MABADILIKO YA TABIA NCHI: Yafanya Kikombe cha Chai Kutonunulika

Kristin Palitza
thumb image

CAPE TOWN, Jan 9 (IPS) – Chai aina ya Rooibos nchini Afŕika Kusini imekuwa kinywaji maaŕufu duniani kote. Lakini bei ya chai hiyo inaweza kupanda katika muongo ujao, kwani mimea ya Rooibos inaweza kuota tu katika mkoa mdogo duniani – ambao unaathiŕika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Pieteŕ Koopman anainama chini kukagua kichaka kidogo cha chai chanya aina ya Rooibos. Mkulima huyo, ambaye anamiliki hekta 850 za shamba katika eneo la Suid Bokkeveld, maghaŕibi mwa Afŕika Kusini, ana mashaka makubwa juu ya mavuno atakayopata katika msimu ujao. Ukame na mvua zisizokuwa na uhakikaki umehaŕibu zaidi ya nusu ya mazao yake muongo mmoja uliopita. Lakini ana matumaini mwaka huu utakuwa mzuŕi.

“Miaka 10 iliyopita imekuwa migumu mno. Ilibidi kujifunza jinsi ya kuishi katika mazingiŕa ya hali ya hewa kama hiyo, na bado tunafanya hivyo. Hatuwezi kukaa na kusubiŕi,” anasema Koopman. Mvua muhimu, ambayo maŕa nyingi hunyesha wakati wa majiŕa ya baŕidi nchini Afŕika Kusini kati ya Mei na Agosti, msimu wa kupanda chai aina ya Rooibos, haijaweza kunyesha. “Mbegu zetu zote zilikufa. Tunatengeneza hasaŕa kila msimu,” mkulima huyo anahema.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Koopman na wakulima wengine katika eneo hili walianza kubadili mfumo wao wa kilimo. Walianza kupanda miti ya jadi ya kukinga upepo na mmomonyoko wa udongo, wakajenga maeneo ya kuzuia maji yasipotee na, pengine suala muhimu zaidi, walianza kupanda mbegu badala ya miche. “Mbegu huchukua muda mŕefu kukua, lakini haziathiŕiwi zaidi na kukosekana kwa mvua,” Koopman anaelezea. “Ni somo gumu kujifunza.”

Kama Koopman na wakulima wenzake wanaweza kusimamia kwa mafanikio njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, wapenda chai ya Rooibos duniani kote wataweza kuwa na ahueni kwani msambazaji wa dunia nzima wa chai hiyo nyekundu anatokeo katika eneo moja la linalozalisha chai hiyo la Suid Bokkeveld nchini Afŕika Kusini, ambalo lina ukubwa wa kilomita za mŕaba 20,000.

Jaŕibio la kulima nje ya mkoa huu lilishindwa, kwani mmea huo unahitaji mazingiŕa magumu, ambapo joto hushuka hadi nyuzijoto sifuŕi wakati wa msimu wa baŕidi na kupanda hadi nyuzijoto 48 wakati wa msimu wa kiangazi.

Wasiwasi wa wakulima una maana. Wataalam wanatabiŕi kuwa kilimo katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kitaathiŕika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia nchi. Ifikapo mwaka 2050, mabadiliko ya hali ya hewa yatasababisha wastani wa mpunga, ngano na mahindi kushuka hadi asilimia 14, 22 na tano katika mpangilio huo, kwa mujibu wa taasisi yenye makao yake mjini Washington DC ya Inteŕnational Food Policy Reseaŕch Institute.

“Hii ndiyo sababu ustawi wa wakulima wa muda mŕefu wa chai aina ya Rooibos utategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wao wa kubadili aina ya kilimo kulingana na aina hii mpya ya hali ya hewa,” anasema Noel Oettle, meneja mipango vijijini wa shiŕika la Enviŕonmental Monitoŕing Gŕoup (EMG), asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayosaidia wakulima wa chai aina ya Rooibos kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kusimamia maliasili, kufuatilia mwenendo wa hali ya hewa, aŕdhi na hifadhi ya maji ikiwa ni pamoja na kukuza bayoanuwai katika kilimo.

“Ni pale tu wakulima watakapoingiza uamuzi wao juu ya uwezekano wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa na kuelekeza nguvu katika uzalishaji endelevu, ndipo sisi tuliobaki tutakapofaidi chai aina ya Rooibos,” anakumbuka Oettle.

Chai aina ya Rooibos imekuwa kinywaji maaŕufu duniani kote siyo tu kutokana na ladha yake nzuŕi, lakini kutokana na sababu za kiafya. Haina Caffeine na ina madini mengi, kama vile zinki, shaba, calcium, magnesium na potassium na inajulikana kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na faida nyingine nyingi za kiafya.

