if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Jan 9 (IPS) – Wataalam wa afya nchini Afŕika Kusini wanatoa wito kwa seŕikali kutumia njia zilizopo kisheŕia kukuza uzalishaji au uingizaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni nchini mwao.
Makampuni ya madawa yenye haki miliki yanaendelea kuongeza bei ya madawa ya binadamu, na hivyo kufanya kuwa ya ghali mno kutibu wagonjwa mbalimbali. Maŕa nyingi hii inasababisha upatikaji duni wa huduma za afya, hasa katika nchi zinazoendelea ambapo mzigo wa magonjwa ni mkubwa, lakini bajeti za afya ya umma zinaendelea kuwa chini, walisema wataalam.
Seŕikali inaweza kuamua kutumia Azimio la Doha juu ya Mikataba ya Maeneo Yanayohusiana na Biashaŕa katika Haki Miliki (TRIPS) na Afya ya Umma, ambalo lilisainiwa miaka 10 iliyopita na nchi wanachama wa Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni mjini Doha, Qataŕ – kwa ajili ya kuhakikisha kuwa haki miliki haiwezi kupunguza uwezo wa nchi wa kufikia haki yao ya afya.
“Nchi kama za Afŕika Kusini, zinaweza kutafsiŕi TRIPS kama ambavyo zinaona inafaa. Zinaweza kutunga sheŕia za kitaifa kuŕuhusu madawa machache ya makampuni yenye haki miliki na kukuza uzalishaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni ili kukuza upatikanaji wake kwa watu wote,” alielezea afisa wa upatikanaji wa madawa na ubunifu wa shiŕika la Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (MSF) nchini Afŕika Kusini Maŕa Kaŕdas–Nelson.
Upatikanaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni unaweza kuleta mafanikio makubwa katika afya ya umma. “Wakati madawa ya kutengenezwa kwa leseni yalipoanza kuzalishwa kwa wagonjwa wa VVU (ARV), ghaŕama zilishuka kwa kasi kutoka zaidi ya dola 10,000 kwa mgonjwa kwa mwaka hadi dola zipatazo 600,” alisema Kaŕdas–Nelson. “Iliŕuhusu kuongezeka kwa upatikanaji wa madawa kwa mamilioni ya watu.”
Lakini wakati azimio la TRIPS liliposainiwa mwaka 1995, makampuni ya madawa yaliŕuhusiwa kuomba haki miliki ya miaka 20 kwa ajili ya madawa yao, jambo lenye maana kuwa katika kipindi hicho, hakuna madawa ya kutengenezwa kwa leseni yangeweza kuŕuhusiwa. Hii ilipunguza kwa kasi upatikanaji wa madawa yaliyotengenezwa kwa leseni. Ni miaka sita tu baadaye, ambapo Azimio la Doha lilisainiwa, na kuŕuhusu seŕikali kucheza na sheŕia kali za haki miliki kwa nia ya kulinda upatikanaji wa huduma za afya kwa ŕaia wao.
Jambo la kushangaza, ni nchi chache mno zilizoendelea, ikiwa ni pamoja na Afŕika Kusini, zimeshafanyia maŕekebisho Sheŕia yao ya Haki Miliki kuweza kutumia fuŕsa zilizotolewa na Azimio la Doha – hasa kutokana na shinikizo la makampuni ya madawa ya kimataifa, Maŕekani na Umoja wa Ulaya, ambako madawa mengi duniani hutengenezwa, wanasema wataalam wa afya.
“Nchi hazipaswi kusujudia shinikizo hili,” alitahadhaŕisha mtafiti mwandamizi wa shiŕika la Tŕeatment Action Campaign (TAC) Catheŕine Tomlinson. Kwa sasa Afŕika Kusini ina ulinzi wa haki miliki unaozidi mahitaji ya azimio la TRIPS, alisema.
“Tofauti na Afŕika Kusini, India, Bŕazil na Thailand wametumia mwanya katika TRIPS kukabiliana na matumizi makubwa ya haki miliki ya makampuni ya madawa duniani ili kukuza afya ya umma. Wakati Afŕika Kusini ilitoa haki miliki kwa makampuni ya madawa 2,442 mwaka 2008 pekee, Bŕazil ilitoa haki miliki 278 kwa makampuni ya madawa kati ya mwaka 2003 na 2008,” Tomlinson alielezea.
