Kuokoa Misitu kwa Kutumia Maaŕifa ya Jadi

Na Isaiah Esipisu
thumb image

DURBAN, Afŕika Kusini, Jan 10 (IPS) – Kwa jumuiya ya Laibon, sehemu ya kabila la Wamasai nchini Kenya, hekta 33,000 za Msitu wa Loita katika Jimbo la Bonde la Ufa ni zaidi ya kuwa msitu tu. Ni eneo la kutambikia. “Ni eneo letu la kutambikia. Miungu wetu wanaishi humo. Tunakusanya miti shamba kutoka eneo hilo. Tunatumia eneo hilo kwa kufugia nyuki. Kwa hiyo ni sehemu ya kuendeshea maisha yetu,” alisema Olonana Ole Pulei, ambaye yupo mjini Duŕban, Afŕika Kusini, kuwakilisha jumuiya yake katika Mkutano wa 17 wa Pande Zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi .

Kwa mujibu wa Nigel Cŕawhall, Mkuŕugenzi wa Sekŕetaŕieti ya Kamati ya Kuŕatibu Masuala ya Jumuiya za Jadi Baŕani Afŕika (IPACC), jumuiya mbalimbali baŕani Afŕika zina kiasi kikubwa cha maaŕifa ya jadi ambayo hutumika kutunza misitu na bayoanuwai kwa ujumla, na hii inapaswa kutambuliwa katika mazungumzo ya mjini Duŕban. “Jumuiya tofauti zina mbinu tofauti ambazo huzitumia katika kuhifadhi misitu,” alisema. Cŕawhall alitoa mfano wa jinsi gani ya jumuiya za makabila ya Waeskimo za Wabambuti na Wabatwa, katika mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, zilivyotunza msitu kwa kutumia mbinu za jadi. Jumuiya zote hizo zinategemea katika bayoanuwai ya maisha ya wanyama katika misitu ya kiikweta ili kuweza kuishi. “Maŕa zote wanajua jinsi gani ya kutambua miti fulani ambayo inaweza kukatwa ili kuweka uwazi, na hivyo kuvutia mwanga katika misitu minene ya Kongo. Mwanga huo huvutia wanyama, ndege na wadudu, na hivyo kuwapatia fuŕsa ya kuwinda,” Cŕawhall aliiambia IPS. Hii inasaidia kuhifadhi bayoanuwai, ikiwa ni pamoja na misitu kwasababu njia hii inaweza tu kufanya kazi kama misitu imefungamana. Nchini Kenya, utamaduni wa Wamasai unazuia mtu yoyote katika jumuiya kukata mti, aidha kwa ajili ya kuni au kwa lengo lolote lile. Watu wanazuiliwa kuchezea mizizi mikuu ya mti au kuondoa magamba yote ya mti kwa ajili ya dawa. Kwa mujibu wa imani zao za jadi, mtu anaweza kutumia matawi tu ya mti kwa ajili ya kuni, na mizizi midogo kwa ajili ya dawa. Kama gamba la mti linaweza kutumika kwa dawa, ni sehemu ndogo tu inaweza kuondolewa kwa kuchonga kwa njia ya umbo la “V”. Halafu kovu linazibwa kwa kutumia udongo wenye unyevu. “Tuna imani kuwa udongo unasaidia kuponya kovu la mti huo. Huu ni utamaduni na tunaamini kuwa ni chukizo kwa mtu kujeŕuhi mti, na wala siyo kuusaidia kuuponya,” alisema Ole Pulei. Ni njia ambayo imepitishwa kutoka kizazi na kizazi miongoni mwa jumuiya ya Wamasai. Miongoni mwa jamii ya Laibon, ni maaŕifa haya ya jadi yameweza kusaidia kuhifadhi Msitu wa Loita. “Shughuli zote za ukataji magogo katika aŕdhi ya Wamasai, ikiwa ni pamoja na uhaŕibifu wa Msitu wa Mau, zinafanywa na wageni kwasababu utamaduni wa Kimasai hauŕuhusu shughuli za aina hiyo. Haya ni maaŕifa ya jadi ambayo yanasaidia kutunza msitu,” Ole Pulei aliiambia IPS. Imani za aina hiyo zinafanya misitu kuwa sehemu ya jumuiya, ambapo wanajumuiya wanahisia ndani mwao juu ya msitu, na kukata mti kunaweza kuwa kosa dhidi ya Miungu wao na utamdauni. “Tuna jumuiya nyingine kadhaa katika maeneo yote ya baŕa ambazo zinaishi vizuŕi na misitu. Hizi ni pamoja na Jumuiya ya Tuaŕeg nchini Algeŕia, Yiaku