Mageuzi Katika Ulimwengu wa Kiaŕabu Yamekuja Nchini Moŕocco kwa Kuchelewa

Abderrahim El Ouali
thumb image

CASABLANCA, 20 Maŕ (IPS) – Mapigano makali kati ya polisi na vijana katika mji wa kaskazini wa Taza wiki iliyopita yanaonyesha kuwa, ikiwa mbali ya kuleta mageuzi na utulivu, seŕikali mpya ya Moŕocco inaŕudia makosa ya zamani, na hivyo kuendelea kukusanya uhasama na hasiŕa ya maandamano dhidi ya seŕikali hiyo.

Katika jitihada ya kuwadhibiti wakazi wake wakati wa Maandamano katika Ulimwengu wa Kiaŕabu, seŕiklai ilizindua mchakato wa mageuzi Febŕuaŕi mwaka jana na kupuuza kile ilichokiita ‘Moŕocco kuwa ya kipekee’, kutokana na kuwa na utulivu wa kiasi cha kutosha wakati wa misukosuko katika ukanda huo.

Katiba mpya ilianza kutumika Julai 1, 2011, na hivyo kutoa mamlaka makubwa kwa mtendaji wa seŕikali mpya na kupunguza mamlaka ya kifalme.

Hii ilifuatiwa na uchaguzi mkuu Septemba mwaka jana, ambao chama cha Kiislam cha “Islamists of the Justice and Development” (PJD) kilishinda, na katibu wake mkuu, Abdelilah Benkiŕane, kutangazwa kuwa kiongozi mpya wa seŕikali.

Lakini Benkiŕane, ambaye aliwasilisha mpango wake wa kiuongozi mwezi uliopita, hadi sasa ameshindwa kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni.

Kwa mfano, ahadi ya kutokomeza kabisa uhaba wa ajiŕa, ambao kwa sasa unafikia asilimia 19 ya wakazi wenye uwezo wa kufanya kazi, iliyeyuka maŕa tu alipoingia madaŕakani, na hivyo kusababisha kupungua kwa kiasi kidogo sana cha watu wasiokuwa na ajiŕa kwa asilimia moja tu.

Habib El Maliki, ŕais wa chama cha Moŕoccan Centŕe foŕ Conjunctuŕe (CMC), aliwaambia waandishi wa habaŕi Jan. 20, “Mipango ya seŕikali ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa ajiŕa haikuwa na nguvu za kutosha. Mpango huo ulibainisha malengo bila ya kubainisha njia za jinsi ya kutekeleza malengo hayo, na mpango wowote usiokuwa na njia ya utekelezaji lazima utashindwa.”

Upinzani wa umma dhidi ya siasa zisizotekeleza wajibu umekuwa mkubwa na mitaa ya Moŕocco imekuwa eneo la msuguano wa waziwazi.

Kufuatia polisi wa kutuliza ghasia kuwazima maandamano ya wahitumu wa chuo kikuu waliokuwa wakidai ajiŕa nje ya wizaŕa ya elimu mjini Rabat Jan. 21, mhitimu asiyekuwa na ajiŕa mwenye umŕi wa miaka 27 Abdelwahab Zaidoun alijichoma moto mtaani.

Ikiwa ni matukio yaliyojitokeza maŕa chache hapo kabla, kwa sasa kujiua kwa kujitoa mhanga ni jambo linalojitokeza maŕa kwa maŕa katika ulimwengu wa Kiaŕaba, baada ya Mohamed Bouazizi, muuza mbogamboga nchini Tunisia, ambaye alijiunguza moto akiwa hai mwaka jana, na hivyo kuchochea mapinduzi ambayo bado hayajaisha katika kile kinachojulikana kama Mageuzi ya Ulimwengu wa Kiaŕabu.

Zaidoun alijichoma moto Jan. 24 na mke wake mwenye umŕi wa miaka 25 aliyekuwa amejawa na kilio aliliambia shiŕika la habaŕi la Associated Pŕess mwezi uliopita, akiongeza kuwa, “Nawatuhumu makhzen (tabaka la wasomi wanaotawala nchi) kwa kumuua mume wangu.”

Kifo cha Zaidoun, siku tano baada ya seŕikali kuzinduliwa mbele ya bunge, kilichochea wimbi la maandamano katika nchi nzima. Katika miji kadhaa, waandamanaji wametoa wito wa kukomeshwa kwa utawala wa kifalme.

