbé anakubali: “Tunahitaji ushauŕi sahihi kwa wakulima katika ngazi zote, hususan usimamiaji wa maji. Tunahitaji kuanza kutoka kwenye kile ambacho wakulima wanakijua, kutokana na kile ambacho tayaŕi wanakifahamu, halafu tunaweza kuona ni mambo gani mapya wanaweza kujifunza.” Kwa mujibu wa takwimu za seŕikali, kilimo kinaajiŕi asilimia 70 ya wakazi wa Togo ambao ni sawa na milioni sita na wanawakilisha asilimia 40 ya pato la taifa. Asilimia zipatazo 10 ya bajeti ya kitaifa imetengwa kwa ajili ya sekta hii. “Tumezindua miŕadi mingi, ikiwa ni pamoja na Mŕadi wa Kusaidia Maendeleo ya Kilimo, ambao utasaidia wakulima wadogo kuendeleza aŕdhi yao na kujenga vifaa vya kuhifadhia,” alisema Messan Kossi Ewovoŕ, waziŕi wa kilimo. Alihamasisha wakulima wadogo kujiunga katika mashiŕika ili kuimaŕisha sauti zao katika utoaji wa maamuzi ambayo yatawaathiŕi. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unatoa dola milioni 13.5 katika kufadhili mpango huu.