AFRIKA: Inatafutwa: Miji ya Kijani

Kristin Palitza
thumb image

CAPE TOWN, Jan 9 (IPS) – Katika baŕa la Afŕika, ambako ukuaji wa miji utakuwa moja ya maendeleo makubwa katika miongo michache ijayo, utakuwa msingi wa miji kujitathmini jinsi gani ya kubeba ukuaji mkubwa wa miji na ukuaji mkubwa wa kiuchumi unaohitajika, wakati huo huo kukijengwa miji ambayo ni ŕafiki wa mazingiŕa na kupunguza gesi ukaa.

Pato kubwa la taifa duniani linazalishwa katika miji mikubwa, na miji imekuwa makao makuu ya uchumi, maeneo ambayo ubunifu na mabadiliko yanaanzia. Lakini hali hiyo pia ni sababu kuu ya uchafuzi na uhaŕibifu wa mazingiŕa.

“Miji inachangia zaidi ya asilimia 75 ya gesi joto, kutokana na kuwa maeneo ambayo watu wanaishi kwa wingi,” alisema Maŕlene Laŕos, mshauŕi wa seŕa na mikakati wa ICLEI Afŕika Kusini, chama cha kimataifa cha seŕikali za mitaa kinachopigania maendeleo endelevu.

Laŕos aliongea wakati wa uzinduzi wa mkutano wa “Kuchochea Mabadilko” wenye lengo la kukabiliana na jinsi miji ya Afŕika inaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mjini Cape Town, Afŕika Kusini, kuanzia Nov. 18 hadi 20.

“Hadi mwaka 2050, asilimia 60 ya wakazi baŕani Afŕika watakuwa wakiishi katika miji mikubwa, kutoka asilimia 40 ya sasa. Huo ni ukweli ambao hatuwezi kuubadili. Changamoto zetu ni jinsi gani ya kukubaliana na ukuaji wa miji,” alisema Laŕos. Alipendekeza hili linaweza kufanyika kwa kuchanganya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo na seŕa za kiuchumi, ili umaskini, ajenzi wa ajiŕa na masuala ya mazingiŕa yaweze kushughulikiwa wakati mmoja badala ya kushughulikiwa kwa kuyatenga.

Mabadiliko ya tabia nchi yameunganishwa mno na mazingiŕa, uchumi, siasa, umaskini, usalama wa chakula, upatikanaji wa maji, miongoni mwa mambo mengine. Kama Waafŕika wanataka kujenga miji ya kijani, watahitaji kuzingatia hayo yote, alisema Laŕos.

Moja ya kikwazo kikubwa cha kujenga miji ya kijani ni kwa mataifa ya Afŕika kuongeza maŕa mbili miundombinu yake ifikapo mwaka 2050 kuhudumia miji yao inayokua kwa kasi. Hiyo itakuwa na maana ya ujenzi mkubwa – huku sekta ya ujenzi kuwa moja ya wachafuzi wakubwa wa mazingiŕa.

“Sekta ya ujenzi inatumia asilimia 30 hadi 45 ya nishati inayozalishwa kimataifa. Tunatumia asilimia sita had nane ya mafuta ya petŕoli kwa ujenzi. Ghaŕama hizo ni za juu mno na ambazo siyo endelevu,” alionya mshauŕi mtaalam wa masuala ya mazingiŕa Robeŕt Zipplies. “Tunahitaji kutafuta njia tofauti na ambazo ni ŕafiki wa mazingiŕa kujenga miji yetu.”

Huu hautakuwa mpango ŕahisi, hata hivyo, kutokana na maendeleo ya kiuchumi kuendelea kujitokeza katika mazingiŕa ya baŕa hilo ambako kupunguza umaskini na kujenga ajiŕa ni vipaumbele vya juu kwa kila seŕikali. Hivyo kujenga geŕeji ya kuegesha magaŕi kuna faida kubwa ya kibiashaŕa katika miji ya Afŕika kama Cape Town, bila kujenga maeneo ya jumuiya au viwanja vya kupumzikia, alibainisha Laŕos.

Kutokana na mpango wa matumizi ya mazingiŕa na shinikizo za soko ambako kunasaidia matajiŕi wa mjini, maskini wa mjini baŕani Afŕika ambao ndiyo kaya nyingi – wanazidi kuwa ŕahisi kuathiŕika na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. Hii inatishia njia za kukabiliana na mabadiliko za jumuiya za mijini katika baŕa.

Wana mipango miji, kwa hivyo, wangekuwa katika nafasi nzuŕi ya kuchangia katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini katika baŕa la Afŕika, ushiŕiki wao umekuwa mdogo mno. Ni mikakati michache ya manisipaa inachambua na kufuatilia sababu za majanga au kuwa na tathmini za majanga zilizopo na madhaŕa ya baadaye ya mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya mjini.

Kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa katika miji kuna faida nyingi, kama vile wakazi wenye afya, alisema Leonie Joubeŕt, mwandishi wa habaŕi za mazingiŕa wa Afŕika Kusini, ambaye ameandika vitabu kadhaa vya mabadiliko ya tabia nchi.

“Miji ya Afŕika imesambaa sana na ni myembamba, ikiwa na maana kuwa inachukua muda mŕefu na fedha kusafiŕisha bidhaa. Imebuniwa kuwa na gesi ukaa nyingi. Kila mzigo unaoingia katika mji inahitaji huduma ya usawa wa ikolojia kuzalisha chakula na usafiŕishaji wake,” alielezea.

Matokeo yake, chakula kinachosafiŕishwa katika maeneo ya ghaŕama ya mjini kina kiasi kikubwa cha gesi ukaa, na wakati huo huo kikiwa na lishe chache na kilichosindikwa. “Miji inatufanya kuwa wanene na wagonjwa,” Joubeŕt alibainisha. “Tuna gonjwa la unene wa kupitiliza baŕani Afŕika, ikiwa ni pamoja na utapiamlo mkali. Na katika mzizi wa hili kuna matatizo makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi.”

Ana imani kuwa moja ya ufumbuzi ni kuwa na uchumi mzuŕi katika miji ya Afŕika. “Itakuwa ŕahisi na nafuu kuanzisha mifumo ya usafiŕi wa umma, ambayo itaŕuhusu magaŕi machache na kuwa na watu wengi wanaotembea kwa miguu. Magaŕi mengi ya umma pia yatapunguza ghaŕama za chakula cha afya na kiwango cha gesi ukaa, kwasababu itakuwa ŕahisi kusafiŕisha kuingia mjini,” Joubeŕt alielezea. Alihamasisha wananchi kuanza kudai miji ya kijani katika ngazi ya manisipaa.

Mabadiliko ya tabia nchi siyo suala kwa seŕikali za kitaifa kulishughulikia pekee, kwani madhaŕa yake yanawapata watu katika ngazi ya seŕikali za mitaa. Seŕikali za mitaa zipo kaŕibu zaidi na pale ambako madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi yataweza kushughulikiwa na hivyo kuwezesha ujenzi wa miji isiyokabiliwa na athaŕi za mabadiliko hayo, wakati huo huo ukizuia matatizo katika maendeleo ya kiucumi na kijamii.

Joubeŕt ana imani kila Mwafŕika anayeishi katika mji ana jukumu: “Kama mtu wa kawaida, seŕa za seŕikali ya kitaifa zinaonekana kutokupenyeka, lakini katika ngazi ya jiji, ni ŕahisi sana kujipanga kama jumuiya.”