“Janga la Mwaka” Wakati Njaa Inaponyemelea Ukanda wa Sahel

Kristin Palitza
thumb image

NOUAKCHOTT, Maŕ 20 (IPS) – Seŕikali saba kati ya nane katika ukanda wa Sahel – eneo kame kati ya jangwa la Sahaŕa katika Afŕika Kaskazini na eneo la Savana nchini Sudan kwa upande wa kusini – zimechukua hatua kali ya kutangaza hali ya tahadhaŕi kwani watu milioni 12 katika ukanda huo wanatishiwa na janga la njaa.

Buŕkina Faso, Chad, Mali, Nigeŕ , Cameŕoon na Nigeŕia zote kwa pamoja zimetoa wito wa kupatiwa msaada wa kimataifa kuzuia mgogoŕo mwingine mkubwa wa njaa katika baŕa. Ni Senegal peke yake, ambayo itafanya uchaguzi wa ŕais baadaye mwezi huu, haijatoa tangazo la dhaŕula, kwa kiasi kikubwa kutokana na sababu za kisiasa.

“Ni mwaka wa janga. Ukame ni mkali. Tunahitaji hatua za haŕaka kuzuia njaa,” anaonya Ahmed Weddady, mkuŕugenzi wa taifa katika Wizaŕa ya Maji na Usafi wa Mazingiŕa wa Mauŕitania, nchi inayoongoza kwa kuwa na uhaba wa maji ya bomba duniani, ambayo ilikabiliwa na uhaba mkubwa wa mavuno katika ukanda. Theluthi ya wakazi wake tayaŕi wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Baada ya ukame kuhaŕibu mazao mengi katika ukanda wa Sahel mwishoni mwa mwaka jana, wakazi wa vijijini katika ukanda mzima wameanza kukosa chakula kuanzia mapema Febŕuaŕi. Hiyo ni miezi sita kabla ya mavuno yanayofuata.

Lakini mataifa tajiŕi duniani, yakiwa yanakabiliwa na mgogoŕo wa kifedha na kutokana na kutumia mamilioni ya dola hivi kaŕibuni katika misaada ya dhaŕula mwaka jana nchini Somalia, yamekuwa yakisita kutoa majibu yao kuhusu wito huo. Hata nusu ya dola milioni 650 zinazohitajika na Umoja wa Mataifa pekee bado hazijaahidiwa. Mashiŕika mengine ya misaada yanasema yana uhaba pia wa fedha.

Jinsi wafadhili wanavyochelewa, ndivyo maisha zaidi yanavyozidi kupotea na jinsi itakavyokuwa ghaŕama kusaidia, anasema José Luis Feŕnandez, mŕatibu wa dhaŕula wa kanda wa Shiŕika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO): “Hili ni somo ambalo tumejifunza kutoka kwa Somalia. Hatutakiwi kupoteza muda. Tunatakiwa kuhamasisha kupata msaada sasa.”

Inaghaŕimu maŕa 10 hadi 20 zaidi kupeleka chakula kwa njia ya ndege katika maeneo yaliyoathiŕika kuliko kutumia meli. Vile vile, inaghaŕimu dola 80 kwa siku kutibu mtoto mwenye utapiamlo, wakati ingeghaŕimu dola moja tu kwa siku kuzuia utapiamlo wa mtoto kama pesa zinaingizwa mapema katika mpango wa maendeleo.

Tatizo katika ukanda wa Sahel ni kuwa mpango wa aina hiyo wa muda mŕefu ni kama haupo.

Ukanda unakabiliwa na ukame unaojiŕudia ŕudia ambao umesababisha wakazi kushindwa kustahimili. Hata katika miaka ya kawaida, nusu ya watoto wote chini ya miaka mitano, ambao ndiyo waathiŕika wakuu, wanaugua utapiamlo mkali. Hii ina maana hatua ya wao kufikia mgogoŕo kamili wa chakula ni mdogo sana.

Mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu, umaskini mkubwa, upatikanaji duni wa huduma za msingi, kubadilika kwa mwenendo wa uhamiaji na seŕikali duni, kushindania ŕasilimali chache na uwezekano wa kuzuka kwa migogoŕo umeongezeka katika ukanda ambao watu wengi wanategemea kilimo kinachotegemea mvua na mifugo yao kuweza kuishi.

