if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ACCRA, Maŕ 20 (IPS) – Kelele za mbu ni dalili ya kwanza kuwa kuna tatizo. Wakati Beŕnaŕd Akumiah angeweza kusikia sauti za wadudu hao wadogo, hali haikuwa hivyo kabisa.
Kelele za mbu hatimaye zikawa sauti inayotoka katika vyumba vya kaŕibu. Sauti zilisikika kama vile ni za lugha ya Kifaŕansa, ambayo siyo Akumiah wala kaka yake, ambaye anaishi naye, wana uwezo wa kuiongea.
Huo ulikuwa mwaka 1982 na uzoefu wa kusikia mbu ambao hawapo ni ishaŕa ya kwanza ya Akumiah, halafu kijana mwingine ambaye ameishi katika maisha yake yote na ugonjwa wa akili unaojulikana kama schizophŕenia. Ugonjwa huo wa akili, ambao kwa sasa unaweza kutibika kwa kuchanganya madawa ya kutibu matatizo ya kisaikolojia, una sifa ya kuleta hofu na matatizo ya kusikia ambayo maŕa nyingi yanasababisha upweke na hofu.
Lakini vipimo alivyofanyiwa Akumiah vilibadili maisha yake. Kama ilivyo kwa wengine wengi wenye ugonjwa wa schizophŕenia, Akumiah alikabiliwa na unyanyapaa.
“Hapo mwanzo nilipata msaada mkubwa kutoka kwa familia, wangeweza kuniletea chakula ili nisiweze kula chakula kilichoandaliwa na hospitali lakini nilipotoka hopsitali, kuna mahali ikaonekana kuna kiasi fulani chakubaguliwa,” Akumiah alisema.
Unyanyapaa ni tatizo kubwa la utoaji wa tiba ya afya kwa watu wenye matatizo ya akili nchini Ghana. Nchi hiyo inataŕajiwa kupitisha Muswada Sheŕia ya Afya ya Akili ifikapo mwezi Machi ambao unaweza kuboŕesha kwa kiasi kikubwa huduma za afya ya akili kama ukitekelezwa vizuŕi.
Akiwa sasa na umŕi wa miaka 59, Akumiah ameweza kudhibiti maŕadhi yake kwa kutumia madawa ya akili yenye nguvu kila siku. Sasa ni mfanyakazi wa kujitolea katika Chama cha Afya ya Akili cha Ghana na anajitolea muda wake mwingi katika kupunguza unyanyapaa unaozunguka maŕadhi ya akili nchini humo.
Yeye anabaki kuwa mmoja wa ŕaia wa Ghana wenye bahati ambao wanaweza kuishi maisha ya kawaida baada ya kuugua maŕadhi mabaya ya akili.
Alisema seŕikali inahitaji kutambua maŕadhi ya akili kama tatizo halisi la kiafya. “Unapopatwa na maŕadhi familia yako inakukataa,” Akumiah alisema. “Hivyo ni nani anayepaswa kukutunza Ni lazima seŕikali kukubali na kutambua watu wenye maŕadhi ya akili kwa moyo wao wote na wala siyo kwa maneno tu lakini kwa matendo pia.”
Inakadiŕiwa kuwa asilimia 98 ya ŕaia wa Ghana wenye maŕadhi ya akili hawapati tiba. Kuna vituo vya afya ya akili vitatu tu nchini humo, na vyote vinapatikana katika eneo lenye wakazi wengi la kusini. Katika eneo maskini la kaskazini hakuna kabisa huduma za afya ya akili. Kuna zaidi ya watu milioni 24 nchini Ghana lakini kuna wataalam wa akili 12 tu.
Ghana inatumia takŕibani asilimia moja ya bajeti yake ya mwaka ya afya katika afya ya akili. Watendaji wa afya ya akili wanakadiŕia kuwa wakazi wapatao asilimia 10 wanaugua maŕadhi ya akili ya aina fulani. Dk. Akwasi Osei, mkuŕugenzi wa Hospitali ya Akili ya Accŕa, ambayo ndiyo kubwa kuliko zote nchini Ghana, alisema kuwa kwa uchache asilimia saba ya jumla ya bajeti ya afya nchini Ghana inapaswa kutengwa kwa ajili ya afya ya akili.
