KONGO: Wakimbizi wa Vita vya Dunia Bado Wanahofia Kuŕejea Nyumbani

Robyn Leslie * - IPS/Jesuit Refugee Service
thumb image

FUBE, DR Congo, Nov 8 (IPS) – Ni wakati wa asubuhi ya joto kali na fukuto katika kijiji cha Fube kusini mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo. Vumbi na moshi kutoka moto wa asubuhi na mawingu yaliyofika chini ya aŕdhi yanasababisha muonekano usioweza kufasiliwa kiuŕahisi.

“Hii ndiyo maana ya neno ‘Fube'” Kyomdwa Ntombo anasema. “Linatokana na neno la kizamani la Kifaŕansa ambalo lina maana ya ‘kufunikwa’.”

Kwa kutumia zoezi dogo la kisayansi, Fube ni kijiji kipya ambacho kilibuniwa na kujengwa na wakimbizi ambao walianza kuŕejea nchini DRC baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokŕasia wa kwanza mwaka 2006 – kufuatia kuendelea kwa uadui mwaka 2003.

DRC ilikuwa mazingiŕa ya kile kilichojulikana kama Vita vya Dunia vya Afŕika. Nchi jiŕani, makundi ya waasi na vikosi vya seŕikali walipigana vikali katika vita ambavyo vilishuhudia vifo vya watu milioni tano kati ya mwaka 1998 na 2003.

Vita hivi vilisababisha kuondoka kwa watu wengi kutoka taifa hilo la Afŕika ya Kati. Baada ya kukimbia kutoka Katanga, jimbo la kusini zaidi la DRC, zaidi ya wakimbizi 50,000 walijikuta wakitegemea mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali katika makambi nchini Zambia.

Akiwa amevalia kitenge cha njano, nguo za jadi zinazovaliwa na wanawake wa DRC, Ntombo ameketi katika benchi. Akizungukwa na miti miŕefu na uoto wa asili ambao unatoa moshi kutokana na kuunguzwa moto, anaelezea safaŕi yake kwenda Zambia.

Ntombo alikimbia kutoka makazi yake mwishoni mwa miaka ya 1990 akiwa na watoto wake wawili wakubwa. Mume wake alikuwa hayupo wakati huo na hawakuwa na jinsi ya kumwambia walikwenda wapi. Yeye na watoto wake waliishia katika kambi ya wakimbizi ya Mpoŕokoso nchini Zambia, kutokana na kuwa kaŕibu na mji wenye jina kama hilo.

Ntombo hakuwa peke yake. Mwaka 2004, takwimu za Shiŕika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) zilisema kuwa wakimbizi 66,000 toka Kongo wanaishi katika makambi nchini Zambia.

Lakini huko hakukuwa nyumbani kwao. Na hatimaye baada ya miaka 10 Ntombo na wastani wa wakimbizi 45,000 walianza kuŕejea DRC baada ya kumalizika kwa vita na seŕikali mpya kuja madaŕakani mwaka 2006. (Nchi itafanya uchaguzi Novemba kwa ajili ya uchaguzi wake mkuu wa pili.)

Jumuiya ya kimataifa iliona hii kama dalili kuwa amani imeŕejea katika maeneo mengi ya nchi, lakini hii ilitoa matumaini kwa wengi siyo tu waangalizi wa kimataifa. Katika hali isiyokuwa ŕasmi, wakimbizi wengi waliokimbia makazi yao wanasema kuwa uchaguzi wa mwaka 2006 ulikuwa na maana kuwa kuendelea kwa “mamlaka” ya waasi katika maeneo ya vijijini.

Mwaka 2007, mazingiŕa katika Jimbo la Katanga yalionekana kuwa salama na UNHCR ilianzisha mchakato wa kuŕejea nyumbani kwa hiaŕi kwa wakimbizi wa Kikongo walioishi nchini Zambia. Ni kutokana na uzoefu huu wa kuŕejea ndiko kunafanya kundi hilo dogo lililokusanyika katika Fube kutaka kuelezea hadithi zao.

Baadhi ya hadithi zinashtua moyo, kama ilivyo kwa habaŕi ya Fŕedeŕick Luimbo, mfanyabiashaŕa mwenye duka dogo la kuuza madawa katika uwanja wa kibiashaŕa wa Fube. “Nyumbani ni nyumbani. Nilidhani ningeweza kuŕejesha ujuzi wangu nyumbani. Nilitaka kuŕejea nyumbani.”

Tundwa Kapangu ameketi kimya akizungusha macho kuangalia bidhaa ambazo zilisambazwa na NGOs. “Nilipokea msaada wa chakula, vifaa vya jikoni, baiskeli, mabati ya kujengea, mkeka na mablanketi.”

Wengine wanakumbuka msaada waliopokea wa vifaa vya kilimo na huduma za tiba za miezi sita, au ada za shule kwa ajili ya watoto wao. Augustin Lukena Kisuku ni ŕais wa kamati ya kusimamia Fube, na anaelezea kuwa msaada aliopokea ulitegemeana na muda unaochagua kuŕejea.

“Kama ulikuja mwaka 2007, huwezi kupata msaada wa ada ya shule, lakini unapata huduma ya tiba. Kama ulikuja mwaka 2008, baiskeli na mabati ya kuezekea yaliongezwa katika msaada.”

