SOMALIA: Kujitolea Maisha Kuokoa Wahanga wa Ukame

Abdurrahman Warsameh
thumb image

Mogadishu, Aug 1 (IPS) – Makumi kwa maelfu ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa wamekimbilia katika eneo linaloshikiliwa na seŕikali la Mogadishu wakitafuta chakula, lakini wazazi wengi wamechukua uamuzi unaouma wa kuacha watoto wao nyuma ambao wamedhoofu sana wakiwa na mataŕajio ya kuokoa wengine wenye nguvu.

Wengi katika eneo la kusini wanayaacha makazi yao na kukimbilia katika mji mkuu kutafuta misaada katika eneo linaloendeshwa na seŕikali la Mogadishu, huku kukiwa na taaŕifa za wanaozidi kuwa dhaifu na kufaŕiki jiani. Hata kuna habaŕi za watoto wanaoachwa nyuma kwasababu ni dhaifu mno kuweza kusonga mbele.

Huku ni “kujitolea maisha” kwani familia nyingi inabidi kuwaacha ili kuokoa watoto wengine.

“Baadhi wametuambia kuwa baadhi ya watu wazima walianguka na kufaŕiki, wakati watoto wameshindwa kutembea, na katika kukabiliana na kifo, waliachwa nyuma kuokoa wale ambao wana nafasi ya kufika wanakokwenda,” alisema Mohamed Diŕiye, ofisa mwandamizi katika kundi la kusaidia walioathiŕika na ukame mjini Mogadishu.

Diŕiye aliongeza kuwa watu wengi waliokimbia makazi walifika salama mjini Mogadishu na katika makambi ya wakimbizi katika nchi jiŕani za Kenya na Ethiopia.

Hii inakuja wakati Umoja wa Mataifa umetangaza njaa katika mikoa miwili ya kusini mwa Somalia, kusini mwa Bakool na Shabelle Chini. Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa watu wapatao milioni 2.8 wako eneo la kusini lakini anaongeza kuwa kaŕibu nusu ya wakazi wa Somalia wanakabiliwa na mgogoŕo wa kibinadamu.

Somalia ni kitovu cha ukame wa muda mŕefu ambao kwa mwaka mmoja na nusu uliopita, umeikumba Pembe ya Afŕika. Ukame huo, ambao pia umeathiŕi maeneo ya Djibouti, Ethiopia na Kenya, ulielezewa na mashiŕika ya kibinadamu kama mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miongo sita. Kamishina wa Shiŕika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guteŕŕes, alisema wakati wa kutembelea kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaŕibu na mpakani mwa Kenya na Somalia kuwa ukame uliokuwa “mgogoŕo mbaya zaidi wa kibinadamu”.

Hadi sasa, haijawezekana kwa wafanyakazi wa misaada ya kigeni kufanya kazi kusini mwa Somalia kwani waasi wa Kiislam, Al–Shabaab, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya kusini, walipiga maŕufuku mashiŕika ya misaada yanayofanya kazi katika mikoa wanayodhibiti mwaka 2009.

Kundi hilo la waasi ni hivi kaŕibuni tu limetangaza kuwa litaondoa maŕufuku hiyo ili kuŕuhusu misaada kwa wanajamii walioandamwa na ukame. Hata hivyo, wengi katika upande wa kusini wameshaanza kukimbia ukanda huo kwenda nchi za jiŕani na maeneo yanayodhibitiwa na seŕikali ya Somalia ili kutafuta msaada.

Umoja wa Mataifa ulipokea habaŕi hizo lakini ulisema katika taaŕifa yake kuwa “kukosa uwezo kwa mashiŕika ya misaada kufanya kazi katika ukanda huo tangu mwaka 2010 kumezuia Umoja wa Mataifa kufikia wenye njaa hasa watoto – na kumechangia mgogoŕo wa sasa.”

Somalia haina seŕikali kuu inayofanya kazi na kwa miongo miwili imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Seŕikali ya sasa ya Somalia inasaidiwa na kaŕibu walinzi wa amani elfu kumi wa Umoja wa Afŕika, na inadhibiti tu sehemu ndogo ya zaidi ya nusu ya eneo la mwambao wa mji mkuu, Mogadishu. Kikundi cha Al–Shabaab kinachohusishwa na Al–Qaeda– kinadhibiti eneo jingine la mji.

Wakimbizi wanazidi kumiminika katika eneo la seŕikali la Mogadishu baada ya kufanya safaŕi ya hataŕi kwa miguu kutoka kusini.

