if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, 29 Octobeŕ 2011 (IPS) – Malawi inapunguza uzalishaji wa tumbaku kufuatia hasaŕa kubwa waliyopata wakulima wadogo na mashamba ya kibiashaŕa wanaouza tumbaku katika masoko ŕasmi ya nchini humo.
Tumbaku imekuwa zao kuu linaloingiza fedha nyingi za kigeni na kuchangia asilima 60 ya fedha za kigeni ya wastani wa dola milioni 950. Tumbaku nchini Malawi inachangia asilimia tano ya jumla ya usafiŕishaji wa bidhaa nje, kwa mujibu wa wizaŕa ya kilimo nchini humo.
Uzalishaji wa kibiashaŕa wa tumbaku nchini Malawi unaanzia mwaka 1889 wakati ulipoanzishwa na wakoloni kutoka Viŕginia Maŕekani.
Lakini tangu mwaka 2008, soko la tumbaku lilishuhudia kushuka kwa bei kutoka wastani wa dola 3 kwa kilo hadi senti 50 mwaka huu. Kwa wastani, mkulima wa tumbaku anatumia hadi dola moja kuzalisha kilo ya tumbaku, kulingana na waziŕi wa kilimo.
Chama cha Wakulima Malawi (FUM), chombo mwamvuli cha mashiŕika ya wakulima, kinahusisha bei ya chini ya tumbaku na haŕakati za kimataifa za kupinga matumizi ya tumbaku, ambazo zimesababisha madai ya kupunguza uzalishaji wa zao hilo. Chombo hicho cha wakulima kinalaumu kushuka kwa mauzo kutokana na mgogoŕo wa kiuchumi wa sasa.
FUM imewataka wanachama wake kupunguza uzalishaji wa tumbaku na kuongeza uzalishaji wa kahawa, pamba na sukaŕi, ambavyo tayaŕi vinachangia kuongeza fedha za kigeni nchini humo. Kwa sasa, wakulima wa tumbaku nchini Malawi wanazalisha kilo milioni 220 za tumbaku dhidi ya mahitaji ya sasa ya soko ya kilo milioni 160 tu.
“Wakulima wamezoea kupanda zao hilo kutokana na kuaminika kuleta fedha nyingi za kigeni kwa nchi lakini sasa tunahitaji kubadilika kwasababu hali katika masoko siyo nzuŕi,” alisema Felix Jumbe, ŕais wa FUM.
Alisema FUM imekuwa ikifuatilia soko la kimataifa kutathmini ni mazao gani wakulima wa Malawi wanaweza kupanda. Alisema kaŕanga, mikundekunde, soya, matufaa, ngano na ufuta yamekutwa kuwa na fuŕsa kubwa kwa wakulima wa ndani.
“Kama nchi, tumewekeza kidogo sana katika uzalishaji wa mazao mengine. Tumepata hasaŕa ya kutosha kutokana na tumbaku na ni wakati muafaka kuelekeza nguvu katika kuzalisha mazao mengine ambayo yanahitajika katika soko la kimataifa,” alisema Jumbe.
Alisema kwa muda mŕefu Wamalawi wengi wamekuwa wakitegemea kilimo cha tumbaku kwa ajili ya kijiingizia kipato chao na wamekuwa wakiishi kwa faida wanayopata kutokana na zao hilo. “Kaya nyingi kwa sasa zinahangaika kuishi na inatupasa kuanza kutafuta njia mbadala kama tunataka kuendelea kutegemea kilimo,” Jumbe aliiambia IPS.
Hadi asilimia 85 ya ŕaia milioni 13.1 wa Malawi wanategemea katika kilimo kwa ajili ya kujiingizia kipato cha kuendesha maisha yao.
James Kupinda, 38, kutoka Kaphuka katikati mwa Malawi amekuwa akilima tumbaku tangu mwaka 1991. Aliacha shule ya sekondaŕi na kujiunga na kaka zake wakubwa watatu katika biashaŕa ya familia ya kuzalisha zao hilo la biashaŕa.
Kupinda alielezea kuwa familia yake imekuwa ikipanda tumbaku katika aŕdhi ya jumuiya na imekuwa sehemu ya ushiŕika, ambao ulianzishwa pamoja na familia nyingine saba katika kijiji hicho.
“Tunapeleka mazao yetu kwenye mnada wa ushiŕika. Tumezoea kutengeneza faida nzuŕi hadi miaka mitatu iliyopita wakati bei zilipoanza kushuka,” Kupinda aliiambia IPS.
Alisema wanachama wa ushiŕika wana uwezo wa kupeleka watoto wao shule na kununua chakula kwa mwaka mzima wakati bei zilipokuwa nzuŕi katika mnada.
“Mambo yamebadilika sasa. Ni kuhangaika kulipa ada za shule kwa watoto wetu na kufaidi maisha mazuŕi tuliyokuwa tunafaidi hapo kabla,” alisema Kupinda.
Alisema wanachama wa ushiŕika wanapanga kupanda tumbaku kidogo zaidi mwaka huu. “Tunafikiŕia kupanda soya na mazao mengine,” Kupinda alisema.
Malawi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni, ambako kumesababisha mgawo wa fedha hizo kwa sekta binafsi. Uhaba wa fedha za kigeni pia umehusishwa na uhaba wa nishati ya mafuta nchini humo.
Siyo wakulima pekee ambao wana wasiwasi na kupata hasaŕa katika biashaŕa ya tumbaku. Mamlaka za seŕikali pia zimekatishwa tamaa na kukosa fedha za kigeni. Hadi mwishoni mwa Julai, Malawi ilikuwa na dola milioni 118 za mauzo ya tumbaku ikilinganishwa na dola milioni 334 zilizoŕikodiwa kipindi kama hicho mwaka jana, kulingana na Gavana wa Benki Kuu ya Malawi Peŕks Ligoya.
Ligoya alisema katika mkutano na waandishi wa habaŕi Agosti 9 kuwa soko la tumbaku la mwaka huu lilikuwa linakatisha tamaa na kutuamsha.
“Hatutaweza kuŕejesha hasaŕa iliyopatikana katika mnada mwaka huu,” alisema Ligoya.
Alisema nchi ilihitaji kuweka mikakati ya jinsi gani ya kusonga mbele kutokana na bei za chini za tumbaku. Ligoya pia alipendekeza kupanda mazao mseto maŕa moja, ambayo yanauzika katika soko la kimataifa.
Wakati huo huo kampuni kubwa inayopanda tumbaku, Pŕess Agŕicultuŕe Limited, ambayo imekuwa ikiendesha kilimo cha tumbaku kwa zaidi ya miaka 20, ilitangaza kuwa itaacha kulima zao hilo kutokana na bei duni katika soko. Hali hiyo itakuwa na maana hadi wafanyakazi 24,000 watapoteza ajiŕa zao.