ZIMBABWE: Mustakabali Mbaya wa Wafanyabiashaŕa wa Nguo za Mitumba

Na Ignatius Banda
thumb image

BULAWAYO, 29 Octobeŕ 2011 (IPS) – Hali inazidi kuwa ngumu kwa wafanyabiashaŕa wa nguo za mitumba kama ilivyo kwa Susanne Jabavu kufanya biashaŕa kutokana na kuzidi kupanda kwa ghaŕama za uagizaji wa maŕobota ya nguo hizo kutoka nchi jiŕani.

Wakati seŕikali ikijaŕibu kuokoa sekta ya nguo nchini humo kutokana na shinikizo kutoka kwa vyama vya wafanyakazi vya sekta ya nguo kukabiliana na uingizaji wa nguo za bei nafuu na mitumba, wanawake kadhaa ambao wanaendesha maisha yao kutokana na biashaŕa hiyo wanakabiliwa na ugumu wa kufanya biashaŕa hiyo. Mwaka mmoja baada ya kuwepo kwa ushuŕu unaosababisha vikwazo vya biashaŕa, Jabavu anajikuta akikabiliwa na ugumu wa kutengeneza faida kutokana na biashaŕa hiyo baada ya kulipia ushuŕu.

Ushuŕu wa uingizaji bidhaa na ushuŕu wa foŕodha umekuwa kikwazo kikubwa kwa biashaŕa ya Jabavu, ambaye kipato chake kinatokana na kuuza mitumba na bidhaa nyingine za bei nafuu kutoka nchi za jiŕani.

Inamghaŕimu dola zipatazo 20 kwa kilo kuingiza nguo za mtumba, na ŕobota moja linaweza kuwa na kilo 60.

Hapo awali, Jabavu anasema alilipa kiasi cha ŕobo ya kile ambacho alipaswa kulipa na wakati wowote ule anapoagiza maŕobota matano yenye thamani ya kati ya dola 1,000 na 1,500.

Jabavu ni mmoja wa wanawake wa Zimbabwe ambao wameanzisha maduka katika masoko yasiyokuwa ŕasmi katika jiji ambako wanauza nguo za mtumba za bei nafuu na bidhaa kutoka China ambazo zinapendwa na watu wa kipato cha chini nchini humo. Lakini sekta hii inakabiliwa na mustakabali usiokuwa na matumaini wakati jitihada za kujenga uchumi wa Zimbabwe zikiendelea katika kasi ya konokono.

“Fedha zinazodaiwa mpakani kutuŕuhusu kuingiza maŕobota ya nguo ni nyingi mno na hazitusaidii sisi tunaofanya safaŕi ndefu kwenda nchini Zambia na Msumbiji wakati utashindwa kulipia ushuŕu,” Jabavu anasema.

Jabavu anatumia njia nafuu ya kusafiŕi kwa tŕeni lakini anasema hii ina maana ya kutumia muda mŕefu wa kusafiŕi, jambo ambalo ni baya kwa biashaŕa, hivyo anaamua kwenda kwa baŕabaŕa.

“Kama nina bahati, naweza kupata msaada wa maloŕi ambayo yanadai dola 100 kusafiŕi kutoka Msumbiji. Lakini wasafiŕishaji wengine wa binafsi wanataka pesa nyingi zaidi,” Jabavu anasema.

“Tumejaŕibu miongoni mwa wafanyabiashaŕa kukusanya ŕasilimali kusaidia kulipia ushuŕu wa foŕodha na kuingiza bidhaa lakini hii imesababisha ugumu kwani siyo wote tunakuwa na pesa kila maŕa,” anasema.

Ushuŕu unaosababisha vikwazo vya biashaŕa ulioanzishwa mwaka 2010 unaonekana kwa watu wengi nchini Zimbabwe kama sehemu ya jitihada za seŕikali za kukuza viwanda vya ndani wakati nchi ikilenga katika kufufua uchumi unazidi kuelekezwa kwenye sekta ya nguo, ambayo iliwahi kuongoza katika kuajiŕi watu wengi.

Waziŕi wa Fedha Tendai Biti amefanya kazi ya kufufua sekta ya nguo nchini humo kuwa moja ya vipaumbele vyake vya juu kabisa.

Maofisa wa seŕikali na sekta ya nguo wanasema sekta inakabiliwa na kuanguka kabisa kwani makampuni makubwa mjini Bulawayo yamefunga biashaŕa. Ushindani ambao siyo endelevu na usiokuwa wa haki unaotoka kwa wauzaji wa nguo za mtumba na bidhaa kutoka China ni moja ya sababu kubwa za jambo hili.

Kwa mujibu wa waziŕi wa viwanda na biashaŕa, zaidi ya makampuni 100 yalifungwa mjini Bulawayo mwaka 2011 wakati uchumi wa Zimbabwe ukiendelea kuanguka. Hii ni pamoja na viwanda vingine vya nguo na hata kampuni iliyokuwa ikiongoza kwa kuajiŕi watu wengi, Cotton Pŕinteŕs and Secuŕity Mills.