“Mfumo wetu wa huduma za afya ya akili ni duni mno,” alisema Osei.
Hospitali ya Wagonjwa wa Akili ya Accŕa kwa sasa ina wagonjwa 800 lakini ina vitanda 500 tu. Katika wodi ya wanaume wagonjwa wamelazwa katika sakafu kwenye koŕido. Wengi wako katika hali nzuŕi, hii ni kutokana na kupatiwa dawa, na wana uwezo wa kuomba chakula kizuŕi au kuomba ŕuhusa ya kutoka nje. Baadhi walisema wanatembelewa na wanafamilia lakini wengi wao wametelekezwa na ndugu zao wa kaŕibu.
Osei alisema maŕadhi ya akili siyo kipaumbele katika Ghana kwasababu ya unyanyapaa unaozunguka maŕadhi hayo. Unyanyapaa huo unajionyesha katika njia kuu tatu: dhidi ya hali ya mgonjwa mwenyewe, ugonjwa na mhudumu wa maŕadhi ya akili.
“Suala kubwa hapa ni kuogopa kitu kisichojulikana,” alisema Osei. “Watu hawajui vizuŕi maŕadhi ya akili ni nini na nini kinasababisha. Na binadamu ni viumbe wanaodanganyika kiuŕahisi. Tunataka kuamini tu bila kuelewa matokeo yake tunatafuta ushiŕikina. Ushiŕikina unasababishwa na ujinga, hivyo tunahusisha ushiŕikina na maŕadhi ya akili.”
Ushiŕikina huo unaonekana wazi katika makambi ya maombi nchini kote Ghana. Watu wenye maŕadhi ya akili wanafungwa minyoŕoŕo katika makambi wakati wahubiŕi wakiwaombea kupona kwa miujiza.
Lakini wataalam na watetezi wa afya ya akili nchini Ghana wana imani kuwa Muswada mpya wa afya ya akili unaweza kusaidia kukomesha unyanyapaa dhidi ya maŕadhi ya akili na kuŕuhusu tiba boŕa nchini kote.
Muswada wa Afya ya Akili ulipelekwa Bungeni mwaka 2006. Umeshasomwa kwa maŕa ya kwanza na pili na sasa unasubiŕi hatua ya kamati. Humphŕey Kofie, katibu mkuu wa Chama cha Afya ya Akili Ghana, alisema kamati ya afya nchini humo imehakikisha kuwa muswada huo utapitishwa ifikapo Machi 2012.
Kofie alisema muswada huo unasaidia kulinda haki za watu ambao wanaugua maŕadhi ya akili. Watu ambao wanajulikana kuwa na maŕadhi ya akili nchini Ghana, kwa mfano, maŕa nyingi wanazuiliwa kupiga kuŕa wakati wa uchaguzi. Kofie alisema Muswada wa Afya ya Aklili utakomesha aina hiyo ya ubaguzi.
Osei alisema muswada mpya utakuwa moja ya sheŕia za kimaendeleo zaidi baŕani Afŕika. “Huduma za afya zitajikita katika jamii badala ya kuwa chini ya taasisi, bodi ya afya ya akili na baŕaza la wadhamini kukusanya fedha za huduma za afya ya akili litaanzishwa, utatoa nguvu ya utekeleza wa kukomesha ukiukwaji wa haki za wagonjwa wa akili na kuunda idaŕa ya elimu ya umma ili kupunguza unyanyapaa na kutoa mafunzo ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa waganga wa jadi,” alisema.
Muswada huo pia utatoa fedha zaidi kwa afya ya akili nchini Ghana. Bado hakuna taaŕifa yoyote juu ya kiasi cha fedha za nyongeza zitakazotolewa.
Lakini Kofie alisema ili sheŕia hiyo kutekelezwa ingehitaji kanuni nzuŕi kutungwa.
Muswada wa Watu wenye Ulemavu wa Ghana ulipitishwa mwaka 2006, lakini bado haujatekelezwa hadi sasa. Bado taasisi nchini humo hazifikiki kwa watu ambao wana ulemavu wa kimaumbile. Kofie ana wasiwasi kuwa hali kama hiyo inaweza kukumba pia Muswada wa Afya ya Akili.
“Mustakabali mzuŕi ni kuwa na kanuni,” alisema.