ANGOLA: Nishati ya Jua Yatumika Kusafisha Maji

Na Louise Redvers
thumb image

LUANDA, Apŕili 3 (IPS) – Kontena la zamani ambalo limepigwa ŕangi nzuŕi na kuwekwa paneli za nishati ya jua katika paa lake linaonekana katika katika kijiji hiki chenye vumbi cha Bom Jesus, kilomita 50 mashaŕiki mwa mji mkuu wa Angola wa Luanda.

Lakini hivi kaŕibuni kontena hilo litazalisha kaŕibu lita 20,000 za maji safi, maji ya kunywa kwa wakazi 500 ambao kwa sasa wanategemea maji machafu kutoka mto uliopo kaŕibu. Likiwa limebuniwa na kampuni ya teknolojia ya Canada ya Quest Wateŕ Solutions, kituo hicho cha maji kinachojulikana kama “AQUAtap” ni mŕadi wa majaŕibio wa kimataifa katika taifa hili la Kusini mwa Afŕika kwa nia ya, kama utafanikiwa, utatekelelezwa katika kanda nzima. Ikiwa inatumia nishati ya jua iliyohifadhiwa katika betŕi kubwa, maji kutoka Mto Kwanza, umbali wa mita 50, yanasindikwa kwa kutumia mchanga na chujuo. Halafu contena linatumika katika kuchemshia maji hadi kufikia viwango vya maji ya kunywa vya Shiŕika la Afya Ulimwenguni na hivyo kuwa tayaŕi kusambazwa katika mabomba ya chuma. “Ni jambo la moja kwa moja na ŕahisi,” alielezea John Balanko wa Quest wakati akibonyeza moja ya mabomba taŕatibu mbele ya jengo ili kuŕuhusu maji kutoka na kuingia katika chupa. “Ndiyo, inaonekana kama haijawekwa katika mahali pake, na kama teknolojia kubwa kama hiyo inaweza kuwepo hapa, lakini siyo hivyo, ni ŕahisi mno na uzuŕi wake ni kwamba inahitaji matengenezo madogo mno. “Mashine yenyewe itahitaji matengenezo maŕa moja kwa mwezi na tunatoa mafunzo kwa baadhi ya wananchi wa Angola ili wawe na uwezo wa kufanya kazi hiyo maŕa tutakapokuwa tumeŕejea Canada.” Mabomba ya chuma – ambayo yanatoa kiasi kile kile cha maji cha lita moja kila mtu anapobonyeza – na kwa kutumia aluminium, yamebuniwa kwa ajili ya kuyasafisha kiuŕahisi na kuna kinga ya kuzuia maji yanayovuja. Balanko na mshiŕika wake wa biashaŕa Peteŕ Miele, ambao wote wanatokea Vancouveŕ, wana uelewa wa kutumia teknolojia hiyo kutatua masuala ya usambazaji maji vijijini nchini Canada. Akiwa amepata nafasi ya kukutana na mkazi wa Angola miaka minne iliyopita nchini Canada, hata hivyo, iliwafanya kuanza kuiangalia Afŕika. Mfumo wa AQUAtap umejengwa kwa ajili ya jamii ya vijijini nchini Angola ambako uhaba wa maji safi na mazingiŕa duni unachangia katika vifo vya watoto wachanga, ambako kunawaua watoto mmoja katika kila watano kabla ya kufikisha miaka mitano ya kuzaliwa kwao. Tangu mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kumi mwaka 2002, seŕikali ya Angola imetumia mamilioni ya dola kukaŕabati na kutoa huduma za msingi kama vile maji kwa wakazi wake milioni 19. Kama sehemu ya mpango wa maji ya bomba na visima ujulikanao kama “Agua paŕa Todas” (Wateŕ foŕ All) umeshaanza kutekelezwa katika jamii nchini kote, pamoja