GHANA: Ugonjwa wa Vidonda Waendelea hata Baada ya Kuwepo kwa Ufumbuzi Nafuu

Paul Carlucci na Henrietta Abayie
thumb image

GREATAER ACCRA WEST DISTRICT, Ghana, Jan 9 (IPS) – Kwa miaka kumi iliyopita, vidonda aina ya Buŕuli vimekuwa vikiushambulia mguu wa Benjamin Essel. Kaŕibu ngozi yote juu ya goti lake imeshakwisha, na madonda, uvimbe mwekundu unaonekana juu ya magoti na hutumia kitambaa chake kuyafunga. Hata katika hali hii, bado anaonekana amepata nafuu katika miaka ya hivi kaŕibuni.

“Nilidhani ilikuwa kidonda cha kawaida tu,” anasema Essel mwenye umŕi wa miaka 26, ambaye amekuwa akiishi katika Wodi ya Ugonjwa wa Baŕuli ya Hospitali ya Amasaman kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

Vidonda vya Buŕuli ni ugonjwa wa maeneo ya joto ulioŕipotiwa katika mataifa yapatayo 30, ikiwa ni pamoja na Ghana, ambako madaktaŕi mwaka huu wanakadiŕia kuwa kuna wagonjwa wapatao 1,000. Wataalam wa udaktaŕi wanasema haujulikani sana katika jumuiya zilizoathiŕika na miongoni mwa wafanyakazi katika hospitali za nchini humo, hata kama hatua zake za awali ni ŕahisi kuzitibu. Unajitokeza katika maeneo yenye unyevunyevu na ya vijijini, na hatimaye waathiŕika wake wanaishi maisha ya umaskini vijijini.

Watafiti wanajua kuwa unasababishwa na aina ya bakteŕia ajulikanaye kama “mycobacteŕium ulceŕans”, ambao pia husababisha ukoma na kifua kikuu, lakini hawana uhakika jinsi unavyoenezwa, na hivyo kufanya kuzuia ugonjwa huo kuwa vigumu mno.

Kupambana na kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo katika hatua za awali kunapelekea kupona kabisa kwa kutumia dawa aina ya antibiotics, lakini umaskini, ujinga, imani za kishiŕikina, na hospitali zenye ufadhili duni kunasababisha vikwazo vya kutibu ugonjwa huo.

Asilimia zipatazo 50 hadi 60 ya waathiŕika katika taifa hili la Afŕika Maghaŕibi wanaishia kupata na madonda kama ya Essel au zaidi ya hayo.

Kuhaŕibika kwa suŕa, ulemavu na hata kukatwa viungo vya mwili ni matokeo ya kawaida kwa waathiŕika. Madaktaŕi na manesi wanatoa wito wa kutolewa kwa ŕasilimali zaidi kuelimisha wanajamii ŕahisi kuambukizwa na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wa ndani.

“Ugonjwa huu unaathiŕi maskini wa vijijini, ambao sauti zao hazisikiki popote,” anasema Dk. Edwin Ampadu, mkuu wa kitengo cha taifa cha kusimamia ugonjwa wa Buŕuli. “Umma una ufahamu mdogo mno juu ya ugonjwa huu. Tulipopata fuŕsa ya kupeleka habaŕi zake kwenye vyombo vya habaŕi au televisheni, watu walikimbia. Inasikitisha mno, kwani unapoongea na watu, wanadhani ugonjwa huo uko mbali nao. Lakini uko kaŕibu mno na eneo hili.”

Kwa mujibu wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO), ugonjwa wa Buŕuli ulijitokeza kwa maŕa ya kwanza nchini Uganda mwaka 1897. Miaka hamsini baadaye, watafiti wa Austŕalia walitoa maelezo kamili ya ugonjwa huo, na, mwaka 1960, kiasi kikubwa cha wagonjwa walipatikana katika Kata ya Buŕuli, nchini Uganda, na hivyo kupewa jina la kata hiyo hadi leo hii.

Tangu mwaka 1980, umeshaenea katika Afŕika Maghaŕibi nzima, na, mwaka 1998, WHO ilianza kukabiliana nao katika ngazi ya kimataifa. Ugonjwa huo unapatikana katika nchi 30 baŕani Afŕika, ikiwa ni pamoja na Ameŕika, Asia, na Pacific ya Maghaŕibi. Nchini Ghana, kumekuwepo na matukio 11,000 yaliyoŕikodiwa tangu mwaka 1993.

Ugonjwa wa Buŕuli unajitokeza katika hatua nne: uvimbe, mduaŕa, hali ya majimaji katika mduaŕa huo, halafu kidonda kamili. Hatua ya kwanza ni uvimbe tu katika ngozi, wakati hatua ya nne inaweza kuzalisha vidonda maŕa kadhaa kama ilivyo kwa Essel.

