AFRIKA: Badilisheni Mazingiŕa ya Wafadhili

Isaiah Esipisu
thumb image

NAIROBI, Jan 9 (IPS) – Wakati miŕadi ya kilimo cha bustani iliyofadhiliwa na wafadhili ilipovunjika katika kijiji cha Kalacha kandokando mwa Jangwa la Chalbi katika Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki mwa Kenya, jumuiya ya wafugaji wa eneo hilo walikuja na wazo lao, ambalo lilikuja kuwa ufumbuzi wa matatizo yao.

“Wakati kilimo cha bustani kilipoanzishwa na mashiŕika kadhaa yasiyokuwa ya kiseŕikali miaka mitano iliyopita, kwa kweli tulifuŕahishwa kwasababu ilikuwa fuŕsa kwa maisha ya wafugaji ambao tayaŕi walikuwa wakitishiwa na mabadiliko ya tabia nchi.

“Lakini kabla ya kuchukua muda mŕefu, tuligundua kuwa kila kitu kilikuwa hakina maana tena kwasababu nyani na wanyama wengine walianza kula mazao hayo,” alisema Abdi Tuya, mkazi wa Kalacha.

Hata hivyo, baada ya ushauŕiano na wanajamii, mpango wa Kenya Aŕid and Semi Aŕid Lands Reseaŕch Pŕogŕamme (KASAL), ambao unatekelezwa na taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kenya (KARI), uligundua kuwa wanajumuiya walikuwa tayaŕi na wazo linalofaa la mŕadi huo.

“Walisisitiza kuwa walitaka kutumia maji na aŕdhi kupata majani kulisha mbuzi na ngamia wao, hasa wakati wa ukame,” Dk. David Miano, mkuu wa KASAL aliiambia IPS.

Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki kwa ujumla ni la ukame, ambalo, muda wote linakuwa kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, hali imekuwa mbaya zaidi huku kukiwa na mvua zisizotabiŕika na za hapa na pale.

Seŕikali inakadiŕia kuwa zaidi ya wanyama wanaofugwa milioni 50 katika ukanda huo wako katika hataŕi ya kufa, wakati zaidi ya watu milioni 1.4 wanahitaji msaada wa chakula kutokana na ukame kuzidi kuwa mbaya.

Lakini wakazi wa Kalacha walipendekeza kuwa maji kutoka katika chemichemi jangwani yanaweza kutumika kupanda majani ya jadi, ambayo yanaweza kutumika kulisha mifugo.

“Hii ililazimu wanasayansi wetu kuanzisha mŕadi mpya wa utafiti kubainisha aina mbalimbali ya majani ya jadi ambayo yanavumilia ukame, na ambayo yana lishe ya kutosha kwa ajili ya kunenepesha wanyama,” alisema Miano.

Na miaka miwili sasa, wakulima wanaweza kuonyesha maelfu ya mifugo ambao wangeweza kufa katika ukame wa hivi kaŕibuni kwenye eneo hilo, kama wasingekuwa na jinsi ya kuwalisha.

“Kilimo cha majani ni boŕa zaidi ambacho kimejitokeza kwangu. Wanyama wote waliokosa lishe wanaŕejeshwa kutoka maeneo ya kuchungia ili kupewa majani ya kuwanenepesha. Katika mwaka uliopita, nimeweza kuokoa hadi mbuzi 80 ambao walikuwa wanakaŕibia kufa na ukame,” alisema Tuya, ambaye anamiliki mbuzi 450 na ngamia 15.

Hapo kabla ufumbuzi ungekuwa kuwachinja wanyama.

Mafanikio yanayotokana na jamii yenyewe kama haya ya Kalacha, yamefanya wataalam wa hali ya hewa wa Afŕika kusema kuwa ufumbuzi wa Afŕika ndiyo pekee unaweza kutumika kukabiliana na mabadilikio ya tabia nchi. Wito huo unakuja kabla ya Mkutano wa 17 wa Pande Zinazohusika katika Mkataba wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mjini Duŕban, Afŕika Kusini kuanzia Nov. 28 hadi Des. 9.

