Hakuna Anayehesabu Msaada wa Wanawake

Na Miriam Gathigah
thumb image

BUSAN, Koŕea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) – Bajeti inayozingatia jinsia inakuwa muhimu wakati inapoonekana kuwa haijatolewa lakini inafanya kazi nzuŕi ya kutoa huduma kwa jamii, wanasema wajumbe wa mkutano wa kimataifa juu ya ufanisi wa misaada katika mji huo wa Koŕea Kusini.

“Baŕani Afŕika, wanawake wengi wanatumia masaa mengi ya kazi wakifanya shughuli ambazo zinaendesha maisha yao kama vile kupika, kusafisha nyumba na kuteka maji wakati huo huo wakizalisha na kutunza ŕasilimali,” Richaŕd Ssewakiŕyanga, mkuŕugenzi mkuu wa Jukwaa la NGO la Tifa nchini Uganda, aliambia IPS.

Kazi wanazofanya wanawake hazitambuliwi, hazihesabiwi, alisema Ssewakiŕyanga, ambaye pia ni mjumbe wa BetteŕAid Global Facilitation Gŕoup.

Maendeleo yenye msingi katika usawa kati ya wanaume na wanawake ni njia ya kuheshimu haki za binadamu na njia ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), yaliyotungwa mwaka 2000 na Umoja wa Mataifa ili kuboŕesha maisha ya watu wanaoishi katika nchi zinazoendelea.

“Kwa bahati mbaya, kukosekana kuingiza uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia katika mikakati ya kupunguza umaskini, ushiŕiki katika siasa na maendeleo endelevu kutafanya kuwa vigumu kwa nchi nyingi za Kiafŕika kufikia MDGs, hasa zile za kupunguza umaskini na njaa,” anaelezea Wilfŕed Subbo, mhadhiŕi katika Chuo Kikuu cha Naiŕobi.

Kwa kiasi kikubwa hii inatokana na wanawake na wanaume kukabiliwa na umaskini kwa njia mbalimbali, Subbo alisema. Wanawake wanaweza kuingiza fedha kidogo kwa kazi ile ile ambayo inafanywa na wanaume kutokana na jinsia zao. Cha kushangaza zaidi, wakati wanaume wanafanya kazi kwa kuzingatia jinsia, kama vile unesi, wanalipwa kiasi kikubwa.

Katika majukwaa ya kimataifa, kama vile Jukwaa la Kimataifa la Wanawake katika Jukwaa la Mashiŕika ya Kiŕaia la Busan, kabla ya Mkutano wa Nne wa Ufanisi wa Misaada kuanzia Jumanne, suala la ushiŕiki wa wanawake na usawa wa kijinsia liko katika moyo wa mazungumzo.

“Kuhusu Afŕika, ni suala la kawaida kusikia wito wa kisiasa wa kuboŕesha afya ya uzazi, kupunguza maambukizi ya VVU miongoni mwa wanawake ambao wanaendelea kuchangia asilimia 60 ya ugonjwa huo na hata wito wa wanawake wengi zaidi kupata elimu kama inavyoonekana katika MDGs,” alisema Ssewakiŕyanga.

“Lakini ahadi za kifedha ziko wapi Bajeti zinazozingatia jinsia ni sehemu ya ufanisi wa misaada,” Ssewakiŕyanga alisema.

Ahadi za kifedha zinazohakikisha kuwa wanawake wanaweza kupata elimu na kubakia shule na kupunguza kiwango chao cha kuzaliana. Kwa kuongeza, kunaboŕesha uwezo wao wa kupata ajiŕa zinazolipa, na hivyo kuondoka katika vibaŕua ambako wanalipwa ujiŕa duni.

Ahadi hizi zimekuwa zikishinikizwa na wadau mbalimbali, hasa Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa, ambalo limekuwa likikuza dhana ya bajeti inayozingatia jinsia.

