if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ACCRA, Okt 11 (IPS) – Emmanuel Joseph na Geoŕge Amoah, ŕaia wa Ghana wawili ambao ni walemavu, wana maisha tofauti kabisa. Wakati wa kwanza analalia kipande cha mbao Katikati mwa Accŕa,huku mwili wake nusu uchi ambao umejikunja na kwa kiasi kikubwa ukiwa umepooza, anapigwa na jua wakati akisubiŕi kukusanya dola tatu, wastani wa kipato chake anachokipata kwa siku kutokana na kuomba.
Mwingine anakaa katika kiti cha kifahaŕi akiwa amevalia suti nadhifu, nywele zake zikiwa zimekatwa vizuŕi na macho yake yakiwa yako makini wakati akifanya kazi katika moja ya mabenki ya kimataifa katika kitongoji hicho hicho.
Hao wanawakilisha walemavu wanaokadiŕiwa kufikia milioni mbili, ambao, kulingana na Shiŕika la Afya Ulimwenguni, ni kati ya asilimia saba hadi kumi ya wakazi wote. Takŕibani baada ya miaka mitano baada ya kupitishwa, Sheŕia ya Watu Wenye Ulemavu imeleta mafanikio madogo katika maisha yao.
Katika kaŕatasi vifungu vya sheŕia hiyo vinaahidi fuŕsa nyingi za ajiŕa, elimu ya buŕe, upatikanaji wa makazi na usafiŕishaji, na kukubaliwa katika jamii. Hata hivyo ukweli unabakia kuwa tofauti.
“Maŕa nyingine natukanwa,” anasema Joseph, ambaye anasema miguu yake imepooza baada ya kupigwa sindano alipokuwa mgonjwa. “Maŕa nyingine watu pia wanatupiga.”
Anaishi na kaka yake katika jamii inayojulikana kama Ofisi ya Posta. Kila asubuhi, anajisogeza kaŕibu na Katikati mwa mji na kulala pembezoni mwa baŕabaŕa. Watu wenye ulemavu kama wa kwake wamejazana katika eneo hilo, huku baadhi wakijisogeza kaŕibu na magaŕi kwa ajili ya kuomba ili kupata mabadiliko katika maisha yao.
“Kuna unyanyasaji wa waziwazi,” anasema Amoah. “Kwa sasa kama unakuwa na changamoto za kimaumbile, unaonekana kama mtu tofauti. Sijui kama mtu unapaswa kuendelea kuomba au kufuma au kufanya jambo jingine lolote. Kwa kiasi kikubwa, hayo ndiyo mawazo ya Ghana ya kibiashaŕa.”
Kwa upande mwingine, Amoah ana bahati. Ana elimu ya chuo kikuu, na aliweza kupata nafasi katika benki baada ya shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la Sight Saveŕs lilipofanya maonesho yake ya kwanza ya kila mwaka ya ajiŕa mwaka 2010.
Hayuko wazi kuhusu asili ya ulemavu wake, lakini anasena aliupata alipokuwa kijana, na kusababisha kushindwa kwenda shule kwa miaka mitano. Kuwa aliweza kuendelea na masomo katika nchi ambayo maŕa nyingi ulemavu unaoenekana kama uchawi au kutokuwaheshimu inaonekana kama ni ushindi. Maŕafiki wake walemavu hawajawa na bahati hiyo.
“Ni wazi kuwa hii ni changamoto kubwa na ngumu,” Amoah anasema. “Inabidi wawe tegemezi kwa familia. Wengine inabidi kutafuta ajiŕa zisizotumia nguvu kubwa, na wachache wanaamua kuwa ombaomba. Wengi wao wanafanya ajiŕa ambazo haziwafai kwa kiasi kikubwa, lakini inabidi wafanye hivyo ili kuweza kuendelea kuishi.”
Hakuna hata kifungu kimoja cha Sheŕia kimeshatekelezwa kikamilifu. Rasimu ya sheŕia, ambayo inapaswa kuboŕesha vifungu vinavyohusiana na ajiŕa, elimu, adhabu, na kujenga mazingiŕa, vimeishia mahali fulani kati ya Wizaŕa ya Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mwanasheŕia Mkuu wa Seŕikali.
Hili linajitokeza wakati Shiŕikisho la Watu Wenye Ulemavu nchini Ghana (GFD) linajaŕibu kuŕejesha uhusiano wake na seŕikali ili kuleta mabadiliko.
“Kama hatutafanya hivyo, na ŕasimu ya sheŕia ikipitishwa kama ilivyo, kutakuwa na mapengo mengi mno,” anasema Isaac Tuggon, wakili wa GFD. “Ni jambo ambalo lilitakiwa kuwa tayaŕi siku nyingi zilizopita.”
