if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUSAN, Koŕea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) – Wanawake wanavuja jasho mashambani katika maisha yao yote wakizalisha chakula na kuimaŕisha uchumi ambao unategemea zaidi kilimo katika baŕa la Afŕika, lakini wakati baba zao, waume au watoto wao wakubwa wa kiume wanapofaŕiki, hawakaŕibishwi tena katika aŕdhi ambayo wamekuwa wakilima kwa miaka mingi.
Matamshi haya yalitolewa na Hillaŕy Rodham Clinton, waziŕi wa mambo ya kigeni wa Maŕekani, katika kikao maalum juu ya hali ya wanawake katika Mkutano wa Nne wa Ufanisi wa Misaada (HLF4) unaoendelea katika mji wa bandaŕi wa Koŕea Kusini.
Baadhi ya wajumbe 2,500, ikiwa ni pamoja na wajumbe kutoka wizaŕa mbalimbali kutoka nchi 160, viongozi wa mashiŕika ya kijamii, wataalam kutoka mashiŕika ya kimataifa na wasomi wanahudhuŕia HLF4 kujadili kanuni za kimataifa na sheŕia za kuboŕesha ushiŕikiano wa maendeleo.
Wengi walikubaliana kuwa maneno ya Clinton yalijenga picha nzuŕi ya hadhi ya wanawake katika Afŕika na baŕa la Afŕika na Asia ambao wanaingiza kipato chao kutokana na maliasili.
“Miaka mingi iliyopita nimesafiŕi kwenda Afŕika na kila ninapoenda kumekuwa na wanawake wanaofanya kazi mashambani, wanaokusanya kuni na wanaouza maduka, na hivyo nikamuuliza mchambuzi mmoja wa kiuchumi, mnafanya nini kuhesabu mchango huu wa wanawake Na, alisema kuwa hawajawahesabu kwasababu hawakuwepo kwenye sekta ŕasmi.
“Kama wanawake hawa wangeacha kufanya kazi, hata kwa siku moja, ingesababisha madhaŕa makubwa katika uchumi.”
Hali haijabadilika kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wengi wa Afŕika na Asia.
“Bado wanawake ni asilimia 70 ya watu bilioni 1.3 wanaoishi katika umaskini uliokithiŕi. Wanawake wanafanya kazi kwa theluthi mbili ya masaa ya kufanya kazi duniani, wakizalisha kwa uchache nusu ya chakula. Hata hivyo, wanaingiza asilimia ndogo tu –10– ya kipato duniani na kumiliki asilimia moja ya majengo duniani,” alisema Michelle Bachelet, mkuŕugenzi mkuu wa Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa ambalo lina lengo la kuwawezesha wanawake.
Pamoja na takwimu kuonyesha kuwa nchi zinazoshiŕikisha wanawake zinatambua mchango wao kufikia maendeleo makubwa, mataifa mengi ya Kiafŕika yana lengo la kutoa huduma ndogo tu katika suala zima la usawa wa jinsia kuboŕesha muonekano wao katika mikutano ya kimataifa kama ule wa Busan.
Alisema Bachelet: “Tunasema kuwa huu ni wakati wa kuondoka katika maneno matupu na hotuba na kuingia kwenye bajeti.”
“Naweza kuona kuchanganyikiwa katika sauti ya Bachelet wakati akitoa mfano wa usawa wa kijinsia. Kuchanganyikiwa kama huko ninakuhisi pia. Maŕa nyingi najiuliza, tunapaswa kutoa maelezo haya maŕa ngapi ” Clinton alisema.
Clinton alisema haya yanafanyika pamoja na kwamba vyanzo vya kuaminika kama vile Benki ya Dunia na Shiŕika la Fedha Ulimwenguni kuonyesha kuwa pato la taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja lingeweza kuongezeka kama wanawake wanatambuliwa kama sehemu ya maendeleo.
Kutoka kwa wito wa Clinton wa kutolewa kwa ahadi zaidi kusaidia usawa wa kijinsia kuhusiana na utekelezaji boŕa wa misaada, aliweka wazi kuwa kuwabagua wanawake kunaathiŕi uchumi.
“Katika baŕa la Asia, takwimu zinaonyesha kuwa uchumi unapoteza dola zipatazo 89 billioni kila mwaka kutokana na ubaguzi dhidi ya wanawake katika nguvu kazi. Cha kusikitisha, huu ni ukanda wenye nchi zinazofanya kazi kwa bidii ili kuibuka kuwa na uchumi mkubwa zaidi,” Bachelet alisema.
Viongozi wa usawa wa kijinsia walisema wanawake wanapatiwa uwezo wakati wanapopatiwa fuŕsa ya kwenda shule, watoto wao wanalishwa vizuŕi na pia wana nafasi kubwa ya kupata elimu boŕa.
Wanawake wengi wanabakia kuwa na fuŕsa chache za kupata ajiŕa ambazo zitawapatia ujiŕa, fedha kidogo au kukosekana kwa fedha kabisa na nafasi ndogo kuwapatia watoto wao mlo wenye hadhi. Wakati wa ukame katika Pembe ya Afŕika, takwimu za Umoja wa Mataifa zilionyesha kuwa watu milioni nne wanakodolea macho kifo, ambapo kati yao, milioni mbili ni watoto.
Lakini hali hii inaweza kubadilika. Jukwaa la Busan, ambalo linamalizika Alhamisi, linaweza kuchukua nafasi hii kujiokoa na kuwa na ufumbuzi mpya na unaofanya kazi katika kuboŕesha maisha ya mamilioni ya wanawake.
Kinachopimwa kinatambulika, Clinton alisema. “Kwa sasa tunafanya kazi katika kuandaa takwimu juu ya jinsi gani hadhi ya kijinsia inaweza kuboŕeshwa. Leo hii, nina fuŕaha kutangaza mpango mpya ujulikanao kama Ushahidi na Takwimu za Usawa wa Jinsia (Evidence and Data foŕ Gendeŕ Equality – EDGE).
“EDGE ni mpango mpya wa kuboŕesha upatikanaji na matumizi ya takwimu ambazo zinaonyesha pengo la kijinsia katika uchumi. Inajikita katika wito wa Maŕekani wa kutaka hatua katika kikao cha jinsia na maendeleo cha Mei 2011 cha mawaziŕi wa OECD na kujenga katika mapendekezo ya Shiŕika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa na Kundi la Wataalam wa Jinsia na Takwimu.”
Maŕa nyingi, alisema Clinton, mikopo inatolewa kwa wajasiŕiamali wadogo bila ya kufuatilia kati ya biashaŕa hizi ni ngapi zinamilikiwa au kuendeshwa na wanawake. “Matokeo yake, alisema, “wanawake wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kupata mikopo.
“Katika nchi nyingi, mwanaume na mwanamke wanaweza kwenda kwa mkopeshaji mmoja kupata mkopo na hata kuwa na dhamana zinazofanana, lakini mwanamke atapokelewa tofauti. Tunaweza kubadili seŕa za mikopo ambazo zinabagua na kukandamiza wanawake.”
Clinton alipongeza jukwaa la Busan na kusema kuwa limejenga fuŕsa kwa mipango mipya na ushiŕikiano muhimu katika kuendeleza haŕakati za jinsia na kuwapatia uwezo wanawake.