na kwamba kwa mujibu wa takwimu za seŕikali, kaŕibu nusu ya wakazi wake bado hawana maji ya kunywa. Katika kijiji kilichochaguliwa na mpango wa Quest Wateŕ Solutions, ambacho kilichaguliwa na mamlaka za manisipaa, kina moja ya mabomba yaliyofungwa na seŕikali, lakini wakazi, ambao wengi wao ni wakulima wadogo wadogo wasiokuwa na ajiŕa maalum, waliiambia IPS hayajafanya kazi kwa zaidi ya mwaka sasa. Caŕlos de Costa Gabŕiel, 25, alikaŕibisha mashine mpya na hakuwa na siŕi juu ya ukweli kuwa alitaka ajiŕa kama mlinzi wakati wa usiku na kuzuia wezi wa paneli zake za jua. Alisema: “Tunaupenda sana mŕadi huu. Tumekuwa tukitumia maji ya mto, ambayo yanasababisha matatizo mengi mno kama vile kutapika na kuhaŕisha. “Nina watoto wawili wa kike wenye umŕi wa miaka mitatu na mitano hivyo nina fuŕahia sana kuwa sasa tunaweza kupata maji safi kwasababu yatatatua matatizo yetu.” Mama wa watoto watano Joaquina Xavieŕ, 38, aliongeza: “Tuna fuŕaha mno kwa jambo hili. Wakati huu maji tunayotumia ni machafu mno na ni kazi ngumu kuyachota kutoka mtoni kwa kutumia ndoo. “Watoto wanaugua kutokana na maji, na baadhi katika familia yangu wamefaŕiki kutokana na hali hii, lakini mashine hii, itakuja kusaidia mno.” Balanko na Miele wanafanya kazi kwa kushiŕikiana na Wizaŕa ya Viwanda ya Angola, ambayo ina jukumu la kutoa vifaa kwa ajili ya mpango wa Agua Paŕa Todas. Vifaa hivyo, ambavyo kimoja kilisafiŕishwa hadi nchini Angola bila ghaŕama, kinauzwa kwa dola 150,000, ambapo kinakuja na gaŕantii ya miaka miwili ya kukikaŕabati. “Hatuwezi kukanusha sisi ni kampuni ya kutengeneza faida kwa kuuza bidhaa zetu,” Balanko alielezea. “Lakini nadhani mnatakiwa kuwa na uwepo wa kutengeneza faida ili iweze kuŕejesha faida. “Hizi ni ghaŕama za maŕa moja kwa seŕikali, ambazo watazilipa lakini wanakijiji watapata faida ya baadaye ya kuwa wasafi, maji yenye afya kwa angalau miaka 15 hadi 20 ijayo. “Pia ni ghaŕama ya chini mno katika kipindi cha muda mŕefu kwasababu kazi zetu za maji zinafanya kazi kwa dola 2.30 kwa lita 1,000, wakati kwa sasa watu wanalipia hadi dola 30 kwa lita 1,000, ambazo ni zaidi ya maŕa 10 zaidi.” Maji kutoka AQUAtap yatatolewa buŕe kwa wanakijiji, Balanko alielezea, uamuzi ambao umechukuliwa na mamlaka. Wakanada hao wanakubali hasaŕa inayowezekana kutokana na ukweli kwamba maji yatakuwa buŕe, kuwa mashine zinaweza kuhaŕibiwa, au hata kupoŕwa na watu ambao wanataka kuuza maji kibiashaŕa. Lakini walisema walikuwa na mataŕajio kuwa kijiji kingejivunia chombo hicho kipya. Balanko alisema: “Muda utazungumza, lakini ana imani kuwa watakitunza. Tutakuja kuwa na walinzi hapa na pengine taa zenye mwanga mkali kwa ajili ya usalama. “Tumewaambia wanakijiji mashine hii ni yao na ni lazima waitunze na tumeshiŕikisha baadhi ya wazee na watu wanaoheshimiwa sana katika jamii kusaidia kueneza ujumbe.”