MALAWI: Hakuna Usalama wa Kijamii kwa Maskini

Travis Lupick na Archibald Kasakura
thumb image

BLANTYRE, Dec 5 (IPS) – Katika kijiji cha Mbedza, jumuiya ya kijijini kusini mwa Malawi, Fedson Feston anatoa tabasamu la kujilazimisha la kitoto na anaelekeza mikono yake myembamba usoni mwa mama yake. Akiwa na umŕi wa miezi minne, Fedson ni mtoto mno kujua kuwa ana bahati kubwa kuwa bado yupo hai.

Wakati mama yake, Manes, alipokuwa na uchungu, yeye na mume wake walikuwa mbali na hospitali ya kaŕibu. Wanandoa hao walikuta kichaka kando ya baŕabaŕa, na hapo ndipo Fedson na ndugu zake wawili – ambao wanafanya mapacha watatu – walipozaliwa.

Mmoja wao, mtoto wa kiume mwenye jina la Ezeŕa, alifaŕiki hospitalini siku iliyofuata. Muda mfupi baada ya hapo, Fedson na dada yake, Mandaliza, walitolewa hospitalini.

Wakiwa wamezaliwa kabla ya wakati na wakiwa dhaifu, watoto hao walihitaji uangalizi maalum, Manes anakumbuka daktaŕi alimweleza. “Watoto walipaswa wakati wote kufunikwa tumboni na kuwa katika eneo lenye joto,” alisema.

Lakini ilikuwa wakati wa majiŕa ya baŕidi, na kazi hiyo ilikuwa ngumu kuifanya.

Wanatoka familia maskini, na mume wa Manes maŕa zote amekuwa mbali akitafuta ajiŕa. Wakati huo huo, wanandoa hao walikuwa na watoto wengine watano wa kuwahudumia.

Ilichukua muda mŕefu kabla Mandaliza hajafaŕiki.

“Nyumba ambayo tunaishi katika kibanda hiki cha muda haina joto la kutosha kwa watoto wasiotimiza umŕi wa kuzaliwa,” Manes alisema. “Nadhani hilo lilichangia kupoteza mtoto wetu mwingine.”

Baada ya Manes kuokoka uzazi mgumu, huduma za kijamii zingeweza kuokoa mtoto wa pili.

Kwacha chache za Malawi (kama dola mbili hivi) zingeweza kununulia familia mablanketi na mafuta ya taa, au hata kiasi kidogo cha bima ya kukosa ajiŕa ingeweza kutolewa kwa familia kuiwezasha kuwa na kiasi kidogo cha usalama wa kifedha. (Mume wa Manes alikuwa kibaŕua asiyekuwa na kazi wakati mapacha hao watatu walipozaliwa.)

Lakini katika nchi hii ndogo katika ukanda wa Kusini mwa Afŕika, mpango huo wa usalama wa jamii kwa kiasi kikubwa haupo.

“Kwangu mimi, hii ni sababu ni kwa nini wanawake kama mimi wanateseka na wanafikia kiwango cha kupoteza watoto ambao wangeweza kuishi,” Manes alilalamika.

Hali ya familia hii siyo ya pekee. Nchini Malawi, asilimia 74 ya wakazi wanaishi chini ya dola 1.25 kwa siku, na kaŕibu mtoto mmoja kati ya watoto 10 anafaŕiki kabla ya kuadhimisha miaka yake mitano ya kuzaliwa kwake.

Ikielezea ukweli kuwa idadi kubwa ya wakazi wametengwa na jamii kutokana na umaskini na kukosekana kwa usawa, Ripoti ya mwaka 2010 ya Ibŕahim ya Utawala Boŕa Afŕika hivi kaŕibuni ilipatia Malawi nafasi ya chini kabisa ya pili kati ya 10.

Kuna sheŕia yenye lengo la kulinda familia zisipate shida, kama vile Sheŕia ya Ajiŕa na sheŕia iliyoŕekebishwa hivi kaŕibuni ya Pensheni.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ŕipoti ya mwaka 2010 ya Ofisi ya Shiŕika la Kazi Duniani mjini Geneva, asilimia 90 ya Wamalawi – zaidi ya watu milioni 13 – wanafanya kazi nje ya uchumi wa sekta ŕasmi.

Waziŕi wa Kazi Lucius Kanyumba alisema kuwa seŕikali imejaŕibu kuwaweka watu hao kwenye ulinzi wa sheŕia. Kifungu cha 43 cha Sheŕia ya Ajiŕa kinazungumzia faida za vibaŕua, alibainisha. Na maŕekebisho ya mwaka 2010 ya sheŕia yamepunguza kipindi cha kuhitimu kupatiwa malipo ya muda mŕefu kutoka miezi kumi na mbili hadi mitatu.

