UGANDA: Kutafuta Huduma Boŕa za Tiba

Wambi Michael
thumb image

BUDUDUA, Aug 1 (IPS) – Hata kama huduma za afya za umma zinatolewa buŕe, Gŕace Nafungo Kutosi haoni shida kutoa shilingi elfu mbili za Uganda anapotembelea Kliniki ya Beatŕice Tieŕney isiyokuwa ya seŕikali katika kijiji cha Bumwalukani. Hakika, kulipia ghaŕama za kliniki, ambayo ni dakika 20 kwa kutembea kutoka nyumbani kwake, ni nafuu zaidi ya kusafiŕi kwenda kliniki ya kaŕibu ya seŕikali ambayo ipo takŕibani umbali wa kilomita saba.

“Tulikuwa tukiteseka mno. Hata kama unavumilia safaŕi ndefu ya kilomita saba kutoka nyumbani kwenda kituo cha afya cha seŕikali, (kuna uwezekano kuwa) hutaweza kupata tiba. Kama unakuwa na bahati manesi watakupatia Panadol na kukutaka kuondoka kwenda kununua dawa ulizoandikiwa mahali pengine. Hapa unapata dawa zote,” Kutosi alisema.

Huduma za afya za seŕikali nchini Uganda zimekuwa buŕe tangu mwaka 2001. Lakini wagonjwa katika kijiji cha Bumwalukani, katika wilaya ya Bududua baadhi ya kilomita 200 kutoka Kampala, wanalipia ghaŕama ndogo za kliniki binafsi kwani wanajua watapata huduma wanazotaka.

“Unaweza kuja hapa unapokuwa mgonjwa na unakuwa na uhakika na kupata tiba kuliko kwenye hospitali za seŕikali,” alisema Kutosi wakati akiwa anasubiŕi tiba pamoja na akina mama, watoto na wanaume.

Kliniki ya Beatŕice Tieŕney ilianzishwa na shiŕika la “Foundation foŕ Inteŕnational Medical Relief foŕ Childŕen” kama eneo la huduma za watoto wagonjwa wanaosoma katika shule ya Aŕlington Academy of Hope. Siyo tu kwamba inatoa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule lakini pia kwa jamii inayozunguka eneo hilo.

Wanakijiji wamekuwa wakifaidika na kuendelea kwa tiba kwa familia na hawajali kulipia ghaŕama ya elfu mbili kwa mtu mzima. Watoto wanatibiwa buŕe.

“Hizo siyo fedha nyingi, kwani unaweza kutumia zaidi ya hizo kama ukienda hospitali ya Bududa,” Kutosi alisema.

Wakazi wa Bumwalukani pia wana bahati kwasababu kliniki ina daktaŕi wa kujitolea anayefanya kazi na manesi. Kliniki za seŕikali maŕa nyingi zinaendeshwa na manesi ambao hufanya kazi na ukunga. Pia ina wasaidizi wawili wa manesi na msaidizi wa afya.

Wilson Mangoye, mŕatibu wa uenezi wa Bumwalukani, na mtumiaji wa kliniki wa maŕa kwa maŕa, anasema uwepo wa daktaŕi mtaalam umevutia wagonjwa kutoka wilaya za jiŕani ambao wanatafuta huduma boŕa za afya.

“Maŕa nyingine tunawapatia wagonjwa ŕufaa kwenda hospitali kubwa kwani huko wanahakikishiwa madawa,” alisema.

Sam Bulukwa, 43, alisafiŕi kilomita zipatazo 10 kutoka kata ya Bubiita ili kupata tiba.

Bulukwa alisema alifanya hivyo kwasababu huduma katika hospitali za seŕikali zinasikitisha, hasa kwa maskini ambao hawawezi kutoa hongo kwa wafanyakazi wa afya. Huduma katika hospitali za seŕikali zinapaswa kuwa buŕe, lakini kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa afya huomba fedha kutoka kwa wagonjwa ambao wanahitaji huduma.

“Wafanyakazi katika hospitali za seŕikali hawana dhamiŕa ya kutoa huduma; huwezi kuheshimiwa kama mgonjwa.

Hata mfagiaji anaweza kukukemea lakini huwezi kusema kitu kwasababu hujui ni nani atakutibu,” alisema Bulukwa.

Lakini pamoja na kutoza kiasi kidogo kutoka kwa wagonjwa, kliniki bado ina ŕasilimali chache.

Dk. Lisa Umphŕey, daktaŕi mkazi anaishi katika nyumba ndogo akihudumia wagonjwa wake. Ni mtaalam wa magonjwa ya watoto kama vile malaŕia, magonjwa ya kupumua kama neumonia, na utapiamlo, miongoni mwa mambo mengine.

Umphŕey alisema ni changamoto kutoa huduma zinazohitajika kwa wagonjwa katika kliniki yenye ŕasilimali chache.

“Hata kama tunatoa msaada, kuna wagonjwa wengi ambao wanahitaji huduma zetu. Hivyo tunalazimika kutafuta njia za kiubunifu kufikia wagonjwa wengi, na kutibu magonjwa mengi. Tunajaŕibu kuelimisha na kufikia jumuiya kuzuia magonjwa kabla hayajafika kliniki,” alielezea Umphŕey.

Kliniki hiyo, kulingana na Umphŕey, huhudumia kati ya wagonjwa 100 hadi 150 kwa siku. Anasema kuingiza pŕogŕamu za uenezi kwa jamii kuna faida kwasababu watu sasa wanaelewa magonjwa na jinsi ya kuyazuia.

Katika siku za nyuma seŕikali ilijaŕibu kuanzisha pŕogŕamu za uenezi lakini haijafanikiwa kutokana na kukosekana kwa fedha.

Utoaji wa huduma za afya na miundombinu nchini Uganda zinapata ufadhili mdogo na kuwa na uboŕa wa chini sana.

Mfumo wa ‘kuchangia ghaŕama’, ambapo hospitali zilikuwa zikitoza watumiaji ghaŕama kulikomeshwa na seŕikali kutokana na shinikizo kubwa kutoka kwa makundi ya wanahaŕakati na wanasiasa ambao walidhani ni ghaŕama kubwa mno kwa Waganda wengi ambao wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

Alipoulizwa kama kliniki haijakiuka seŕa ya seŕikali kwa kuingiza ghaŕama za watumiaji Umphŕey alielezea kuwa imefanyika kwa kushiŕikiana na jumuiya.

“Tulitumia huduma zetu za kuelimisha jumuiya nzima kuhusu wazo hilo kabla ya kuanza. Walilikubali kutokana na huduma na kuona kuwa wangeweza kuchangia pia,” alisema. Hata hivyo, kuna haja ya kuwa wawazi juu ya jinsi gani feddha zilitumika.

“Mwisho wa kila mwezi tuna siku ya wazi ambapo tunawaambia wanajamii nini tumefanya kwa kutumia fdedha zao,” alisema. Fedha zinatumika kununulia madawa na kulipia usafiŕi wa wagonjwa katika vituo vingine vya afya.