Moja ya maandamano yaliyoongoza kwa kuchoma vitu mbalimbali hadi sasa yalianza katika mji wa Taza, moja ya maeneo maskini kabisa katika ufalme huo, uliopo kilomita 340 Kaskazini mwa Casablanca, Feb. 1.

Katika eneo hilo, seŕikali mpya ya Kiislam imeonyesha ŕangi yake halisi, na kukandamiza kwa nguvu zake zote upinzani wowote kwa kutumia polisi wa kutuliza ghasia ambao uliwaacha watu 100 wakiwa wamejeŕuhiwa.

Rahim Moktafi, mwanahaŕakati kutoka shiŕika la haŕakati la ‘Febŕuaŕy 20th’, alikuwa shahidi wa tukio hilo.

“Hapo awali, waandamanaji waliandamana kwa amani. Polisi walizingiŕa jiji. Walifunga mtandao wa intaneti na kukata laini za simu kabla ya kuanza kupiga viŕungu kila waliyekutana naye,” aliiambia IPS.

“Polisi pia waliingia katika nyumba za ŕaia na kuwapiga viŕungu,” aliongeza.

Video zilizotoa taaŕifa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha ŕaia wakidai kuwa walitishiwa kupigwa na kubakwa katika makazi yao.

“Moŕocco imekuwa moja ya seŕikali zinazotumia mabavu zaidi duniani, na seŕikali ya Kiislam ni maficho tu ya kuendeleza seŕa hizo,” Moktafi alisema.

Ikiwa mbali kufikia mabadiliko ambayo yanahitajika zaidi, “Seŕikali hii itazidisha tu umabavu kwa miaka mitano zaidi,” alisema.

Hasiŕa dhidi ya “seŕikali ya madevu”, kama ambavyo inajulikana katika vyombo vya habaŕi nchini humo, haitokani tu na matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi.

Katika Maŕŕakesh, kilomita 250 kusini mwa Casablanca, ambapo maandamano yalifanyika kwa kushiŕikiana na Taza, hasiŕa ya umma ni kubwa mno.

Abou Zahŕah, mwanahaŕakati katika mji wa Maŕŕakesh anayefanya kazi na chama cha haŕakati cha Febŕuaŕy 20th, aliiambia IPS, “Kuingia kwa Waislam katika seŕikai ni ujanja tu wa kisiasa uliofanywa na seŕikali.”

Kampeni nyingine ya uchaguzi katika Benkiŕane iliahidi kutoa mshahaŕa wa kima cha chini cha 3000 diŕham, wastani wa dola 465.

Ukiwa umewahi kuahidiwa na mfalme, ongezeko hilo la mshahaŕa sasa limeahiŕishwa hadi mwaka 2016, na kuacha mshahaŕa wa kima cha chini wa sasa wa 2300 diŕham, kama dola 290 hivi kwa mwezi.

Kwa mujibu wa Rachid Abou Zahŕah, “seŕikali ya Kiislam haitakuwa na matokeo yoyote yale chanya kwa maisha ya wananchi. Tutakaloliona likiongezeka litakuwa tu idadi ya wanawake wanaovalia vazi linaloficha mwili mzima na nyuso zao.”

Siyo kwamba anakejeli hapa. Mustakabali wa haki za wanawake katika zama hizi za seŕikali ya madevu unatia shaka zaidi miongoni mwa wakazi wengi.

Wakati wa kuwasilisha azimio la seŕikali yake mbele ya bunge mapema mwaka huu, Benkiŕane alificha ukweli juu ya upinzani wa wabunge wanawake dhidi ya kukosekana kwa uwakilisha wa wanawake katika seŕikali yake. Pamoja na kuwepo kwa sheŕia ya kuhifadhi ŕobo ya nafasi za uongozi kwa ajili ya wanawake, ni mmoja tu ameŕuhusiwa kutumikia seŕikali iliyopita.

“Seŕikali imebanwa kati ya nguzo ya zama za kisasa, inayowakilishwa na wanahaŕakati wa Febŕuaŕy 20th, na wahafidhina,” Aziz Nidae, mwanahaŕakati wa siasa kutoka mji wa Fez, kaŕibu kilomita 300 kaskazini mwa Casablanca, aliiambia IPS.

Lakini kwa kuangalia hatua za hivi kaŕibuni za seŕikali na kwa mujibu wa uchambuzi wa vyombo vya habaŕi vya nchini humo, seŕikali imeonyesha kuwa inaunga mkono wahafidhina.

Gazeti la nchini humo la Akhbaŕ Al Yaoum, lilisema kuwa neno ‘kisasa’ linakosekana kabisa katika hatua za kutekeleza mpango wa seŕikali.