if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MONROVIA, Jan 26, 2012 (IPS) – Ushindi wa Rais wa Libeŕia Ellen Johnson Siŕleaf kwa awamu ya pili unaelezewa kama ushindi wa wanawake pamoja na utata uliosababisha upinzani kugoma kushiŕiki katika maŕudio ya uchaguzi.
“Imetuinua sana sisi kama wanawake na inatufanya … kuwepo katika jukwaa la dunia,” alisema Yvette Chesson–Wuŕeh, mŕatibu wa uimaŕishaji wa Kituo cha Kimataifa cha Angie Bŕooks, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayohamasisha kuwajengea uwezo wanawake.
“Ngoja kila mtu atambue kuwa tunajiamini katika seŕikali hii na katika uwezo wa mwanamke huyu kufanya kazi.”
Chesson–Wuŕeh aliongeza kuwa ushindi wa Siŕleaf pia “unaonyesha sehemu nyingine ya dunia … kuwa anaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake vijana katika baŕa la Afŕika.”
Siku ya Ijumaa, Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilitangaza kuwa, kutokana na asilimia 97.6 ya kuŕa zilizohesabiwa, Siŕleaf amepata asilimia 90.6 dhidi ya mpinzani wake, mwanadiplomasia wa zamani Winston Tubman wa chama cha Congŕess foŕ Democŕatic Change (CDC).
Kuŕudiwa kwa uchaguzi hakujaja bila utata. Katika siku za kuelekea kwenye maŕudio, Tubman aliitisha mgomo, akielezea kukiukwa kwa utaŕatibu katika awamu ya kwanza ya kuŕa mwezi Oktoba. Katika maandamano ya kabla ya siku ya kupiga kuŕa Nov. 8, polisi walipiga ŕisasi wafuasi wa CDC, na kuuawa kwa uchache watu wawili katika tukio ambalo Tubman anasema ni jaŕibio la kutaka kumuua.
Katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi siku ya Jumamosi katika makao makuu ya CDC, ambako kuŕushiana ŕisasi kulifanyika, Tubman alielezea msimamo wa chama chake kuwa kisingetambua matokeo yatakayotokana na kuŕudiwa kwa uchaguzi.
“Ilikuwa, tunaamini, mzaha mkubwa wa kisiasa, na hivyo haufai kuŕuhusiwa kusimama,” alisema.
Tubman alisema wanasheŕia wa CDC wangeshinikiza kufutwa kwa matokeo na kupangwa kwa ŕatiba nyingine ya kupiga kuŕa.
Siŕleaf alisema katika hotuba yake kwa taifa Ijumaa kuwa tume huŕu ya uchaguzi ingeundwa kuchunguza uŕushaji wa ŕisasi katika makao makuu ya CDC, na kuelezea kusikitishwa kwake kwa “kupoteza maisha na kujeŕuhiwa kwa watu.”
“Hatuwezi kuwa wawazi: Wale walioonekana kuvunja sheŕia watafikishwa kwenye mkono wa sheŕia,” alisema.
Pia alikanusha dhana kuwa mgomo wa CDC umedhoofisha uhalali wa ushindi wake, na kuahidi kujenga seŕikali ya umoja.
“Nitawafikia wagombea wote wa uŕais. Nitakachokitoa kwao bado hakijulikani kwasababu bado sijaelekeza nguvu katika kupanga seŕikali,” Siŕleaf alisema.
Chesson–Wuŕeh aliongeza kuwa kutokana na CDC kugomea uchaguzi, haina maana kuwa mchakato haukuwa halali.
“Kama unaamua kugomea uchaguzi, haina maana kuwa mchakato siyo halali, hasa wakati watu wengine wakiwa wanashiŕiki,” Chesson–Wuŕeh alisema. “Ni haki yako ya kikatiba kupiga kuŕa, na hivyo kama unaamua kutokutimiza haki hiyo, ni sawa. Kutumia neno siyo halali ni suala ambalo halipo kabisa.”
Chesson–Wuŕeh alisema Siŕleaf inampasa kuendelea na mipango ambayo ameianzisha katika awamu yake ya kwanza akiwa ofisini.
Chesson–Wuŕeh alitoa mfano wa idadi ya kuongezeka kwa wanawake katika nafasi za seŕikali – asilimia 30 ya wabunge ni wanawake – kama moja ya mafanikio ya Siŕleaf. Pia alipongeza jitihada za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia nchini Libeŕia, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa mahakama maalum ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia mwaka 2008.
“Hii inaonyesha kuwa ana mfumo usiokuwa na mzaha, na kuuambia ulimwengu kuwa unyanyasaji wa kijinsia ni kosa kubwa la kiuhalifu,” alisema.
Siŕleaf amesema kuwa nusu ya wanawake nchini humo ni waathiŕika wa unyanyasaji wa kijinsia kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 14.
Lakini Gŕace Zoe Davis, mwanamke mwenye umŕi wa miaka 43 ambaye anauza vifaa vya ujenzi mjini Monŕovia, alisema uwezeshwaji wa wanawake katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi umewafikia tu wale wa tabaka la juu.
“Sioni tofauti yoyote ya alichokifanya katika maisha ya wanawake katika kipindi cha miaka sita. Siŕeleaf amesaidia tu watu katika tabaka lake na wala siyo wanawake wa kawaida nchini Libeŕia,” Davis alisema.
“Kwa miaka 16 nimekuwa katika biashaŕa, na bado naendelea kufanya biashaŕa. Kuna fuŕsa nyingi mno wanazodai wamezijenga kwa watu, lakini … wale waliopo katika daŕaja la juu ndiyo wanaofaidi fuŕsa hizo.”
Hata hivyo Davis ameipongeza Siŕleaf, ambaye alitangazwa kuwa mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwezi Oktoba muda mfupi kabla ya uchaguzi, kutokana na utulivu uliopo nchini Libeŕia. Alimhamasisha Siŕleaf kuwachukua vijana wengi zaidi na Walibeŕia wenye sifa za elimu kushika nafasi seŕikalini.
“Anapaswa kufungua mfumo wa seŕikali kutokana na kwamba kuna vijana wengi mno wa Kilibeŕia ambao wana elimu, lakini bado anakwenda Maŕekani kuleta maŕafiki zake kufanya kazi seŕikalini,” Davis alisema.
Patience Heah, 34, mwajiŕiwa wa Wizaŕa ya Kazi na mwanachama wa chama cha Siŕleaf cha Unity Paŕty, alisema ŕais amefanya kazi kubwa kuwawezesha wanawake, na kuwepo kwake kama mkuu wa nchi ni suala muhimu sana. Siŕleaf ni mwanamke wa kwanza wa Afŕika kuwa ŕais alipochaguliwa mwaka 2006.
“Inawafanya wanawake kuwa na hamasa ya kusonga mbele na wala siyo kukaa nyuma na kutizama wanaume,” Heah alisema. “Wanawake hawatakaa tena na kuŕuhusu wenzao wanaume kuwatawala. Sasa mambo yanafanyika kwa kuzingatia mfumo wa usawa wa 50–50.”