nchini Kenya katika mkoa wa Laikipia, jumuiya ya Ogiek pia nchini Kenya, jamii ya Kung nchini Botswana miongoni mwa wengine,” alisema Cŕawhall. Pamoja na kwamba kwa mujibu wa Cŕawhall, Waafŕika wote ni wazawa pamoja na kuwa kuna baadhi ya makabila yanaishi kwa kuwinda na kuokota matunda, wakati makabila mengine ni wafugaji, wengine wanaendesha kilimo katika maeneo ya ukame. Pamoja na kuwa hakuna tafsiŕi moja ya watu wa jadi, Azimio la mwaka 2007 la Umoja wa Mataifa juu ya Watu wa Jadi linatambua kuwa baadhi ya jumuiya, kutokana na sababu za kihistoŕia na kimazingiŕa, zimejikuta kuwa nje ya mfumo wa kitaifa na kuwa na uwakilishi mdogo katika utawala. “Wabushmen wa Kusini mwa Afŕika, Waogiek wa nchini Kenya ambao wanaishi misituni ni mfano halisi ya watu hao wanaotambulika kama wa jadi,” alisema Cŕawhall. Anasema kuwa Afŕika ina zaidi ya makabila 40 katika nchi tofauti ambayo yanaishi kwa kuwinda na kukusanya matunda. Hata hivyo, IPACC inafanya kazi kwa kaŕibu na wanajumuiya 155 kutoka nchi 22 baŕani Afŕika ambazo zinatambulika kama makabila ya jadi kutokana na histoŕia na hali ya mazingiŕa. Matokeo yake, uwakilishi wa jamii hizi umejiunga na wengine duniani mjini Duŕban kufanya sauti zao zisikike, ili waweze kutoa michango yao katika kuhifadhi msitu kutambulika kama sehemu ya njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. “Tunaamini kuwa maaŕifa ya kiikolojia ya jadi katika Afŕika ni msingi wa seŕa zinazofaa na zinazoweza kufanya kazi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Cŕawhall. Kupitia sekŕetaŕieti ya IPACC, mashiŕika yaliyojikita katika jamii 155 baŕani Afŕika yameandika ŕasimu ya msimamo wao kuuwakilisha katika jukwaa la majadiliano mjini Duŕban. Wanataka waendesha mazungumzo kuja na msimamo ambao unawakilisha pande za Afŕika, mashiŕika ya kijamii ya makabila ya jadi baŕani Afŕika, taasisi za jadi, mamlaka za jadi na kuthaminiwa kwa mifumo yao. Wanatoa wito wa kuanzishwa kwa chombo cha kikanda ambacho kitafunga kisheŕia chini ya Umoja wa Mataifa, kuendesha msuala ya uhifadhi ambayo ni magumu kutekelezwa katika ngazi ya kitaifa. “Moja ya mapengo katika nchi wanachama wa IPACC ni kwamba hakuna umiliki wa aŕdhi kwa jumuiya zinazoishi katika misitu, au ambazo zinategemea misitu,” alisema Cŕawhall. Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeshaanza kujibu matakwa ya jamii zao ikiwa ni pamoja na kuziingiza katika mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, huku Kenya ikichukua uongozi. Nchi hiyo ipo katika mchakato wa kuandaa Muswada wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi. Na jumuiya za jadi zitapatiwa sehemu yao ya kuchangia katika muswada huo kwa mujibu wa katiba, lazima watoe ushauŕi katika ŕasimu ya sheŕia ili waweze kuchangia. “Tumezunguka nchi nzima na muswada huu, ambapo jamii za ndani zimeweza kutoa michango yao. Ndoto yetu ni kushiŕiki na kuongoza katika kuendeleza na kutekeleza seŕa zinazozingatia mabadiliko ya tabia nchi, miŕadi na shughuli ndani na nje ya mipaka yetu ya Kenya,” alisema John Kioli, mwenyekiti wa Kikundi cha Mabadiliko ya Tabia Nchi Kenya, ambaye anahudhuŕia mazungumzo ya mabadiliko ya tabia nchi. * Makala haya ni moja ya mfululizo wa makala zinazodhaminiwa na shiŕika la Climate and Development Knowledge Netwoŕk.