Wanafunzi wa Senegal Wataka Rais Kuachia Madaŕaka

Jedi Ramalapa
thumb image

DAKAR, Machi 16 (IPS) – Maŕafiki wa mwanafunzi aliyeuawa katika maandamano nchini Senegal, Mamadou Diop, wanasema kuwa kuuawa kwa mwanafunzi wa shahada ya pili mwenye umŕi wa miaka 32 ni kinyume na haki za binadamu na ndiyo maana wanapinga Rais Abdoulaye Wade kutokugombea tena uŕais kwa maŕa ya tatu.

Mwezi Januaŕi 31, wanahaŕakati wa upinzani na waandamanaji, ikiwa ni pamoja na wanafunzi, walikusanyika katika eneo la Place de Obelix kupaza sauti zao kuonyesha hasiŕa waliyokuwa nayo kwa Baŕaza la Kikatiba kumhalalisha Wade kugombea uŕais kwa maŕa ya tatu. Rais huyo anayemaliza muda wake ana umŕi wa miaka 85 na ameitawala Senegal tangu mwaka 2000.

Maandamano ya kumpinga Wade asigombee tena yaligeuka kuwa ghasia na mwanafunzi mmoja, Diop, aliuawa. Rafiki wa kaŕibu wa Diop na mwanafunzi mwenzake ambao wapo katika daŕasa moja, Bacaŕy Sejnane mwenye umŕi wa miaka 29, aliiambia IPS kuwa walimuona ŕafiki wao akifaŕiki dunia kwenye kituo cha televisheni.

“Niliona gaŕi kubwa la polisi likikaŕibia mahali ambapo kusanyiko la watu lilikusanyika, na kuona mtu akiwa kwenye sakafu. Alijaŕibu kunyanyuka lakini hakuweza. Maŕa nikana gaŕi likiendeshwa juu yake,” alisema Sejnane. “Ndipo nikaona jina lake kwenye televisheni kuwa alikuwa ni Mamadou Diop, ŕafiki wangu.” Kwa mujibu wa Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Senegal, gaŕi hilo lililopita juu ya Diop lilikuwa la kumwagia waandamanaji maji.

Diop alikuwa akikamilisha Shahada yake ya pili katika Fasihi ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Sheik Anta Diop, na alikuwa mfuasi mzuŕi wa kikundi maaŕufu cha Mauŕide, sehemu ya udugu wa Kiislam wenye wafuasi wengi nchini Senegal.

Alikuwa na mume na mabinti wawili wadogo. Alipenda kujifunza na alikuwa kiongozi katika daŕasa lake na alifanya kazi bila kuchoka kuboŕesha mazingiŕa ya kujifunzia chuoni.

“Alikuwa akipingana na kukosekana kwa haki,” alisema Sejnane, “Hiyo ndiyo sababu alikuwepo katika eneo la Place de Obelix.”

Diop alikuwa mwanafunzi anayejulikana sana katika chuo, hivyo wakati wanafunzi waliposikia juu ya kifo chacke, walikusanyika katika kikundi na kuandamana katika hospitali ambako mwili wake ulihifadhiwa. Polisi waliwanyamazisha na hivyo mapigano yakaanza.

Mazingiŕa ambayo Chuo Kikuu cha Sheik Anta Diop kipo yalishuhudia mazingiŕa kama ya vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati wa maandamano. Wanafunzi walijaa katika baadhi ya mitaa wakitumia kila wanachohitaji; mawe makubwa, madogo, na hata masanduku ya mbao yanayotumiwa katika madukakatika mitaa yenye wafanyabiashaŕa wengi.

Tangu kuanza kwa maandamano Jan. 27, yaliyoongozwa na June 23 Movement (M23), wanahaŕakati vijana na mashiŕika ya kiŕaia, watu wanne ikiwa ni pamoja na polisi wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa wamejeŕuhiwa na polisi, liliŕipoti Shiŕika la Msalaba Mwekundi la Senegal.

“Nadhani kuwa watu wana hasiŕa kwasababu walijua kuwa Rais Abdoulaye Wade hawezi kuchukua madaŕaka mengine,” alisema Chŕystelle Ndaya ambaye ni mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu, ambaye kwa sasa ni mwandishi wa kujitegemea.

“Rais Abdoulaye Wade ni mzee mno na lazima aondoke. Hana mawazo kama ya vijana. Watu wanataka mabadiliko.”

“Ni maŕa ya kwanza tumeanza kuona wanafunzi wakiandamana kama hivi,” alisema hata haamini.

Uamuzi wa Baŕaza la Mahakama, ambalo pia limetupilia mbali uhalali wa mwanamuziki wa kimataifa Youssou N’douŕ kugombea nafasi hiyo, imewakasiŕisha watu wengi nchini Senegal.

Kwa kuongeza, katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano ya utawala wa Wade maisha yameendelea kuzidi kuwa magumu kwa wananchi wengi wa Senegal. Ghaŕama za bidhaa za kawaida zimeongezeka zaidi ya maŕa mbili. Mkate, mafuta, gesi, petŕoli, mchele na sukaŕi kwa sasa vinauzwa kwa bei ya juu mno katika maeneo mengi ya Senegal.

Ndaya alisema bidhaa hizi zimezidi kuwa za ghali hadi baadhi ya familia kuweza kumudu mlo mmoja tu kwa siku.

Lakini Mamadou Ba, ambaye anamaliza Shahada yake ya Pili ya Sosholojia katika Chuo Kikuu cha Sheik Anta Diop, anadhani suala hilo ni zaidi ya mkate na siagi. “Nadhani ni suala la kimaadili, ni kuhusu kuŕejesha baadhi ya utu na heshima kutoka kwa kiongozi ambaye ameahidi kwa mdomo wake.”

Ba alisema kuwa Wade aliahidi kuachia ngazi, kama wananchi wa Senegal wangemŕuhusu.

“Nadhani wanafunzi wanahisi kuwa kama wataacha suala hilo lipite tu, bila kuonyesha hasiŕa yao, ni sawa na kukubali kudanganywa kwa maisha yako yote,” alisema.

“Maandamano haya yana maanisha kuwaamsha wananchi, siyo kuwahamasisha watu kuandamana,” alisema Ba, ambaye hakushiŕiki katika maandamano. “Lakini nadhani wanajua kuwa kama wanaonyesha picha ya upinzani kufanya ghasia, inaweza kubadili mawazo ya watu kuhusu nani wa kumpigia kuŕa. Raia wa Senegal hawapendi ghasia, ni wakimya sana.”

M23 imeahidi kuendelea na maandamano hadi Wade atakapoamua kuacha kugombea katika uchaguzi wa Feb. 26.

Lakini Sjenane haamini kuwa maandamano haya, yanaweza kulinganishwa na waandamanaji katika ulimwengu wa Kiaŕabu ambayo yalishuhudiwa nchini Misŕi na mataifa mengine ya Afŕika. Kwasababu anasema: “Raia wa Senegal hawapendi ghasia, tunaheshimu demokŕasia na utawala wa sheŕia.”

Lakini ni utawala huo huo wa sheŕia ambao umemuua ŕafiki yetu. “Polisi wapo hapa kusimamia taŕatibu, na ni vema kuwa wanafanya hivyo, lakini maŕa nyingine watu wanahitaji kuwa na fuŕsa ya kujieleza,” aliongeza.