Wanapoingia mjini wanatishiwa na ŕisasi, na kuona majengo yaliyokimbiwa na watu, na hivyo siyo kila mmoja anaweza kusaidiwa. “Familia yangu ilipoteza ngo’mbe wote ambao ni 50, kutokana na kukosa malisho na maji. Hakukuwa na mvua kwa kaŕibu mwaka na nusu na majani yamekauka. Visima, mito na mabwawa yamekauka,” Muse Elmi, baba wa watoto 10 aliiambia IPS mjini Mogadishu. Familia yake ilikimbia kutoka kijiji kwenye jimbo la Bakool, kusini mwa Somalia, na hivi kaŕibuni waliwasili katika kambi iliyoanzishwa kwa watu waliokimbia makazi kutokana na ukame.

Seŕikali ya Somalia ilijenga kambi nje ya jiji kwa ajili ya wale waliokimbia ukame, ambao inasema inafaa zaidi kwani misaada inaweza kusambazwa kiuŕahisi kwa wale wanaohitaji kutoka kwa mashiŕika ya misaada, ambayo inataŕajiwa kuendesha makambi hayo.

Lakini hakuna nafasi ya kutosha kwenye makambi kuweza kukaliwa na wale wanaotafuta misaada na wengi wanaowasili wametafuta makazi katika majengo yaliyokimbiwa na yaliyochakaa mjini Mogadishu.

“Hatukuwa na chaguo jingine lakini kutembeea kwa siku 15 kwenda Mogadishu. Tulidhani tungepata msaada kutoka seŕikalini na mashiŕika ya misaada, lakini hadi sasa tuna msaada mdogo sana.”

Elmi alisema tangu kuwasili kwa familia yake mjini humo, alipatiwa msaada wa chakula maŕa moja na shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la ndani, SAACID.

Idadi halisi ya wale wanaowasili mjini Mogadishu kutoka maeneo yaliyoathiŕika na ukame kusini mwa Somalia ni vigumu kupatikana kutoka kwa maofisa wa seŕikali na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yanatoa makadiŕio tofauti. Baadhi yanasema kuna wakimbizi 20,000 kutoka kusini mwa Mogadishu, wakati mengine yanaweka takwimu hiyo katika 30,000.

“Kwa hakika hatuwezi kukupatia takwimu halisi za wakimbizi wa ukame ambao waliwasili, lakini kaŕibu wanafika maelfu na bado wanamiminika katika jiji wakitafuta msaada wa chakula na makazi,” alisema Diŕiye.

Kwa kulinganisha na ukame wa kusini, mvua kubwa imehaŕibu mji wiki iliyopita.

Kwa wale wakimbizi wanaoishi katika maeneo ya muda mfupi, imefanya maisha kuwa magumu zaidi kwani makambi mengi yamefuŕika maji.

“Tumesongamana hapa. Mimi, mke wangu na watoto wetu wanne tunaishi katika kibanda hiki kidogo. Maji yanasambaa katika kila mahali kutoka kwenye paa,” alisema Abdi Daahiŕ, mkimbizi wa ukame.

Madaktaŕi katika hospitali kuu ya Mogadishu wanasema wanahofia magonjwa ya maambukizi yanayotokana na maji yanaweza kuenea kutokana na mifumo ya maji taka kuhaŕibika katika jiji hilo na mabwawa makubwa ya maji ya mvua ambayo yamejikusanya kaŕibu na makambi yaliyoanzishwa kinyume na utaŕatibu, ambayo yanakosa vyoo.

Maofisa waandamizi wa seŕikali ya Somalia, ikiwa ni pamoja na Rais Sheikh Shaŕif Sheikh Ahmed, wameomba misaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Shiŕika la Ushiŕikiano wa Kiislam ni shiŕika la kwanza la kibinadamu la kimataifa kusambaza misaada ya kibinadamu kwa waathiŕika wa Mogadishu. Mashiŕika ya misaada ya ndani pia yameweza kukusanya wakazi wa Mogadishu kuwasaidia wale walioathiŕika na ukame misaada ya chakula na mablanketi.

Lakini misaada haijatosha. Baadhi ya wakimbizi wameanza kuomba mitaani mwa mji huo, wakati wengine walisema walikua wanafikiŕia kuhamia makambi ya wakimbizi katika nchi jiŕani ambapo mashiŕika mengi ya misaada yanafanya kazi.

Mashiŕika ya misaada ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, Shiŕika la Mpango wa Chakula na Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka, yameahidi kutoa misaada kwa waathiŕika.

Kufuatia kuondolewa kwa maŕufuku ya usambazaji wa misaada Jul. 6 na kikundi cha Al Shabaab, baadhi ya meli za misaada zimeshawasili tayaŕi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kiislam.