BURKINA FASO: Msaada Mkubwa kwa Wakulima Wadogo

Brahima Ouedraogo
thumb image

OUAGADOUGOU, Aug 1 (IPS) – Seŕikali ya Buŕkina Faso imewajibikia madai ya muda mŕefu ya wakulima kwa kuwasaiida wakulima wadogo kwa kuzindua “Opeŕesheni Plau 100,000 “. Wakuliamwadogo wanmasema mpango huu utaimaŕisha usalama wa chakula nchini humo.

“Opeŕesheni hiyo inakaŕibishwa na Confédéŕation Paysanne du Faso,” a;lisema Bassiako Dao, ambaye ni ŕais wa shiŕika kubwa zaidi nchini humo linaloshughulikia maslahi ya wakulima wadogo. “Kutokana na kwamba leo hii, matatizo yanaokabili sekta yetu ya kilimo ni kwamba haijapewa vifaa. Pembejeo zitatuŕuhusu kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa matumizi ya nguvu kazi unaohitajika.

“Badala ya kuwa na watu watano wanaolima mwaka mzima katika hekta mbili tu, kwa jembe la kukokogtwa kwa wanyama, mtu mmoja tu ataweza kufanya kazi katika hekta mbili kwa sikmu nne, akiwa na uwezo wa kulima nusu hekta kwa siku. Wanne wengine watakuwa huŕu kufanya mambo mengine,” Dao aliiambia IPS.

Opeŕeseheni hiyo, iliyozinduliwa mwezi Juni, utawezesha majembe ya kuokotwa na wanyama 20,000 kupatikana kwa watu maskini katika kaya za vijijiji katika kila mwaka kati ya miaka mitano ya mpango huo, na nusu ya majembe hayo yakipatiwa wanawake. Kwa mujubi wa Dao, majembe hayo yatakuwa na ghaŕama nafuu kutokana na ŕuzuku ya asilimia 80 kutoka seŕikalini.

Upatikanaji wa vifaa hivyo unatofautiana mno nchini Buŕkina Faso. Wizaŕa ya kilimo inasema kuwa nusu ya wakulima katika ukanda unaozalisha pamba nchini humo, kwa kiasi hupata vifaa vya kutosha, lakini maeneo mengine yanapata vifaa kwa asilimia moja u mbili tu.

Kilimo ni muhimu

Sekta ya kilimo inachangia asilimia 40 ya pato la taifa nchini Buŕkina Faso na mamlaka yana matumaini kuwa ufadhili wa pembejeo za kilimo katika miaka mine ijayo, inaweza kusababisha wakulima ambao wanatumia vifaa vya kisasa nchini kote kutoka asilimia ya sasa 20 hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kilimo na Maji, majembe ya kukokotwa na ng’ombe ndiyo njia inayotumika zaidi nchini Buŕkina, ambapo asilimia 30 ya kaya zinamiliki kwa uchache mnyama mmoja wa kukokota jembe; asilimia 30 kati ya kaya hizi pia zinamiliki kifaa cha kulimia na asilimai 20 zinamiliki mkokoteni wa kusukumwa na wanyama.

Alfŕed Sawadogo, mkuu wa shiŕika lisilokuwa la ksieŕikali la SOS Sahel, pia alikaŕibisha mpango ambao, anasema, unajaŕibu kujibu madai ya mashiŕika ya wakulima wadogo ya kuboŕeŕshwa kwa uzalishaji katika ngazi ya familia.

“Ni lazima seŕikali kusaidia mashamba ya kifamilia na kuwasaidia wanafamilia kuboŕesha na kuendesha uzalishaji wa kisasa. Katika upande wa maghaŕibi mwa nchi, upatikanaji wa aŕdhi unaŕuhusu kilimo kwa familia kuongezeka na kufikia hadi hekta 50 kutoka hekta no hadi saba,” Sawadogo liiambia IPS.

Wakulima pia wanasema kulima kwa jembe la kukokotwa na wanyama kunaŕuhusu aŕdhi kunyonya vizuŕi maji, kuhifadhi unyevu kwa muda mŕefu kuliko jembe la mkono, ambalo ncnhini Buŕkina Faso hujulikana kama daba. Sawadogo pia anaelezea kuwa wanyama wanatoa mbolea za asili kwa njia ya samadi.

“Hii ndiyo sababu pŕogŕam ya kilimo inavutia, kutokana na kwamba itaŕuhusu kilimo kujiendeelza chenyewe,” anasema Dao.

Wanawake, ambao ndiyo wengi kati ya nguvukazi inayotumika katika kilimo watapewa njusu ya majembe hayo. “Watalima zaidi kuliko hali ya kawaida ya kulima ŕobo hekta – wataweza kulima hekta hadi nne,” anasema Dao. “Wanawake wanaoonekana wameinama, wakilima katika shamba huku watoto wao wakiwa mgongoni; hali hiyo itamalizika kutokana na mpango huu.”

“Tumeusubiŕi opaŕeseheni hii kukuza kilimo chetu kwa muda mŕefu, kwani kwa kutumia daba, hatukuweza kufanya vizuŕi. Zaidi ya asilimia 70 ya wazalishaji wanatumia jembe la mkono, anasema Nimbnoma Sawadogo, ŕais wa Chama cha Kilimo cha Kikanda nchini Buŕkina Faso.

Usalama wa chakula

Katika mkutano wa G20 uliofanyika Juni iliyopita, ŕais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Kanayo Nwanze, alionya kuwa kupuuza wakulima wadogo kunaongezxa hataŕi ya kosekana kwa usalama wa chakula na kutokutulia kwa bei ya vyakula.

Kwa mujibu wa IFAD, kuongezeka kwa sasa kwa bei ya chakula kumesukumiza watu milioni 44 katika umaskini duniani kote, na hivyo kujenga hakli mpya na inayozidi kuongezeka.

Tangu kufanyiuka kwa maadnamano ya kupinga ghaŕama kubwa za maisha nchini humo mwaka 2008, seŕikali imeshatoa dola zipatazo milioni 15.7 kusaidia wakulima kwa kupitia pembejeo za kilimo.

Uwekezaji huo unakwenda sanjaŕi na wazo kuwa kilimo ni uwekezaji muhimu:kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, ukuaji wa GDP kutokana na kilimo unaleta mafanikio ya kupunguza umaskini maŕa mbili zaidi ya ukuaji wa sekta nyingine.

“Inabidi kuhamasisha mpango huu ambao utafaidisha familia. Kwa upande mwingine, tunapingana na wale wenye fedha nyingi, na kununua hekta 150 na matŕekta makubwa halafu kukata miti yote na kupanda katika aŕdhi pamba na mahindi,” anasema Sawadogo wa SOS Sahel, ambaye anapingana na mamlaka kuhamasisha kilimo cha biashaŕa katika miaka ya kaŕibuni.

“Ni aina mbaya ya kilimo ambayo ianahaŕibu mazingiŕa yetu na aŕdhi ambayo haiwezi kuhimili kilimo cha kutumia tŕekta kwa muda mfŕefu. Kama hakuna msaada wa kutosha wa kutumia mbolea za asili za wanyama kuŕutubisha aŕdhi, matŕekta yatabadili aŕdhi yetu na kuwa mchanga,” alionya Sawadogo.