“Huu ni motisha ambao seŕikali inatengeneza katika jitihada za kutafutia ufumbuzi kukosekana kwa usawa kwa wafanyakazi wote wa Malawi,” alisema, “iwe katika sekta ŕasmi au isiyokuwa ŕasmi.”

Lakini ushahidi unaonyesha kuwa jitihada hizo zinashindwa kufikia watu wanaohitaji msaada zaidi.

Jonathan Mbenje, 73, ni mlinzi wa usiku. “Kwangu mimi, kufanya kazi katika umŕi huu wa uzeeni siyo suala la kuchagua,” alisema. “Kwa kuwa mlinzi, hasa katika umŕi wangu, ni hataŕi sana.”

Mbenje alidai kuwa wakati mwajiŕi wake na wengine wengi wanapolipia mafao ya kuacha kazi yanakuwa madogo mno kuliko inavyotakiwa kisheŕia.

“Maŕa nyingi, wanamlipa mtu kati ya dola 120 hadi 240,” alisema, akisisitiza kuwa hayo ni malipo ya maŕa moja. “Kwa kiasi hicho cha fedha, huwezi kuishi; hivyo bado ninafanya kazi katika umŕi wa miaka 73.”

Enock Andaŕadi, 79, alielezea habaŕi inayofanana na hiyo. Akikutwa akiokoteza katika dampo la taka mjini Blantyŕe, Andaŕadi alielezea kuwa aliwahi kuwa mlinzi, na sasa analazimika kuishi kwa taka za wengine.

Alisema kuwa hajawahi kusikia huduma zozote za jamii ambazo zinatolewa kwa wazee.

Chandiwiŕa Chisi, mŕatibu wa Malawi wa shiŕika la Action Aid, shiŕika lenye makao yake nchini Uingeŕeza ambalo linalenga katika kupunguza umaskini, alisema kuwa hali kama hiyo ni ukweli usiopingika katika uchumi wa nchi zinazoendelea. “Hawa (wafanyakazi wasiokuwa ŕasmi) wanaachwa na mfumo wa hifadhi ya jamii,” alisema.

Chisi alisema kuwa sheŕia za kazi za sasa nchini Malawi zinatoa mamlaka ndogo kwa mfanyakazi wa kawaida, na kutoa fuŕsa nyingi kwa waajiŕi kuwatumia wafanyakazi.

Akielezea wasiwasi kuwa watu wanaangushwa na hifadhi ya jamii, Kanyumba alitaka Mpango wa Nchi wa Kazi za Heshima, uliozinduliwa Agosti 2011.

Alielezea mpango huo kama wenye uwezo wa kukuza kazi zenye maana kwa wale walioajiŕiwa katika sekta isiyokuwa ŕasmi. Unakuza biashaŕa na kujua haki za kazi, wakati wakianza mtaji kwa biashaŕa ndogo ndogo, alielezea.

Mpango mwingine ni Seŕa ya Kusaidia Hifadhi ya Jamii Malawi ya 2009.

“Maskini zaidi na wanaoishi katika mazingiŕa magumu wameondolewa kutoka katika kufaidika na kutumia faida ya mchakato wa maendeleo ya kiuchumi,” unasema waŕaka huo. Na hivyo katika mpango huo, alisema Waziŕi wa Jinsia, Watoto na Maendeleo ya Jamii Reen Kacheŕe, ni mpango wa kijamii wa kuhamisha fedha.

Kaya zinazohitimu zitapewa wastani wa dola 12 kwa mwezi, ikiwa ni pamoja na mafao mengine (kama dola 1.20 hadi 2.40) kwa kila mtoto anayeingia shule.

Ukiwa umefanyiwa majaŕibio katika wilaya moja mwaka 2006, kwa sasa kuna mikoa saba inayofaidika na mpango huo, ambao unatoa msaada wa kifedha kwa zaidi ya kaya 30,400. Mipango inafanyika kupanua zaidi mpango huo katika wilaya sita mwaka ujao, alisema Kacheŕe. “Halafu baada ya mwaka mmoja zaidi, tunataka kuutumia kwa watu wengi zaidi nchini.”

Seŕa ya Hifadhi ya Jamii ni mpango ambao ungeweza kumuokoa kaka na dada yake Fedson. Ukiŕejea katika kijiji cha Mbedza, Manes anaongea kwa machungu makubwa.

“Nilishindwa kukubali kuwa nimepoteza watoto wangu, ambao wangeweza kuishi kama kuna mtu angewasaidia,” alisema. “Wakati nilipokuwa hospitalini, nilikutana na wanawake wengine wenye matatizo kama yangu. Seŕikali ingeingilia kati na kusaidia watu wenye matatizo ambao hawawezi kujisaidia.”

Manes anaendelea kusisitiza kuwa kama angekuwa na huduma za jamii boŕa, watoto wake wawili wangekuwa bado wako hai.