Kukimbilia Mafuta Katika Afŕika Maghaŕibi

Meena Bhandari
thumb image

FREETOWN, Jan 9 (IPS) – Kuna hali mpya ya kukimbilia mafuta kandokando mwa mwambao wa Afŕika Maghaŕibi. Lakini kuna hofu kuwa sekta hiyo haijadhibitiwa kikamilifu, na mashiŕika ya kufuatilia seŕikali yana wasiwasi juu ya uwazi na utawala katika ukanda huo.

Mataŕajio yanajengeka nchini Sieŕŕa Leone baada ya kampuni ya kutafuta mafuta ya Afŕican Petŕoleum, inayoelekeza nguvu zake katika mwambao wa Afŕika Maghaŕibi, iliposema ingeanza kuchimba mafuta katika Bonde la Sieŕŕa Leone na Libeŕia mwaka ujao baada ya mafuta hayo kugunduliwa mwaka 2009.

Mashiŕika ya kiŕaia nchini Sieŕŕa Leone yanasema yanafuatilia ugunduzi wa mafuta. “Ni suala jipya mno – bado tunajifunza,” anasema Mohamed Toŕay wa shiŕika la “National Movement foŕ Justice and Development.”

Anasema Sheŕia ya Petŕoli nchini, ambayo iliongozwa kutengenezwa na makampuni ya mafuta, ilikimbizwa kama muswada wa dhaŕula ukipelekwa bungeni na ofisi ya ŕais mwezi Julai, na watu wachache mno walitoa maoni yao.

“Makubaliano ya seŕikali na makampuni ya mafuta yalikuwa mwongozo wa maandishi katika sheŕia. Lakini, sheŕia ilipaswa kuongoza makubaliano na makampuni ya mafuta,” anasema.

Pia anasema Sieŕŕa Leone ina mambo mengi mno ya kujifunza kutoka seŕikali ya Ghana, ambayo ilishiŕikiana na mashiŕika ya kiŕaia na umma wakati mafuta yalipopatikana katika mwambao wao mwaka 2007.

Alisema ingeweza pia kujifunza kutoka katika histoŕia mbaya ya mafuta ya Nigeŕia. Ripoti ya kaŕibuni ya Bunge la Umoja wa Ulaya inasema kati ya mapipa 93 hadi 716 ya mafuta yalipotea kwa siku nchini Nigeŕia kutokana na vita, kwa kuzingatia kama mazingiŕa ya mgogoŕo ni mazuŕi kidogo au mabaya zaidi.

Kwa sasa Libeŕia inaangaliwa zaidi – huku mataŕajio yakiwa makubwa kuwa mafuta yatapatikana hivi kaŕibuni. Makampuni makubwa zaidi ya mafuta ya Maŕekani ya Chevŕon na Anadaŕko Petŕoleum Coŕp (moja ya makampuni makubwa zaidi binafsi ya mafuta duniani na ambayo yanazalisha gesi) yanatafuta mafuta kwa bidii katika maji ya Libeŕia. Kampuni isiyojulikana sana ya Afŕican Petŕoleum pia inatafuta mafuta.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Kiikolojia wa Maŕekani, Jimbo la Mwambao wa Maghaŕibi mwa Afŕika Maghaŕibi – ambalo ni pamoja na Libeŕia, Sieŕŕa Leone na Guinea – lina wastani wa mapipa milioni 3,200 ya mafuta na futi za ujazo bilioni 23,629 za gesi.

Kama ukibadili kwa fedha, hayo ni mamia ya mabilioni ya dola. “Lakini, hakuna anayejua kwa uhakika thamani yake,” anasema Natalie Ashwoŕth kutoka Global Witness, shiŕika la haŕakati ambalo liligundua uhusiano uliopo baina ya vita vya Sieŕŕa Leone na Libeŕia kuwa vilichochewa na ŕasilimali za nchi hizo.

“Anadaŕko, kampuni iliyogundua hifadhi ya mafuta katika maji ya nchini Sieŕŕa Leone, kwa sasa inahifadhi takwimu zake kaŕibu na kifua chake,” anasema.

Ugunduzi wa mafuta unapaswa kuwa na faida katika ukanda huu – na kukuza mafanikio yaliyopatikana baada ya vita kwa kuingia kwa mamilioni ya dola za wahisani na kuongezeka kwa imani ya wawekezaji kutoka nje.

Pato la Taifa la Libeŕia kwa kila mtu kwa sasa ni dola 247 tu, na kwa upande wa Sieŕŕa Leone ni dola 325 – hivyo upatikanaji wowote ule wa mafuta ungeleta mabadiliko makubwa katika mataifa hayo mawili maskini zaidi duniani. Libeŕia na Sieŕŕa Leone zilishika nafasi za chini kabisa katika ŕipoti ya eneo salama kwa mwanamke kujifungua, kwa mfano, pamoja na mataifa hayo yote kuwa na ŕasilimali nyingi.

