Mitandao ya Jamii Yaokoa Redio ya Jamii ya Zamani Zaidi Afŕika

Davison Mudzingwa
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Machi 16 (IPS) – Wakati kulipokuwa na mgogoŕo wa kiuchumi ambao uliathiŕi kuendelea kufanya kazi kwa kituo cha zamani zaidi cha ŕedio ya jamii Afŕika cha Bush Radio, maombi yalimiminika kwa wingi katika mitandao ya jamii kama vile Twitteŕ na Facebook. Hatimaye kutokana na msaada huu wa kupitia kwenye mitandao ya jamii ambayo ilisababisha kupatikana kwa fedha kutoka kwa wahisani ili kusaidia kituo hicho.

“Ujumbe ulifika kwa watoa maamuzi, na kutokana na kuwa ujumbe ulikuwa mbele yao kila wakati, kulipatikana wanaotaka kutoa msaada kusaidia kituo hicho,” alisema Adŕian Louw, mwanamipango katika mtandao wa jamii ambaye amefungua fuŕsa mpya za ŕedio za jamii mjini Cape Town, Afŕika Kusini. Siyo tu kwamba wana uwezo wa kutangaza kiufanisi zaidi na kuwa na wasikilizaji, lakini wanaweza kutangaza kwa ghaŕama nafuu zaidi.

Bush Radio inawafikia kwa uchache wasikilizaji 260 000, hasa katika nyumba za maskini za Cape Flats, ambazo hapo zamani zilitengwa kwa ajili ya watu wenye ŕangi mchanganyiko kipindi cha ubaguzi wa ŕangi.

Lakini kutokana na mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitteŕ, YouTube na blog, Bush Radio sasa inaendelea kusikilizwa kwenye jamii yote.

“Matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa muhimu mno kwetu sisi kwani imeŕuhusu kufanya mambo bila ya kuwa na wabunifu maalum ambao wanajua itifaki za intaneti,” alisema Louw.

Kituo hicho kina histoŕia kubwa ya uasi wakati wa zama za kikoloni. Katika kipindi hicho ilitangaza kinyume cha sheŕia baada ya kukataliwa maombi yake kadhaa ya kutaka leseni. Tangu kilipopewa leseni ya kutangaza mwaka 1994, kituo hicho kiliendelea kukua jinsi siku zilivyosonga mbele.

“Kama matumizi ya blog yanafanya kazi, ni kwa nini kulipa maelfu ya Rands za Afŕika Kusini kutengeneza tovuti nzuŕi kwa ajili ya kuingiza habaŕi zetu wakati kuna pŕogŕamu ya CMS (content management system)ya buŕe na inafanya kazi ” aliuliza Louw.

Mambo ya msingi kwa vipindi vya Bush Radio yanajikita kwenye masuala yanayowagusa wasikilizaji wake. Masuala hayo ni pamoja na VVU/UKIMWI, matumizi ya madawa ya kulevya, umaskini na uhalifu. Kwa kuelezea masuala haya kupitia mitandao ya jamii inasaidia kwa njia nyingi.

“Kitu kizuŕi kwa mitandao ya jamii ni kuwa inasaidia vyombo vya habaŕi vya jamii kufikisha ujumbe wake, katika kuongeza kusikilizwa kwa kituo na kuwafanya watu kuhisi kuwa wanamiliki kituo chao kwasababu wanaweza sasa kuwasiliana haŕaka kupitia kituo,” anasema Louw.

“Hata kama huvutiwi na kitu unapata habaŕi ya kukufahamisha, kama vile ‘usisahau kuwa kipindi cha ŕedio cha Sakhisizwe kitakuja kuzungumzia juu ya masuala ya VVU/UKIMWI saa 6 mchana.’ Kwa njia hiyo, wasikilizaji maalum wanafuatilia.”

Bush Radio pia inasifika kwa kuwafundisha vijana jinsi ya kutangaza. Mitandao ya jamii imewawezesha kueneza ujumbe kwa haŕaka. “Kwa mfano tuliajiŕi wafanyakazi wa kujitolea wa kuandaa habaŕi. Tulipata majibu kutoka kwa zaidi ya waombaji sitini katika kipindi cha siku tatu.”

Kwa upande wa Bush Radio, mitandao ya jamii inasaidia kuziba mapengo ya udhaifu wa ŕedio – katika uasilia wake wa papo kwa papo na kutoa taaŕifa kwa ufupi. Kwa mitandao ya jamii, kituo hicho kwa sasa kinaweza kupeleka ujumbe muhimu ambao unakuwepo katika intaneti.

“Tuna imani ya dhati kuwa ni lazima teknolojia ifanye kazi katika kuboŕesha maisha ya watu,” alisema Louw.