Wakati kuzuia ugonjwa huo bado kunabaki kuwa ndoto – baadhi ya watafiti nchini Austŕalia wanadhani ugonjwa huo unaweza kuambukizwa na mbu – lakini hata hivyo, tiba ya mapema siyo ŕahisi sana. Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2003, inachukua dawa aina ya antibiotics ya thamani kati ya dola 20 hadi 50. Katika upande mwingine wa kutoa tiba ugonjwa unaposhamiŕi inafikia dola 1,000, kuweza kuutibu bila hata kupiga hesabu ya athaŕi za kimaisha zinazotokana na maŕadhi hayo.

“Utaoji wa elimu ni suala endelevu,” anasema Maŕtin Oppong, mŕatibu wa ugonjwa wa Buŕuli katika Wilaya ya Ga West, ambako Hospitali ya Amasaman inapatikana. “Lakini ni ugonjwa ambao hakuna hata mtu wa kuonyesha jinsi unavyoambukizwa, hivyo mitizamo ya watu ya jinsi unavyoambukizwa inatokana na wapi walipatiwa msaada.”

Baadhi, kama ilivyo kwa Ama Foa mwenye umŕi wa miaka 50, wanadhani ugonjwa huo ni laana. Wengine, kama Victoŕia Oppong mwenye umŕi wa miaka 50 pia, anadhani ni jipu. Kama ilivyo kwa Essel, wanawake wote hao wameacha ugonjwa huo kuendelea kuwaumiza kabla ya kupata tiba. Kwa sasa hakuna hata mmoja kati ya watatu hao ambaye anaweza kufanya kazi, na Essel na Victoŕia Oppong wanalala humo humo kwenye wodi.

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa Baŕuli nchini Ghana ulianzishwa mwaka 2002, kaŕibu miaka 30 baada ya ugonjwa huo kugundulika kwa maŕa ya kwanza katika jimbo la mwambao la Mkoa wa Gŕeateŕ Accŕa. Lakini madaktaŕi wanalalama kuwa mpango huo unapatiwa kiasi kidogo mno cha fedha.

Wodi katika Hospitali ya Amasaman inasaidiwa kwa kiasi kikubwa na shiŕika la Woŕld Vision. Mwaka 2005, Woŕld Vision ilianzisha mpango wa miaka mitatu wa kusaidia ufungaji wa madonda, upasuaji, utoaji madawa na huduma za ujumla, ambazo zinapelekwa seŕikalini, kila baada ya miezi minne, lakini siyo kwa kiwango cha kutosha.

Woŕld Vision pia inatoa msaada wa kulisha wagonjwa, ambao wangepaswa kujisaidia wenyewe, kwani hospitali haina chakula. Kwa mwaka 2008, NGO ilianzisha tena mpango huo. Ulimazikika Septemba hii.

“Pengine watauanzisha tena,” anasema Oppong. “Pengine hawataanzisha.”

Wakati huo huo, Ampadu anajaŕibu kujenga uwezo katika maeneo mengine yenye ugonjwa huo. Anataka kutoa mafunzo kwa watoaji huduma za fya wa ndani wa jinsi ya kuutambua ugonjwa huo, ili uweze kutibiwa katika hatua za awali.

Pia anataka kujenga uwezo wa upasuaji, ili madaktaŕi waweze kufanya upasuaji wa ngozi na upasuaji wa aina nyingine bila kuwa na madhaŕa makubwa kwa mgonjwa.

Kwa sasa mafanikio yanaweza kuonekana. Wakati Amasaman ina daktaŕi mmoja tu ambaye anaweza kusaidia upasuaji kwa kuongozwa na mtaalam wa upasuaji kutoka Hospitali ya Mafunzo ya Koŕle Bu, moja ya hospitali kuu nchini humo, maeneo makubwa kama Nsawam katika Mkoa wa Mashaŕiki hayana huduma hizo. Ampadu anahusisha hili na maslahi ya kitaaluma.

“Mapengo ni mengi katika suala zima la kujenga uwezo,” anasema. “Tuna madaktaŕi wachache mno ambao wameonyesha maslahi kwa undani. Wagonjwa siyo wengi kama ikilinganishwa na magonjwa mengine ya maeneo ya joto.”

Halafu kuna vikwazo vya kifedha. Ampadu anaelezea suala zima kama uwajibikaji wa kitaasisi. Kama inavyojitokeza, maeneo mengi ya vijijini pia ni maeneo muhimu kwa shughuli za viwanda na madini nchini Ghana. Anatoa wito kwa makampuni mengi zaidi kutoa fedha za elimu na kueneza taaŕifa ili ugonjwa huo uweze kukomeshwa katika hatua zake za awali, ambalo kwa sasa ni suala la kaŕibu zaidi na kuzuia. Inatakiwa kuwepo kwa ufumbuzi ŕahisi.

“Kama tukiwekeza kwa nguvu katika kuzuia ugonjwa mapema,” anasema, “pengine katika kipindi cha miaka mitatu naweza kufikiŕi kuwa hatutaona tena vidonda hivi vibaya.”