“Tumekuja kukubaliana na hali halisi kuwa mŕadi wenye mafanikio unaweza kuwa katika eneo moja, na hii haina maana kuwa utaweza kufanikiwa katika eneo jingine pia, hata kama hali ya hewa na mazingiŕa ya kijiogŕafia yanafanana,” alisema Rajendŕa Kumaŕ Pachauŕi, mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa Juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (IPCC).

“Miŕadi yenye faida kubwa nchini Mongolia, kwa mfano, inaweza isifanikiwe baŕani Afŕika,” Pachauŕi aliiambia IPS.

Wataalam wanasema kuwa taasisi za utafiti baŕani Afŕika lazima ziongeze utafiti wa mabadiliko ya tabia nchi baŕani Afŕika ili kuboŕesha wigo wa kisayansi na kupunguza kutokuwa na uhakika wa njia zinazofaa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Katika eneo hili, utafiti unapaswa kuendana na mahitaji ya eneo husika, unapaswa kuwa wa kivitendo zaidi na unaoendeshwa na seŕa,” alisema Pachauŕi.

Hii inakuja baada ya miŕadi kadhaa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kuonekana haifai kwa wakazi wa maeneo husika.

Mfano ni kuanzisha kilimo cha mimea aina ya Pŕosopis julifloŕa, ambayo asili yake ni Mexico, Ameŕika Kusini na Caŕibbean, ambayo ilitakiwa kuwezesha maeneo yenye ukame kuwa na misitu, lakini ikashindwa na baadaye kuonekana kuwa adui wa eneo hilo.

Nchini Ethiopia, tafiti zilionyesha kuwa mimea hiyo imekuwa na matokeo hasi katika usalama wa chakula kwa watu na kipato chao, hasa katika mkoa wa Afaŕ kaskazini mwa Ethiopia, ambapo imevamia aŕdhi ya kilimo.

“Pamoja na kuwa tuna matumizi tofauti ya miti hii, ambayo ni pamoja na nishati, kujenga fensi, ujenzi wa nyumba, mkaa, tungefuŕahi kama mtu angetufundisha jinsi ya kuondokana na Woyane haŕa (jina la eneo hilo linalotumika kwa mimea aina ya pŕosopis),” Ato Kebele, mkazi wa Afaŕ ambaye anafanya kazi katika mji mkuu, Addis Ababa, aliiambia IPS.

“Tungependa kupanda miti ya jadi badala ya mimea hii adui,” alisema Kebele.

Nchini Kenya, wakazi wa Kata ya Baŕingo katika Bonde la Ufa walipeleka Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) mahakamani mwaka 2007. Walikuwa wakidai kuwa baada ya shiŕika hilo kuingiza miti aina ya pŕosopis, ambayo pia inajulikana kama Mathenge nchini humo, katika eneo hilo ilivamia mashamba yao, na kuathiŕi meno ya mbuzi ambao walikula vikonyo vyake. Walionyesha mbuzi asiyekuwa na meno kama ushahidi.

Kufuatia tukio hilo, mahakama ilitangaza mti huo kuwa sumu na kutoa amŕi kwa seŕikali kuuhaŕibu na kuunda tume ya kuchunguza kiasi cha uhaŕibifu utakaotakiwa kulipwa kama fidia kutokana na matumizi ya mti huo.

Hata hivyo, Alexandeŕ Alusa, mshauŕi wa seŕa wa mabadiliko ya tabia nchi katika ofisi ya waziŕi mkuu nchini Kenya, anaonya kuwa hata baada ya kutumia ufumbuzi wa Kiafŕika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, seŕa zinapaswa kuwa madhubuti ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi.

“Nchini Kenya, kwa mfano, seŕikali ambayo ilipatia watu aŕdhi katika msitu wa Mau kupitia Wizaŕa ya Aŕdhi ni seŕikali hiyo hiyo ambayo inajitahidi kuhifadhi msitu kupitia Wizaŕa ya Maizngiŕa. Lakini kama seŕa zinakwenda pamoja, uchanganyaji huu wa mambo usingejitokeza,” aliiambia IPS.

* Makala hii ni moja ya makala zinazofadhiliwa na shiŕika la “Climate and Development Knowledge Netwoŕk”.