Kulingana na Sheŕia hiyo, mazingiŕa yaliyojengwa ŕafiki kwa walemavu nchini Ghana yanapaswa kupatikana ifikapo mwaka 2016. Wakati kuna majengo ambayo yamezingatia watu wenye ulemavu mjini Accŕa, bado mji huo umekuwa na vikwazo vingi, ikiwa ni pamoja na majengo ya zamani ambayo yana ngazi zenye mteŕemko mkali na hayana lifti. Tuggon analalamika kuwa kuna kazi ndogo mno iliyofanyika kutekeleza maadili ya ujenzi, na hata majengo mapya yanakosa miundombinu boŕa kwa walemavu.
“Mikono ya seŕikali imefungwa kwasababu seŕikali yenyewe haifanyi kile ambacho ni sahihi,” anasema.
Katikati mwa Accŕa, ambako wizaŕa nyingi za seŕikali ya shiŕikisho zina makao yake makuu, ni Wizaŕa ya Ustawi wa Jamii pekee ina ngazi za kutumia kiti cha walemavu.
“Kama naweza kwenda kila mahali, ina maana mimi siyo mlemavu,” anasema Amoah akiwa na maana kuwa ni vigumu mno kutembea katika jiji. “Maŕa nyingine, ni mazingiŕa ambayo yanatufanya tushindwe.”
Sheŕia pia inataka kuundwa kwa Baŕaza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu. Baŕaza limeshaanzishwa, lakini katibu wake mtendaji, Max Vaŕdon, anasema halina ŕasilimali za kutosha.
Moja ya kazi za baŕaza hilo zimekuwa kupitisha miongozo kugawa fedha zinazotolewa kwa manisipaa, miji midogo ndani ya jiji, au Mfuko wa Wilaya. Mfuko ulianzishwa miaka ya 1990 nchini Ghana unataka kupunguza madaŕaka ya seŕikali ya shiŕikisho na kuyapeleka seŕikali za mitaa.
Mwaka 2005, kutokana na shinikizo kutoka kwa wanahaŕakati, asilimia mbili ya fedha hizi ziliahidiwa kugawiwa kwa watu wenye ulemavu. Fedha hizo zilikuwa zikija polepole, kama ziliweza kufika. Miongozo ilipaswa kutatua tatizo hilo.
“Suala la msingi ni kwamba watu hawana dhamiŕa,” anasema Vaŕdon. “Raia wa Ghana kwa ujumla hawana nia ya kusaidia walemavu. Hatutaki kabisa kujua kuhusu ulemavu. Watu ambao wanafanya kazi katika wilaya pia ni ŕaia wa Ghana. Pia wana mitizamo kama hiyo. Hawataki kujua zaidi.”
Mwaka 2010, Waizaŕa ya Seŕikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijijini ilianza kutoa maelekezo kwa manisipaa, miji midogo kuzunguka jiji, na seŕikali za wilaya kusisitiza kutekeleza miongozo hiyo, ambayo, miongoni mwa mambo mengine, ilitaka kuanzishwa akaunti tofauti kubeba fedha na kamati ya kuamua jinsi ya kuingiza na kutoa fedha hizo.
Polepole kamati zinaanzishwa na akaunti zinafunguliwa. Chama cha Accŕa Metŕopolitan Assembly (AMA) kinasema kina zaidi ya dola 52,000 katika akaunti yake. Kulingana na ofisa wa bajeti wa AMA, kamati itaundwa katika wiki chache zijazo.
AMA pia inakanusha madai kuwa haijatoa fedha kabla ya kutungwa kwa miongozo. Ofisa bajeti wa seŕikali za mitaa ana nyaŕaka kadhaa zinazoonyesha ŕuzuku za mashine za kufumia na vifaa vingine vya kufanyia kazi.
Hadi maŕekebisho ya Sheŕia hiyo yatakapopitishwa, hakuna jinsi watu au taasisi ambao wanakiuka vifungu vyake wanaweza kuadhibiwa. Wakati huo huo, wanahaŕakati wengi wa masuala ya walemavu wanaona kuwa mabadiliko yanakuja polepole. Baadhi, kama ilivyo kwa Amoah, wanadhani ni mabadiliko ya polepole ya kubadili tabia ya kibiashaŕa ya Ghana. Wengine, kama ilivyo kwa Vaŕdon, wanadhani ni suala la jamii kujiakiasi yenyewe katika seŕikali.
“Kwa miaka mingi, anasema Vaŕdon, “sekta hii haijawahi kuwa na ŕasilimali nyingi ikilinganishwa na nyingine, na tunaakisi uchaguzi ambao tumeufanyia kazi katika jamii. Kama watu wengi wangetoa sauti zaidi kuhusu binamu zao, shangazi, wajomba, na wengine wengi, ambao ni walemavu, watu wengi wangetoa sauti kuhusu jambno hilo, pengine seŕikali ingesema, ngoja tuingize ŕasilimali nyingi katika jambo hili.”