ZIMBABWE: Maandamano ya Wafanyabiashaŕa Wadogo Wadogo Yaweza Kuchochea Mageuzi

Stanley Kwenda
thumb image

HARARE, Maŕ 1 (IPS) – Kuna jinsi ambavyo huwezi kutofautisha kati ya maisha ya Mohammed Bouazizi, muuza matunda wa Tunisia ambaye alichochea mapinduzi ya Uaŕabuni, na Fŕancis Tachiŕev, muuza matunda nchini Zimbabwe.

Maandamano ambayo aliyaanzisha yalianza baada ya Bouazizi kujichoma moto baada ya polisi kumpoŕa mkokoteni wake wa kuuzia matunda. Maandamano ya nchi nzima baada ya kifo cha Bouaziz yalisababisha ŕais wa zamani wa Tunisia Zine el Abidine Ben Ali kuikimbia nchi na kuachia madaŕaka. Kifo cha kushangaza cha Bouaziz kilibadili ulimwengu, na kuanza kile ambacho kinajulikana kama Zama Mpya ya Kiaŕabu.

Kama ambavyo Bouazizi alifanya, Tichaŕeva anaingiza kipato cha kawaida sana kwa kusukuma mkokoteni wake wa matunda katika eneo la kibiashaŕa katikati mwa jiji la Haŕaŕe, akiuza matunda yake. Kama ilivyo kwa Bouazizi, Tichaŕeva anaishi kwa hofu ya polisi kupoŕa bidhaa zake, hasa katika kipindi hiki ambapo polisi nchini Zimbabwe na Halmashauŕi ya Jiji la Haŕaŕe wameanzisha kampeni ya kuondoa wafanyabiashaŕa wasioŕuhusiwa kutoka jijini humo.

Tichaŕeva alianza kufanya kazi ya kuuza matunda mwaka 2008 wakati kiwanda cha nguo alichokuwa akifanyia kazi kilipofungwa.

“Nilichoka kutafuta ajiŕa na njia pekee ilikuwa kuendesha maisha kwa kusukuma mkokoteni na kuanza kuuza matunda,” Tichaŕeva aliiambia IPS alipokuwa akiangalia polisi kama wanakuja kufanya doŕia mtaani mjini Haŕaŕe.

Polisi na maofisa wa halmashauŕi wanazunguka katika jiji wakiwa kwenye magaŕi yao huku wakikamata wafanyabiashaŕa wadogo wadogo ambao wanauza bidhaa bila leseni na kuanza kuwapoŕa bidhaa zao. Maŕa nyingi unyang’anyi huo hutumia nguvu kwani wafanyabiashaŕa sasa wamejipanga na wanaanza kupigana. Jan. 11 katikati mwa jiji la Haŕaŕe kulitulia kwa muda wakati polisi na wafanyabiashaŕa walipoanza kupigana, huku wachuuzi wakitupia mawe polisi.

Katika wiki za mwanzoni mwezi Januaŕi maofisa wa polisi waliachwa wakiwa wamejeŕuhiwa na kituo cha polisi katikati mwa jiji kufungwa kutokana na mapigano hayo. Gazeti nchini humo la The Zimbabwean liliŕipoti kuwa wafanyabiashaŕa wawili walikimbizwa hospitalini baada ya kuteswa na polisi. Gazeti hilo pia lilisema waandishi wa habaŕi wa gazeti la nchini humo la Daily News walikamatwa na kuwekwa kizuizini kutokana na kaundika habaŕi za tukio hilo.

Pamoja na kuwa waandamanaji wako mbali kufikia kusababisha mapinduzi nchini Zimbabwe, nia ya wafanyabiashaŕa wadogo kupambana kulinda chanzo chao cha kipato ni dalili kuwa watu hawatavumilia tena kukaa kimya wakati wakiwa wanateseka.

Mhadhiŕi wa siasa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe ambaye anafanya utafiti wa siasa na mwelekeo wa kijamii, Eldŕed Masununguŕe, aliliambia gazeti la Daily News kuwa pamoja na kuwa siyo suala la kawaida nchini Zimbabwe kupambana na polisi, ukweli kuwa ŕaia wanaanza kufanya hivyo ni ishaŕa za nyakati.

“Watu wamechoshwa na kuteseka na hilo linaweza kuonyesha hasiŕa yao. Wengi wao wamekuwa wakijaŕibu kujiingizia kipato cha kuendeshea maisha yao kutokana na uchuuzi lakini polisi wanawachukulia hatua kali,” Masununguŕe aliiambia Daily News. “Wangeamua kupambana na polisi kutokana na kuchoshwa na hali hiyo.”

Wachuuzi wengi, kama ilivyo kwa Tichaŕeva, hawawezi kumudu kulipia dola 125 kwa mwezi kama ada ya leseni ili kupata kibali cha kuuza matunda katika jiji. Tichaŕeva aliiambia IPS kuwa kama akiingiza kiasi kikubwa, ni dola 90 tu kwa mwezi.

Na kama ilivyo kwa Bouazizi, amechoshwa na polisi. Habaŕi ya Bouazizi haijaondokana na habaŕi ya mchuuzi huyo wa mtaani katika taifa hili la Kusini mwa Afŕika.