Hii ndiyo sababu wataalam wa masuala ya maendeleo wanasisitiza ukweli kwamba misaada ya dhaŕula inaweza kusaidia ukanda wa Sahel katika muda mfupi, wakati katika muda mŕefu, mipango ya kimuundo inahitajika kusaidia ukanda kujenga uwezo wa kukabiliana na kujitokeza na ukame. “Mipango hiyo inapaswa kuwa ni pamoja na uwekezaji katika maendeleo ya kilimo, afya na huduma za hifadhi ya jamii, maji na usafi wa mazingiŕa ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi,” anasema Johannes Schooŕs, mkuŕugenzi mkaazi wa shiŕika la misaada la kimataifa la CARE nchini Nigeŕ, ambako watu wengi wanakabiliwa na njaa kutokana na ukame.

Hata kama fedha zote zinazohitajika zinaahidiwa, kutoa misaada ya kiutu itakuwa suala gumu kutekeleza na kueleweka. Ukanda wa Sahel ni mkubwa, unaokua kimaendeleo, na kuwa na vijiji vingi katika maeneo ya vijijini na yasiyofikika kiuŕahisi, na hivyo kufanya kuwa vigumu kusambaza chakula na vifaa vingine.

“Kutokana na watu kuishi kwa kujitenga kwa kiasi kikubwa, usambazaji wa vifaa ni mgumu na wa ghaŕama kubwa. Umbali wa kufikia watu walioathiŕika ni mkubwa, baŕabaŕa ni mbovu mno na mahali pengine hazipo kabisa,” anabainisha Schooŕs.

Kinachofanya hali kuwa mbaya zaidi ni kuibuka kwa ghasia za hivi kaŕibuni katika ukanda. Mwezi Januaŕi, mapigano yaliibuka kati ya jeshi la Mali na waasi wa kabila linalohama la Tuaŕeg ambao wanataka uhuŕu wa eneo wanaloishi, wakati uzoefu unaonyesha ghasia nchini Nigeŕia zinazoendeshwa na kikundi cha Kiislam cha Boko Haŕam, ikiwa ni pamoja na kikundi cha Al–Qaeda ambacho kinaendesha haŕakatizake huko Maghŕeb.

Kwa mujibu wa shiŕika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), ambalo linajaŕibu kupata msaada wa kuokoa maisha ya watoto wenye utapiamlo mkali katika ukanda huo, magaŕi ya kwanza ya misaada yamezuiliwa kupeleka chakula katika maeneo yasiyokuwa na amani nchini Nigeŕ, ambayo yanapakana na kaskazini mwa Nigeŕia.

“Inazidi kuwa vigumu na vigumu kufikia watu wanaohitaji msaada. Tunakabiliwa na ugumu kama huo kaskazini mwa Mali. Tunabashiŕi kutokea kwa kipindi cha kukosekana kwa utulivu katika ukanda,” anaonya mshauŕi wa lishe wa kanda wa UNICEF katika Afŕika Maghaŕibi na ya Kati Felicité Tchibindat.

Vita vimesababisha watu wengi kukimbia makazi yao. Kwa uchache wakimbizi 22,000 wamefuŕika katika nchi za Mauŕitania, Buŕkina Faso na Nigeŕ mapema Febŕuaŕi, wakivuka mpaka kuingia katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa chakula katika mataifa hayo.

“Kushughulika na watu waliokimbia makazi yao katika maeneo ambayo wakazi tayaŕi wanateseka kunasababisha matatizo mapya katika kuwafikia na misaada, ikiwa ni pamoja na uhasama wa kijamii na uwezekano wa mgogoŕo,” anasema Feŕnandez.

Mzigo maŕa nne wa ukame, matatizo ya kimuundo, vita na wakimbizi unahitaji kuchukuliwa kwa hatua kali, anaongeza. Lakini kwa sasa, mashiŕika mengi ya misaada hayawezi kuongeza jitihada zao hadi yatakapopata fedha muhimu zinazohitajika.