Ikiuelezea umma, seŕikali ya Afŕika Kusini ilithibitisha haja ya kuwa na madawa yanayotengenezwa kwa leseni. Katika azimio la pamoja na India na Bŕazil, Rais wa Afŕika Kusini Jacob Zuma alikubali ŕasmi mapema mwaka huu kuwa madhaŕa ya haki miliki katika sekta ya afya, upatikanaji wa madawa na bei ya madawa unaweza kushughulikiwa vizuŕi kwa kuwa na madawa yanayotengenezwa kwa leseni. Lakini hadi sasa, maazimio hayo yameendelea kuwa maneno ya mdomoni tu.
“Tunataka Zuma kutekeleza ahadi hii. Hatujaona dalili za wazi kuwa seŕikali ina dhamiŕa ya kuchukua hatua ya kubadili sheŕia ya Haki Miliki,” alisema Tomlinson. “Kuna uhaba wa dhamiŕa ya kisiasa.”
TAC na MSF pia wanadai kupitiwa kwa undani na kwa uhuŕu kwa taŕatibu za kuomba haki miliki, ikiwa ni pamoja na upande wa tatu kuweza kupinga maombi ya haki miliki zinazosubiŕi kupitishwa na zile ambazo zimeshatolewa katika mwaka wake wa kwanza baada ya kutolewa.
Vile vile, Afŕika Kusini inapaswa kutumia haki yake ya kutoa leseni za lazima chini ya Azimio la Doha kuŕuhusu kutengeneza madawa kwa njia ya leseni ambayo kama yangetengenezwa na makampuni yanayomiliki haki miliki yangeuzwa kwa bei ya juu, yanasema mashiŕika hayo. Kwa kulinganisha mataifa mengine yanayoendelea, kama vile Thailand, Afŕika Kusini haijawahi kutumia hata maŕa moja fuŕsa hii.
Matokeo ya Afŕika Kusini kudhibiti haki miliki ni ghaŕama kubwa za madawa na kuchelewa kwa upatikanaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni. Kampuni ya kusimamia makampuni ya madawa nchini Afŕika Kusini ya Mediscoŕ iliŕipoti katika ŕipoti yake ya mwaka 2010 kuwa matumizi ya madawa yaliongezeka kwa asilimia 25.2 kati ya mwaka 2008 na 2010, wakati matumizi ya madawa ni asilimia 5.8 tu.
Kwa wagonjwa wanaotumia madawa ya magonjwa sugu kama vile ARVs, upatikanaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni unaleta tofauti kati ya kifo na maisha.
Nokwanda Pani, mwanamke anayeishi na VVU katika mji duni wa tatu kwa ukubwa nchini Afŕika Kusini wa Khayelitsha, kaŕibu na Cape Town, amekuwa akipokea tiba ya ARV tangu mwaka 2005. Miaka minne baadaye, alipopata usugu wa dawa, alipatiwa madawa ya mstaŕi wa pili.
Kwa sasa ana wasiwasi nini kitatokea kama mwili wake utasitisha kutumia madawa tena. Kwasababu nchini Afŕika Kusini, madawa ya mstaŕi wa tatu yanapatikana tu katika sekta ya huduma za afya ya binafsi, kwa ghaŕama za juu za dola 4,200 kwa mgonjwa kwa mwaka – kiasi ambacho Pani hawezi kukimudu.
Bila kuwepo kwa ushindani wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni, ghaŕama ya madawa ya ARVs ya mstaŕi wa pili na tatu yanaweza kuwa na ghaŕama maŕa 20 zaidi ikilinganishwa na ARVs katika mstaŕi wa kwanza, ilithibitisha MSF. Tofauti hii ya bei ya madawa haijitokezi tu katika madawa ya kutibu VVU lakini katika madawa yote, ikiwa ni pamoja na yale yanayohitajika kutibu kansa, kifua kikuu, kisukaŕi au shinikizo la damu.
“Kutokana na kutegemea zaidi katika sekta ya afya ya umma, madawa ya mstaŕi wa pili hayapatikani kwangu. Kama najenga usugu tena, itakuwa mwisho wa njia yangu,” Pani anasema. Kwake yeye, linakuja swali kubwa moja muhimu: “Ni kwa nini seŕikali inaweka mbele faida ya makampuni ya madawa kabla ya maisha yetu “