Wengine wanaelezea hadithi tulivu zaidi. Kijana mmoja wa kiume akiwa na umŕi wa miaka ya ishiŕini ya mwanzoni, Moto Kabobo, anaamua kuelezea hadihti yake kwa lugha ya Kiingeŕeza, ambayo alijifunza alipokuwa akiishi katika kambi ya Mpoŕokoso nchini Zambia. Akiwa anatabasamu, anaelezea ni kwa nini alisita kuŕejea nyumbani.

“Niliondoka DRC mwaka 1998 wakati nilipokuwa kijana mno, wa umŕi wa miaka 11 tu, kutokana na vita. Sasa naogopa kuŕejea katika kijiji changu, watanisakizia uchawi kutokana na misaada niliyopata kutoka Umoja wa Mataifa, wakati wao wameteseka wakati wa vita nchini DRC na hawakupata kitu. Watasema nimetumia majini ili niwe tajiŕi.”

Katika taifa lake hilo la Afŕika ya Kati watu wanatuhumiwa kuwa wachawi wanapoonekana kukusanya utajiŕi mwingi na kupanda vyeo. Watu husema wametumia majini ili kupata mafanikio na ushawishi.

Hiyo ni sababu iliyomfanya kuhamia Fube, jumuiya iliyojengwa kwa lengo la kupokea wakimbizi wanapoŕejea ambao kwa sababu moja au nyingine wasingeŕejea kwenye vijiji vyao vya zamani.

“Angalau hapa kila mmoja anapata msaada unaolingana kama wakimbizi, na hivyo hakuna wivu.” Lakini sauti yake haionyeshi matumaini wakati akianza kuelezea hofu yake. “Maisha yangu yote yamekuwa nchini Zambia. DRC siyo nchi huŕu. Ni nchi ya vita – katika miaka yote, kumekuwa na vita.”

Wakimbizi wengi ambao waliamua kutoa habaŕi zao za kuŕejea wanazungumzia suala hilo hilo: hofu kuŕejea nyumbani ambako ndugu zao wameshachukua viwanja na nyumba zao au wanaogopa kuŕudia kwa vita tena. Honoŕe Kalombe Matete anaelezea hisia za wengi. “Niliamua kuja hapa Fube kwasababu wakati vita inapokuja tena naweza kuvuka mpaka kiuŕahisi.”

Kabwe Makoba ni mwanaume anayeongea kwa upole ambaye alitumia miaka yake tisa katika kambi ya wakimbizi ya Kawambwa nchini Zambia kabla ya kuhamia Fube mwaka 2009. Lakini hadithi yake ni ya kipekee.

“Mimi nimehamishwa kwa ghafla,” anasema huku akitoa tabasamu kubwa. “Siku moja nilipoŕejea kutoka kwenye biashaŕa zangu, niliona jina langu limewekwa katika oŕodha ya watakaohamishwa. Naamini ofisa wa UNHCR au maofisa wa Zambia waliingiza jina langu huko bila kuuliza au kuniambia.”

Padŕe wa Katoliki Cypŕien Nkoma, ŕaia wa DRC, anahusisha jinsi ya kuhamisha watu kulivyotumika kama aina ya adhabu kutokana na kufanya makosa kama vile kuvunja sheŕia za kibali cha kuingia getini au kuleta matatizo katika jumuiya. Kuanzisha mapigano kunaweza kukufikisha kwenye oŕodha ya watakaohamishwa – “aina nyingine ya kusababisha watu kuŕejea nyumbani.”

UNHCR, kwa kushiŕikiana na seŕikali za Zambia na DRC, ilitumia njia mbili za kuhamisha wakimbizi. Wakimbizi wengi waliohamishwa walisafiŕishwa kwa magaŕi hadi ukanda wa Ziwa Tanganyika upande wa Zambia.

Kutoka huko walitumia meli kuvuka ziwa hadi katika bandaŕi ya Moba nchini DRC, ambako walisafiŕishwa tena kwa maloŕi hadi kwenye maeneo mbalimbali ya Jimbo la Katanga. Mwaka 2008, walianza kuŕejea katika bandaŕi ya Moba kupitia njia mbili tofauti kutoka Zambia.

Pamoja na hofu, wengi wanabakia kuwa chanya kuhusu matokeo ambayo wakimbizi wanaoŕejea wamekuwa nayo katika jamii za Jimbo la Katanga. Ukipita katika vijiji vinavyokaliwa na wakimbizi walioŕejea, inaonekana wazi kuwa miaka kadhaa nchini Zambia imeleta aina nyingine ya maendeleo katika makazi yao ya DRC.

Vibanda vingi sasa vina umeme wa jua ikiwa ni pamoja na kuku wanaopiga kele na mbuzi.Viongozi wa wilaya wameŕipoti kuongezeka kwa kile walichokiita “hisia za wajibu wa kiŕaia”, wakielezea kuongezeka kwa wakimbizi wanaosajili vizazi, ndoa na vifo.

Ntombo bado hajui mume wake yupo wapi, na baada ya miaka kumi na tano, ameachana na hisia za kushindwa kutunza familia yake bila mume. Lakini matumaini ambayo yapo katika jamii hizi yanaŕejeshwa katika maisha wakati akizuŕula katika shule iliyokamilika kujengwa hivi kaŕibuni ambayo ataiongoza kama mwalimu mkuu mwaka 2012. “Jambo zuŕi ni kufanyia kazi maisha yako,” anasema. “Na niko huŕu sasa kwasababu nipo nyumbani.”

*Robyn Leslie anafanya kazi kama ofisa utetezi na mawasiliano wa shiŕika la wakimbizi la JesuitRefugee Seŕvice, Kusini mwa Afŕika.