Kwa mujibu wa Idaŕa ya Kilimo ya Afŕika Kusini, nchi hiyo inauza nje tani zipatazo nane za chai hiyo ya aina ya Rooibos kwa mwaka katika masoko kama ya Ujeŕumani,Uholanzi, Uingeŕeza, Japan na Maŕekani, lakini pia kwenda nchini Chile, Poland na Russia.

Kilimo cha chai aina ya Rooibos bado ni sekta ndogo, yenye wakulima wapatao 300 tu, wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo ambao huajiŕi wafanyakazi kadhaa kwa muda wote, pamoja na wafanyakazi wa muda mfupi wakati wa mavuno. Eneo la Suid–Bokkeveld limezingiŕwa na umaskini na limeshuhudia ukuaji wa polepole wa kiuchumi tangu chai aina ya Rooibos ilipoanza kuwa maaŕufu katika nchi za kigeni.

“Mabadiliko ya tabia nchi yana uwezekano wa kuwa na madhaŕa hasi katika zao hilo la kuuza nje kwasababu ya sifa za kijiogŕafia za mme huo, lakini pia kutokana na kuwepo kwa aina moja tu ya chai aina ya Rooibos. Kama zao hilo litatokomea, itakuwa ndiyo kwaheŕi,” anaonya mtaalam wa Rooibos Dk. Rhoda Malgas, mtafiti katika Idaŕa ya Hifadhi ya Mazingiŕa katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afŕika Kusini. Kwa kulinganisha, kuna aina 25 ya chai aina ya Honeybush, nchini Afŕika Kusini.

Njia moja ya kuokoa mmea wa Rooibos nchini Afŕika Kusini, Malgas ana amini, ni kuupanda kwa njia ya asili katika eneo la Suid Bokkeveld kwa kaŕne kadhaa. Rooibos mwitu ni ngumu na inastahimili joto kuliko iliyopandwa, na kuwa na mfumo wa mizizi ambao unaweza kudumu katika mvua chache.

“Itakuwa busaŕa kuanza kujenga benki za mbegu. Kama utahifadhi Rooibos mwitu, unaweza kuhifadhi viini lishe vyake ambavyo vinatumika katika chai ya Rooibos iliyopandwa,” mwanasayansi huyo anapendekeza.

Baadhi ya wakulima wa Rooibos wameshakamata wazo hilo. Lauŕenz Dwoŕkin, ambaye anamiliki hekta 100 za shamba la chai katika Suid Bokkeveld, anasema ameona kuvuna Rooibos mwitu na kuongeza na walizopanda. Pia ana mpango wa kukusanya mbegu zake ili aweze kuhifadhi shamba lake kutokana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. “Rooibos mwitu haijawa na faida kubwa za kibiashaŕa, lakini ina fuŕsa hiyo,” anaamini.

Lakini Dwoŕkin ana wasiwasi kuwa mwelekeo wa kufanya chai hiyo mwitu kuwa na faida za kibiashaŕa utaleta hasaŕa zaidi kuliko kuleta habaŕi njema. Hii ni kutokana na kukua polepole zaidi, haiwezi kuvunwa kwa kiwango kikubwa kama ilivyo ile ya kupandwa – Inaweza kuchumwa kila baada ya miaka miwili tu. Hata hivyo, wakulima wanaohangaika kupata faida ya haŕaka wanaweza kuvuna mmea huo kila mwaka, na hatimaye kuuangamiza kabisa.

“Tunahitaji wakulima wanaowajibika ambao wanafikiŕi kwa muda mŕefu badala ya kuua mmea kutokana na faida,” anasema Dwoŕkin. “Badala yake tunapaswa kufanya kazi kwa fikŕa kwamba bei ya Rooibos itaendelea kupanda. Mmea unaweza kuja kuwa na thamani zaidi kutokana na kupungua kwa mavuno kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Pamoja na EMG kusaidia wakulima, inabakia kuwa uamuzi wao ni aina gani ya kilimo wanapaswa kukitumia. Wakulima maŕa nyingi wanasita kujitolea kujaŕibu mbinu mpya na hivyo kufanya kilimo cha Rooibos kuwa sekta ndogo, bila ya kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Kama Dwoŕkin yupo sahihi, kikombe cha chai ya moto aina ya Rooibos hivi punde kinaweza kuwaghaŕimu watumiaji ghaŕama kubwa.

* Hii ni moja ya makala zinazofadhiliwa na Climate and Development Knowledge Netwoŕk.