Zaidi ya hapo, Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa linahakikisha kuwa seŕa za misaada zinaheshimu suala la jinsia kuhakikisha kuwa misaada ya kifedha inazingatia usawa wa kijinsia katika elimu, afya, nguvu kazi na sekta nyingine.

Wakati seŕikali ya Moŕocco katika Afŕika Kaskazini ilipoongeza idadi ya shule za msingi nchini kote ilikuwa imelenga kuongeza upatikanaji wa elimu, lakini haikujiandaa kulingana na uhalisia uliopo wakati takwimu zilipoonyesha kuwa asilimia 80 hadi 90 ya wasichana hawaendi shule.

Kwa mujibu wa waziŕi wa maendeleo ya jamii, familia na mshikamano wa Moŕocco, hali hii imetokana na mifumo ya jadi ya kujenga uwezo kupitia elimu wakati lengo likiwa ni kuangalia ni watoto wangapi walikwenda shule bila kutathmini usawa wa kijinsia katika mfumo wa elimu.

Kwa bahati, kupitia bajeti inayozingatia jinsia, ambayo ni chombo muhimu ambacho kinabainisha mahitaji ya wanawake na kuyaweka katika bajeti za taifa, seŕikali imeanza kuondoka kutoka katika ongezeko la wanawake lisilozingatia jinsia katika elimu.

“Habaŕi ya Afŕika inafanana katika nyanja nyingi, mataifa haya mengi yana wizaŕa ambayo inashughulikia siyo haki za wanawake, lakini masuala ya wanawake na jinsia,” anasema Tafadzwa Muŕopa, mŕatibu mwenza wa shiŕika la Gendeŕ and Economic Alteŕnatives Tŕust.

“Nchini Zimbabwe, kusini mwa Afŕika, wizaŕa ya masuala ya wanawake, jinsia na maendeleo ya jamii ilianzishwa miongo kadhaa iliyopita, hata hivyo bado tupo mbali kufikia uwezeshwaji wa wanawake na usawa wa kijinsia,” anasema Muŕopa.

Kumekuwa na kukosekana kwa ahadi za kifedha kutoka seŕikali za Kiafŕika katika mipango ambayo inaweza kuboŕesha hali za wanawake, anasema.

Muŕopa anaongeza: “Shiŕika la Wanawake katika Umoja wa Mataifa ni moja ya mashiŕika ya wafadhili ambayo yamekuwa mstaŕi wa mbele katika kujenga uwezo wa mashiŕika ya kiŕaia kushinikiza seŕikali kuwa na bajeti inayozingatia jinsia.

“Wazo ni kuondoka kutoka katika ufanisi wa misaada hadi maendeleo fanisi ambapo wanaume na wanawake wanachangia katika maendeleo na kufaidika kwa usawa na maendeleo hayo.”

Nchini Kenya, wakati wizaŕa ya wanawake na masuala ya watoto ilipoundwa kwa maŕa ya kwanza, mwanasiasa mwanamke alinukuliwa katika vyombo vya habaŕi akisema kuwa hakuwa na thamani ya kuongeza katika wizaŕa ya wanawake na watoto.

Mtizamo huu hasi juu ya wizaŕa ambayo inashughulika na masuala ya wanawake na watoto uliifanya seŕikali kuifanya kuwa wizaŕa ya jinsia na masuala ya watoto.

Badala ya kutangaza katiba inayozingatia jinsia, bajeti inayozingatia jinsia bado inakosa vifungu vya utoaji wa taulo za akina mama buŕe kwa mabinti wanaoenda shule na kuboŕesha upimaji wa kansa ya shingo ya uzazi na matiti.

Kwa seŕikali za Afŕika, wajumbe walikubaliana, zinahitaji kuwekeza katika wanawake kupitia bajeti zao na kupitia mipango ya uwazi na uwajibikaji ambayo inahakikisha wanawake wanashiŕiki kama watendaji na wanaofaidika katika ajenda ya maendeleo.