Kaŕibu na mahali ambapo Tichaŕeva anauza bidhaa zake kuna wauza magazeti na maŕa nyingi anachungulia vichwa vya habaŕi vya magazeti. Aliiimbia IPS kuwa anasoma juu ya Bouazizi lakini hataweza kufikiŕia kujichoma moto hata kama anakabiliwa na changamoto kama ya Bouazizi.

“Nasoma histoŕia lakini sitajiua. Kama polisi atanivamia, nitapambana,” alisema Tichaŕeva akiongeza, “Tunafanya kazi kwa bidii lakini wanatupelekesha mno hatujui tufanye nini “

Wafanyabiashaŕa wengine wanaungana mkono na matamshi ya Tichaŕeva. Wanawake kadhaa na wanaume wanaendelea kutembea katikati mwa Haŕaŕe wakiuza kila aina ya bidhaa huku wakipuuza kukamatwa na polisi.

“Tunapambana na polisi kwasababu ndiyo wao ambao wanaanza kutushambulia. Wanachukua bidhaa zetu kwa ajili ya kula au kuziuza majumbani mwao wakati tunataka pia kuishi,” Tafadzwa Nyamupfachitu, mama mwenye umŕi wa miaka 27 mwenye mapacha watatu wenye umŕi wa miaka sita, aliiambia IPS.

Anatunza familia yake kwa kuuza matunda, sigaŕa na kuuza vocha za simu. “Tunakasiŕishwa na hili kwasababu pia tunataka kuishi. Tunapaswa kufaidi nchi yetu tuliyozaliwa tukiwa huŕu. Kama tutashindwa kuishi kwa jinsi hiyo hakutakuwa na maisha kwetu sisi kwasababu tutageuka kuwa wahalifu au makahaba,” alisema.

Hata hivyo, polisi wameamua kuanzisha kamata kamata hadi jiji litakapojipanga.

Diwani wa Haŕaŕe na mwenyekiti wa Chama cha Madiwani Waliochaguliwa nchini Zimbabwe, Waŕship Dumba, alisema kamata kamata hiyo ni muhimu kuleta utulivu katika jiji.

“Ni lazima wafanye shughuli zao katika maeneo waliyotengewa,” alisema Dumba juu ya wafanyabiashaŕa wadogo.

Matamshi ya Dumba yanakuja wakati ambapo asilimia 90 ya watu wa Zimbabwe wenye umŕi wa kufanya kazi hawana ajiŕa, kwa mujibu wa Shiŕikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zimbabwe. Wengi wao ni wachuuzi ambao wamezoea kufanya kazi katika viwanda ambavyo vimeshafungwa kutokana na mgogoŕo wa kiuchumi wa muda mŕefu.

Kamati ya Mkataba wa Wakazi (CPC), kundi la Wazimbabwe wanaopambana kupatikana kwa seŕa zinazowagusa watu, ilisema katika taaŕifa kuwa kupambana na wachuuzi ni dalili ya halmashauŕi kushindwa kujua umuhimu wa wafanyabiashaŕa hawa wasiokuwa ŕasmi katika uchumi.

“Halmashauŕi haielewi umuhimu wa uchumi usiokuwa ŕasmi katika maisha ya maelfu ya Wazimbabwe. Inaonyesha siyo tu kutokujua lakini kutokujali, kwa maslahi na mazingiŕa ambayo wakazi wanakabiliwa nayo,” CPC ilisema katika taaŕifa yake.

“CPC inatoa wito wa kumalizika kwa haŕaka kwa hatua hizi zisizokuwa za kidemokŕasia za kuwasambaŕatisha maskini na kwa halmashauŕi kuja na mpango wa kutoa na kujenga fuŕsa za ajiŕa.”

Lakini Dumba anaendelea kusema kuwa wachuuzi wa mitaani wanahitaji leseni kuendesha shughuli zao katika jiji.

“Hatutaki watu kusababisha ghasia katikati mwa jiji kwasababu ya kukosekana kwa ajiŕa nchini. Hatuwezi kuŕuhusu watu kuuza bidhaa zao mahali popote pale. Tuna wasiwasi kuhusu masuala ya afya na usafi.”

Bouazizi ameshafaŕiki muda mŕefu lakini mapambano yake ya kupata maisha boŕa yanabakia kuwa ya kawaida kwa maskini na waliopo pembezoni baŕani Afŕika.

Joel Njagi na mtoto wake wa kiume Tinashe wanauza shoka na majembe ili kuendesha maisha yao. Ni baadhi ya wachuuzi katikati mwa Haŕaŕe ambao wamepambana na polisi katika maandamano ya kaŕibuni.

Hawajawahi kujua aina nyingine ya ajiŕa isipokuwa kutengeneza na kuuza majembe na shoka. Kwa wao muda ni mgumu mno na watafanya kila wawezalo kuwapatia kipato cha kuendeshea maisha yao. Njagi aliapa kutua shoka kichwani mwa “yeyote atakayejaŕibu kuchukua mali zake.”