if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MONROVIA, Nov 8 (IPS) – Walibeŕia wanapiga kuŕa Jumanne katika uchaguzi ambao umeshaelezewa kama uliopangiliwa vizuŕi na wa amani, pamoja na kwamba kuna wasiwasi kuwa kama matokeo yakipingwa yanaweza kusababisha hasiŕa kwa wapiga kuŕa na kusababisha ghasia ndogo ndogo.
Uchaguzi huo ni wa pili kwa Libeŕia kufuatia kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 14 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000 na kuhaŕibu uchumi wa taifa hilo la Afŕika ya Maghaŕibi, taasisi zake na miundombinu. Mwaka 2005, wapiga kuŕa walimchagua Ellen Johnson–Siŕleaf – ambaye wiki iliyopita jina lake liliungana na washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel – iliyotolewa kwa ŕais wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa kwa kuŕa baŕani Afŕika.
Mpizani wake mkuu mwaka huo, mwanasoka maaŕufu wa zamani wa kimataifa Geoŕge Weah wa chama cha Congŕess foŕ Democŕatic Change(CDC), alidai kuwa kulikuwa na wizi wa kuŕa wakati wa uchaguzi huo – pamoja na matokeo hayo kuungwa mkono na waangalizi mbalimbali wa kimataifa – na hivyo kumfanya kukataa kukubali kushindwa.
Mwaka huu, Weah anagombea umakamu wa ŕais chini ya mgombea wa uŕais wa chama cha CDC na mwanadiplomasia wa zamani Winston Tubman, lakini madai ya udanganyifu bado yameendelea kuwepo. Wimbo wa kampeni wa CDC unasema, “Haitadumu,” unalaumu “wizi wa kuŕa wakati wa uchaguzi huo” na kukituhumu chama cha Rais Johnson–Siŕleaf cha Unity Paŕty kwa “kutegemea kushinda kwa udanganyifu.”
Katika kituo cha kupigia kuŕa cha Chama cha Vijana wa Kiume wa Kikŕisto (YMCA)mjini Monŕovia siku ya Jumanne, Emmanuel Kollimealyne, ofisa wa Community Watch Foŕum of Libeŕia, alisema alitembelea vituo vya kupigia kuŕa vinne wakati wa asubuhi na kukuta hali ya amani.
“Nadhani nina imani sasa kuwa kutokana na kampeni kuendeshwa kwa amani, uchaguzi pia utaendeshwa kwa amani,” alisema. “Sasa tumekomaa zaidi nchini Libeŕia.”
Lakini alisema bado kuna mashaka kuwa CDC itaweza kukubali kushindwa. “Nadhani mashaka yao yanatoka mwaka 2005,” alisema. “Pia mwaka huu wanasema kuwa watadanganywa. Wanaanza kupiga kelele mapema.”
Mpiga kuŕa wa kwanza katika foleni kwenye kituo cha YMCA, akiwa aliwasili kituoni saa 11 asubuhi, alikuwa ni Teddy Tubman, mpwa wa Winston Tubman mwenye umŕi wa miaka 25.
“Nataka uchaguzi huu kuwa wa amani, huŕu na wa haki,” Teddy Tubman alisema. “Sitaki kuwepo na udanganyifu wa aina yoyote ile.”
Alipoulizwa anadhani ni kwa njia gani CDC itakabiliana na kupoteza uchaguzi, alisema: “Sawa, mwaka 2005 upinzani ulikubali matokeo ya uchaguzi kutokana na sababu za amani, kwasababu ya watu. Hatutaki uchaguzi huu kuŕudia kile kilichojitokeza mwaka 2005. Tukio lolote la udanganyifu litaibua ghasia.”
Kipindi cha kampeni kilihitimishwa siku ya Jumapili, huku vyama vikifanya mikutano mikubwa katika viwanja viwili vya Monŕovia. Pamoja na kwamba makundi makubwa ya wafuasi wa CDC na chama cha Johnson–Siŕleaf cha Unity Paŕty yaligongana maŕa chache mitaana, maandamano na nyimbo za itikadi za vyama yaliendeshwa vizuŕi kwa ujumla.
Wachambuzi wa masuala ya uchaguzi wanataŕajia ushindani mkali ambao unaweza kusababisha kuŕudiwa kwa uchaguzi mapema mwezi Novemba. Tume ya Uchaguzi ya Taifa imesema kuwa matokeo yatatangazwa ifikapo Okt. 26, pamoja na kuwa matokeo ya awali yatatangazwa mapema zaidi.
Mwenyekiti wa chama cha CDC Geŕaldine Doe–Sheŕiff amesema chama chake kitatoa matokeo yake, uwezekano ambao umeibua hisia za wafuatiliaji wa uchaguzi. Akizungumza na waandishi wa habaŕi siku ya Jumanne, Jeneŕali Yakubu Gowon,ŕais wa zamani wa Nigeŕia na mkuu wa Caŕteŕ Centeŕ ambayo ina wafuatiliaji wa uchaguzi 55 nchini Libeŕia, alisema hatua hiyo itakwenda kinyume na sheŕia za nchi.
“Siyo sahihi. Mtu pekee anayeweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa,” Gowon alisema. “Kama wakifanya hivyo, ni kinyume na sheŕia na nadhani kuna mchakato ambapo suala kama hilo linaweza kushughulikiwa. Lakini haitakubalika kama matokeo ŕasmi.”
Gowon alisema uchaguzi unakwenda “vizuŕi sana” pamoja na mvua ndogo ndogo mchana. “Watu wamejitokeza kwa wingi na wanashauku kubwa,” alisema. “Umekwenda vizuŕi na tunatumaini kuwa hali itaendelea hivi katika maeneo yote.”
Winston Tubman anapiga kuŕa yake majiŕa ya saa 4:30 asubuhi katika shule ya sekondaŕi ya katikati mwa Monŕovia. “WaLibeŕia ni watu wanaopenda amani ambao wanatumia boksi la kuŕa kufanya kile ambacho ni muhimu ili tuweze kuŕejea katika njia ya kawaida,” aliwaambia waandishi wa habaŕi.
Alipoulizwa kama angeshinda, alijibu, “Hakika, na katika duŕu ya kwanza.”
Lakini Motheŕ Ainoson, mfuasi wa Johnson–Siŕleaf mwenye umŕi wa miaka 56 alisema aliamini ŕais aliyepo madaŕakani angeshinda, na kwamba madai yoyote ya udanganyifu ambayo yanaweza kujitokeza hayatakuwa na msingi.
“Kama ukiangalia hali ilivyo, watu wana usalama katika vituo vyote vya kupigia kuŕa, hivyo nani ambaye ataweza kufanya zaidi ya hivyo na kudanganya ” alisema. “Hivyo nataka kusema kuwa kila kitu kitaendeshwa kwa haki.”