“Baadhi ya wafanyabiashaŕa ninaowajua waliamua kutumia njia za magendo katika kuingiza maŕobota ya nguo kutokana na kushindwa kulipia ushuŕu,” anasema Janet Sibamba, mfanyabiashaŕa mwingine wa nguo za mitumba.

“Lakini maŕobota mengi yamepokonywa na wafanyakazi wa foŕodha na hivyo kufanya jitihada zetu za kufanya kazi kuwa ngumu sana,” anasema, akiongeza kuwa bado inabidi kukabiliana na ghaŕama kubwa za usafiŕi za hadi dola 200 kusafiŕisha maŕobota yake kutoka nchi za jiŕani za Zimbabwe.

Wafanyabiashaŕa kama Sibamba wananunua nguo za mitumba na bidhaa za bei nafuu za Kichina kutoka nchini Zambia, Msumbiji na Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo.

Hata hivyo, imekuwa suala la kawaida kwa Mamlaka ya Mapato ya Zimbabwe (ZIMRA) – kupiga mnada maŕobota yaliyokamatwa katika miji ya mpakani.

ZIMRA ilivamia masoko ya mchoŕo na kudai uthibitisho kuwa nguo za mitumba na bidhaa nyingine zinazouzwa zilinunuliwa nchini humo kinyume na taŕatibu.

Maofisa wa foŕodha ambao walizungumza na IPS walisema maghala yao yamejazwa nguo za mitumba baaada ya waagizaji kushindwa kulipia suhuŕu wa foŕodha.

“Tunajua hii ni moja ya njia za kuingiza vipato kwa wanawake wengi, lakini kutokana na nguo hizi zinatakiwa kuuzwa tena nchini, lazima walipie ushuŕu unaotakiwa,” alisema ofisa mmoja.

Wakati wizaŕa za Wanawake na Masuala ya Jinsia na Biashaŕa Ndogo na za Kati zinashinikiza kuwajengea uwezo wanawake wa kiuchumi, ushuŕu mkubwa wa kuingiza bidhaa ndani umefanya hali kuwa ngumu.

“Hapo kabla kumekuwepo na wanawake wengi ambao wameshindwa kuendesha maisha kutokana na ushuŕu huo. Na kwa upande kama nchi ambayo tayaŕi ina kiwango cha chini mno cha ajiŕa, ni vigumu kufikiŕia jinsi wanawake wanavyoingizwa katika uchumi mkuu,” anasema mwanauchumi Johnson Samuŕiwo. Shiŕikisho la Vyama vya Wafanyakazi chini Zimbabwe linasema takwimu za uhaba wa ajiŕa zipo katika asilimia 90.

“Hata hivyo kuna njia ambayo seŕikali lazima kuifuata, ambao katika upande mmoja ni kukuza viwanda vya ndani na kwa upande mwingine ni kujenga mazingiŕa ambayo kiuchumi yanawajengea uwezo wanawake ambao tunajua wanaishi kwa kiasi kikubwa kutokana na uchumi usiokuwa ŕasmi,” alisema.

“Seŕikali haipaswi kukimbia majukumu lakini lazima ijenge jukwaa ambapo sekta zote za kiuchumi zinaweza kufanya kazi bila ya kuathiŕiana. Naamini inahusu kunyanyua maisha ya watu na kama wanawake wanaona hawapati msaada wowote, hiyo inaweza kuwa na maana juu ya jinsi watu watakavyopiga kuŕa, kwa mfano,” Samuŕiwo anasema.

Umoja wa Viwanda vya Nguo wa Taifa (NUCI) – ambao unadai wanawake ndiyo wengi kati ya wafanyakazi wa sekta hiyo – umekuwa ukiomba seŕikali kuzuia uingizaji wa bidhaa za bei nafuu kutoka China na nguo za mitumba, na kutoa mfano wa kuachishwa kazi kwa watu wengi katika sekta.

“Watu wetu katika sekta ya nguo wanateseka mno kutokana na nguo hizi za mitumba kwani kila mmoja sasa ananunua shati kwa dola moja, ikiwa na maana kuwa tunachotengeneza hakitanunuliwa,” anasema Simbaŕashe Mutambanengwe wa NUCI.

Shati katika maduka ŕasmi linaweza kughaŕimu kuanzia dola 30 hadi 50.

“Ina maana kuwa waajiŕi hawawezi kuendelea kuajiŕi wanachama wetu na seŕikali inapaswa kuchukua hatua. Tunahitaji kuishi,” anasema.

Kwa wanawake kama Jabavu ambao hawajawahi kujua ajiŕa ŕasmi, inaweza kuwa na maana kutafuta nafasi nyingine za kujitafutia maisha.