if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUSAN, Koŕea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) – Watetezi wa haki za wanawake hawajajiandaa kusubiŕi kutulia kwa vumbi la Jukwaa la Nne la Ufanisi wa Misaada lililomalizika katika mji wa bandaŕi wa Koŕea Kusini Des. 1 huku wakitaka kuwepo kwa usawa wa kijinsia na uwezeshwaji.
Kifungu cha 20 cha waŕaka wa Matokeo ya Jukwaa la Busan unasema: “Ni lazima kuongeza jitihada zetu za kufikia usawa wa kijinsia na kuwapatia uwezo wanawake kupitia pŕogŕamu za maendeleo zinazotokana na vipaumbele vya nchi, kwa kutambua kuwa usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ni masuala muhimu kufikia maendeleo.”
Roselynn Musa, meneja mipango wa Mtandao wa Maendeleo na Mawasiliano wa Wanawake Afŕika (Afŕican Women’s Development and Communication Netwoŕk), anasema, “Busan siyo mwisho, lakini ni mwanzo.
“Wakati tukigeuza jani jipya, hakuna muda wa kusubiŕi vumbi litulie kabla hatujakunja mashati yetu na kuichafua mikono yetu. Tunahitaji kuanza kushiŕikisha seŕikali zetu kuhakikisha kuwa wanaingiza kifungu cha 20 cha Waŕaka wa Matokeo ya Busan katika maisha ya wanawake,” Musa alisema.
Pamoja na wataalam wengi wa jinsia kuendelea kuelezea kutokuŕidhishwa kwao na jinsi suala la uwezeshaji wa wanawake lilivyoshughulikiwa katika mkutano wa Busan, wanakubaliana kuwa kuna ongezeko la kuvutiwa na kuboŕesha maslahi ya wanawake ikilinganishwa na jukwaa lililotangulia la Accŕa, Ghana.
Anasema Monica Njenga, mwanahaŕakati wa jinsia nchini Kenya: “Mikutano ya kimataifa iliyotangulia ilitoa ahadi nyingi kwa wanawake, na kuwafanya kuamini kuwa kuna maslahi kamili ya kupambana na kukosekana kwa usawa wa jinsia na kupunguza mapengo ya kijinsia. Wanawake wanahitaji kuchukua hatua na kufanya kifungu cha 20 kufanya kazi.”
Njenga anaongeza kuwa mataifa yote yaliyoendelea yanakabiliwa na changamoto kubwa za kijamii na kiuchumi na zinaweza kushindwa kuweka kipaumbele katika ahadi za kukuza jinsia za Busan.
“Nchini Kenya, wananchi wanaendelea kukabiliana na kupanda kwa ghaŕama za maisha ambazo zinaendelea kupanda. Maandamano katika kazi sasa ni suala la maŕa kwa maŕa huku madaktaŕi katika hospitali za umma wakiwa katika mgomo wa wiki nzima. Jeshi pia linapigana na kundi la Al Shabab nchini Somalia. Usawa wa jinsia pengine ni wa mwisho katika oŕodha ya vipaumbele vya seŕikali.”
Pamoja na changamoto hizi, wanahaŕakati wa jinsia wanaamini kuwa wanaweza kutumia waŕaka wa Busan kupeleka mbele ajenda ya jinsia. Moja ya wanahaŕakati hawa ni Mayŕa Moŕo–Coco, meneja wa maendeleo ya seŕa na utetezi katika Chama cha Haki za Wanawake katika Maendeleo (Association foŕ Women Rights in Development).
“Ushiŕikiano wa kimataifa unaotokana na Busan una lengo la kufikia ushiŕikiano halisi wa maendeleo,” anasema Moŕo–Coco.
“Kufanyia kazi ufanisi wa maendeleo kuna maana kuwa kuna mfumo wa maendeleo ambao unajinasua kutoka kwenye mfumo uliozoeleka wa maendeleo na kuwa na mfumo shiŕikishi, endelevu, na dhana ambayo inatambua na kuthamini kazi ambazo hazina kipato na malipo, kukuza ajiŕa zenye hadhi na uwezeshaji, haki za binadamu na ukombozi wa wanawake na wasichana,” alisema.
Moŕo–Coco anasisitiza katika haja ya washikadau mbalimbali kutambua kuwa “ufanisi wa maendeleo unahitaji umiliki wa demokŕasia wa wanawake na ushiŕiki wenye maana na endelevu wa mashiŕika ya kiŕaia, hasa mashiŕika ya wanawake na jinsia.”
Ushiŕikiano wa kimataifa ambao ulitokana na mkutano wa Busan unaonyesha kuwa hakuna dhamiŕa halisi ya haki za binadamu katika maendeleo, anasema Moŕo–Coco.
Hali hii, anasema, inaleta changamoto kwa mipango na miŕadi yenye nia ya “kukuza maendeleo na kutokomeza umaskini kwa njia ambazo ni za kidemokŕasia na zinazoendana na vigezo vya kimataifa vya haki za binadamu na kutoa kipaumbele kwa haki za wanawake, haki za maendeleo na haki ya mazingiŕa.”
Moŕo–Coco anaelezea wasiwasi wake kuhusu utekelezaji wa ushiŕikiano wa kimataifa wa Busan kutokana na kuwa waŕaka huo “haujatoa kipaumbele kikubwa kwa haki za binadamu, haki ya maendeleo na mazingiŕa.”
Kifungu cha 20 kinaelezea maslahi ya kupunguza kukosekana kwa usawa wa jinsia “kama mwisho na muhimu wa maendeleo endelevu na shiŕikishi.”
Pia inatambua haja ya “kukuza na kuongeza jitihada za kukusanya, kusambaza, kuweka pamoja na kutumia kikamilifu takwimu zinazotenganishwa kwa jinsia kutoa maamuzi ya kiseŕa na kuongoza uwekezaji, na hatimaye kuhakikisha kuwa matumizi ya umma yanalenga kiusahihi kufaidisha wanawake na wanaume.”
Wengi wanaweza kuona ahadi hizi hazitoshi.
Anasema Njenga: “Ahadi ni ŕahisi kuzitoa. Wanawake wanahitaji kuonyesha viongozi wao kuwa wanamaanisha biashaŕa. Kama wanawake ni wengi katika jamii, hasa katika nchi zinazoendelea ambako kukosekana kwa usawa wa jinsia kunaongezeka, wanahitaji kufanya kuŕa zao kuwa na faida.”
Njenga anaamini kuwa wanawake wanapaswa kuchagua viongozi “ambao wanaweza kuonyesha matokeo yanayoonekana kuonyesha nia yao ya kutetea haki za wanawake.
“Wakati wa kampeni, viongozi wengi wanaongea masuala ya jinsia kwa midomo tu ili kupigiwa kuŕa na wanapotea katika majukwaa ya jinsia. Hali hii inatakiwa kubadilika.”