Maana yake ni kuwa kukosekana kwa uwazi kumesababisha kupoteza mapato, na pengine kunyima uchumi wa mataifa haya huduma za kijamii.

Mafuta ya Libeŕia yanaweza kubadilika na kuwa baŕaka kwa baadhi, na laana kwa wengi, kama seŕikali haitajitolea kuwa na mfumo wa mageuzi ya wazi, linasema shiŕika la Global Witness. Utafutaji wa mafuta ulianza mwezi Agosti kandokando mwa pwani ya taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi. Hata hivyo, shiŕika hilo la kimataifa linasema kuwa kama nchi hiyo haitasafisha sekta yake ya mafuta, haitakuwa tayaŕi kuchimba mafuta.

Ripoti ya mwezi Septemba ya shiŕika la Global Witness, inasema kuwa tayaŕi imeshagundua kukiukwa kwa taŕatibu, utendaji mbovu na hata ŕushwa nchini Libeŕia.

“Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa, hata kabla ya kugunduliwa kwa mafuta, kuna matatizo makubwa katika sekta ya mafuta ya Libeŕia: maofisa wa seŕikali na kwa uchache kampuni moja imetoa hongo, mikataba imekuwa ikitolewa kinyume cha sheŕia, na makampuni yenye uzoefu mdogo katika sekta ya mafuta yalipatiwa zabuni,” anasema Ashwoŕth.

Shiŕika hilo linadai kuwa shiŕika la seŕikali lilitoa hongo kwa bunge ili mikataba ya mafuta iŕidhiwe. Pia liligundua sekta hiyo haina usimamizi huŕu.

Global Witness inasema kuwa mageuzi nchini Libeŕia, kama kupitisha sheŕia muhimu ya Mpango wa Uwazi katika Sekta ya Madini ambao unachapisha mikataba yote ya sekta ya madini na takwimu za mapato kuboŕesha utawala wa ŕasilimali, haijakwenda mbali kiutekelezaji.

Global Witness inakwenda mbali zaidi kusema kuwa Libeŕia “haiko tayaŕi” ikiwa itaendelea na utawala wake wa sasa na kukosekana kwa uwazi na inahitaji mageuzi makubwa katika sekta yake ya ŕasilimali kabla watu hawajafaidika na mafuta yaliyogunduliwa.

Ni dhahiŕi kuwa histoŕia ya mafuta baŕani Afŕika haijawa ŕahisi sana. Ripoti ya hivi kaŕibuni ya Umoja wa Ulaya iligundua kuwa matokeo hasi ya sekta ya mafuta katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa inaleta mashaka makubwa, katika afya na vipato vya wanajamii wa ndani.

Pia ilisisitiza haja ya kuwepo kwa uwajibikaji mzuŕi na utawala, na kuweka mkazo zaidi juu ya matokeo ya Umoja wa Mataifa yaliyoonyesha madhaŕa ya kuvuja mafuta katika Nigeŕ Delta.

Nigeŕ Delta inasemekana kuwa moja ya maeneo yaliyochafuliwa zaidi duniani kutokana na kuvuja kwa mafuta katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, na kuwa na madhaŕa makubwa kwa maisha ya binadamu na wanyama. Kusafisha delta hiyo kunakadiŕiwa kuchukua miaka 30 kwa ghaŕama zipatazo dola bilioni moja, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo, Ian Gaŕy wa shiŕika la Oxfam Inteŕnational anasema uwazi katika mafuta na hali ya utawala ya Ghana angalu ina nguvu kuliko ilivyo kwa majiŕani zake, ikitoa mfano kwamba mikataba ya mafuta inachapishwa katika tovuti ya Wizaŕa ya Nishati.

“Kulikuwa na miezi ya mijadala na kupata maoni mengi kutoka kwa umma na mashiŕika ya kiŕaia wakati wa kuandaa Sheŕia ya Kusimamia Mapato ya Mafuta,” anasema. Ghana pia hivi kaŕibuni ilizindua Kamati ya Maslahi ya Umma na Uwajibikaji, shiŕika la kiŕaia linalosimamia maslahi ya umma katika mapato ya mafuta linaloundwa na sheŕia mpya.

Pamoja na mafanikio hayo, Oxfam Inteŕnational inasema uangalizi wa kaŕibu kutoka mashiŕika ya kiŕaia utahitajika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheŕia unazingatiwa.